Alivyopoteza utu wake ndani ya Verossa

Alivyopoteza utu wake ndani ya Verossa

AL SADY OLPLANER

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2016
Posts
294
Reaction score
218
Nimeombwa niirudie!

NDANI YA VEROSSA

REPOST: Ndani ya verossa, unaweza kudhani ni gari ya kawaida, ila ndio humo alipopoteza bikira yake, utu na heshima yake.

Ndani ya verossa alitegemea kupata lifti ya kumpeleka nyumbani, humo ndimo alipoahidiwa kazi, maisha mazuri, na kila kitu.

Ndani ya verossa ndimo alipomvua nguo zake na kuzizima kabisa ndoto zake, ndimo alimopoteza degree yake anayoihangaikia mwaka wa tatu huu, haki ya kuwa mke wa mtu na familia.

Ndani ya verossa muathirika mwingine wa UKIMWI aliongezwa katika bajeti ya kuchukua dawa za kupunguza makali ya UKIMWI yaani ARVs. Alimuona kama ni mtu mzima mzuri tu, ana afya njema anaendesha Verossa hawezi kuwa na UKIMWI.

Ndani ya Verossa alimwachia nafasi ya kumgusa, kumpapasa na kumpetipeti. Mshtuko na msisimuko wa raha ulipita katikati ya vena za mwili wake.

Ndani ya verossa alimvua top yake taratibu, ilipofika karibu na kichwa chake akakumbuka maonyo yote aliyokuwa akipewa na mama yake siku zote. Ndani ya verossa akafungua kifungo cha suruali yake ya 'skin jeans' akaacha avuliwe kirahisi kama anabadili nguo vile.

Ndani ya verossa, mama yako anajua? Kwamba mlikuwa siti za mbele sasa mmehamia siti za nyuma na gari mmepaki kwenye kichaka kidogo.

Ndani ya verossa kama gari yako vile msichana mdogo, miguu ukampanulia na kumuacha aiondoe kabisa. Hakuvaa hata 'kinga' na hukumuuliza, ilikuwa raha ee?

Ndani ya Verossa ilikuchukua mwezi mmoja tu kugundua umebeba ujauzito, ulifikiri nini? Hapana siwezi kuwa na mimba! Hey haukusoma 'Reproduction' katika Biologia kidato cha tatu?

Ndani ya verossa, ukaenda kupima afya baada ya miezi miwili. Si ndicho ulichokuwa ukitegemea? Hatimaye ulifaulu vipimo. Ukakutwa na HIV postive yaani umeathirika, mimba ya miezi miwili na ghonorea.

Ndani ya verossa chuoni nako matokeo yakatoka umefeli una supplimentary nne pamoja na carry moja, kiufupi huna chuo tena!

Ndani ya verossa, ulitaka kumpigia aliyekusababishia hayo yote, lakini namba yake haipatikani, ameku block kila sehemu anaendelea kula maisha na warembo wengine.

Ndani ya verossa, unaweza kudhani ni gari ya kawaida, ila humo ndimo alimopoteza bikira yake, elimu yake, utu na heshima. Ndimo alimopoteza haki ya kuwa mke wa mtu.

Inside a Verossa you'd think its some sleek automobile, There she lost her virginity, her dignity and her guile!!!

Hakuna tunu kubwa duniani kama uhai na afya njema, mwenye kusoma asome sana, mwenye kazi afanye kazi kwa bidii, kila mtu ale kwa jasho lake, shortcut always cuts long life.

Dada zetu msipende vya bure vina madhara, mwanaume hua hatoi bure vile alivyohangaikia labda kwa mama yake,mchumba wake, mkewe, au mwanae tu!

Shule bila ada, vaa uniform Twenzetu.
 
Verossa ilipotezaje shule yake " wakati alipata yote hayo akiwa tayari amefanya paper....... Af nyie mnaojiita magreat thinker hivi kwann huo ugreat wenu msiufanye uwape dawa ya ngoma """

Huwa naskitika sana mwafrica kujiita msomi ...
Na wakati huo huo
Hata kutengeneza wembe
HAWEZIIII

Nmejikuta tu naongea haya:

SAMAHANINI KUTOKA NJE
YA MADA
Japo kuna kaukwel kwa ndan iviii!!!!
 
Wanawake wanaojitahid kutunza bikira zao mpka ukubwan wengi wao wanaangukia kwny mikono ya waharibifu wakijakushtukia wameshabebesha takataka kibao...
Pole yake afuate mashart na matibabu ataish milele kupata ukimwi sio mwisho wa maisha
 
Back
Top Bottom