MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Nakata kuelewa, je mnano tarehe 2 sept 2012 kulitokea tukio baya sana la mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel 10 ndugu Daud MWANGOSI kuuawa na mlipuko wa bomu uliotekelezwa na askari polisi. Tukio hili lilitokea wakati huo ikiwa ni jitihada za jeshi la polisi mkoa wa Iringa Kuzuia shughuli za CHADEMA zilizoongozwa na katibu mkuu wa chama wakati huo akiwa Dr Slaa, polisi walizuia shughuli hizo wakidai kua hawakutoa kibali kwa viongozi wa CHADEMA na shughuli hizo zilikua batili kwa Maelezo yao.
Shughuli hizo hazikua tofauti na rapsha zilizotokea miezi mwili iliyopita na kusababisha kifo cha mwanafunzi wa chuo cha NIT Aqwillina Aquilin, najiuliza ni vipi wakati huo kina Dr Slaa hawakukamatwa na polisi na kuswekwa mahabusu kwa kusababisha kifo cha Mwandishi Mwangosi? Ilikuaje ikuaje mpaka leo hatukuona kina Dr Slaa wakiwa mahakamani kujibu tuhuma ikiwa walifanya shughuli baitili kwa mujibu wa jeshi la polisi wakati huo?
Polisi wanamkamata Mh Mbowe na wafuasi wake kwa kosa lipi? Waliandamana wakielekea time ya taifa ya uchaguzi wakiwa na mabango yenye ujumbe gani? hata kama hawakubeba mabango, kwani maandamano kwa tafsiri ya kisheria ya nchi ni kitu gani? Kulikua na haja gani kwa polisi kupiga silaha za moto kutawanya watu wasiokua hata na matawi ya miti mikononi? Kwani form za mawakala zingetolewa kwa wakati hayo yote yangetokea? Mkurugenzi wa Kinondoni angetoa hizo form mapema angepatwa na nini? Tafsi ya neno uasi ni nini?
Kwa hakika, lazima tukubaliane kua tunacheza mchezo ambao unatengenezwa na watu ambao nadhani hawajaifikiria vyema kesho ya vizazi vyao, hakuna uzalendo wowote kwa kuwabambikizia watu kesi zisizowahusu. Tukumbuke kila moja wetu ni kiumbe wa Mungu na anapolia kwa uchungu huku nafsi yake ikisonononeka kwa kuonewa, mtu huyu anaposali na kuomba hakika kuna siku tutashukudia maajabu makubwa sana juu ya mgongo wa ardhi. Uonevu na dhulma hata siku haviwezi kushinda nuru au haki. Tuwadanganye wanyonge kua tunawatetea huku tunawatesa na kuwaonea wachache ambao hawana hatia, ipo siku watatambua dhamira zetu na hakika taifa litazungumza.
Naamini hakuna tena mshikamano ndani ya taifa letu,nuru iliyokuwepo inatokomea kusipojulikana, chuki na hofu vimetanda kila mahali. Huwezi kubeba viongozi wakuu wote wa chama kikuu cha upinzani ambao wana wafuasi zaidi ya million 6, million 2 nchini ya chama tawala halafu unawaweka mahabusu kwa kesi ambayo iko wazi. Tunakolipeleka taifa tutafika huko tunakoelekea.
Tunafikiri tunajenga amani ndani ya taifa ambao lina watu million 50 kwa kuwatia watu hofu badala ya maridhiano na busara kwa kushauriana na kuzungumza juu ya tofauti zetu? Watu million 50 sio na watu million 5 wa taifa la Rwanda, siku wakichukia sijui tutazungumza nini baadae.
Wazee wetu wastaafu wamemaliza muda wao wamekaa kimya hawasemi, kwanini wamekaa kimya? Hivi amgekuwepo Nyerere kwa yanayotokea kwa akili zetu angekubaliana nayo kama mwasisi wa taifa letu?