Jaman yule dada ambae nilimlipia nauli kwny daladala jumapili iliyopita halafu akanipeleka kwa mume wake akaenda kunirudishia....jana tumeonana tena.
Kama inavyofahamika kwa sisi watanzania wengi ukiwa oficn ikafika mida ya lunch utaenda kula lakin lazima ushushie vibia viwili, sasa nna ka chupa kangu mezani mara nikashangaa muhudumu naongezwa bia nyingine wakati hata cjaagiza.
Muhudumu akaniambia:- umeagiziwa na yule mdada....nilipogeuka kuangalia, lahaula" nikakutana na tabasamu kali la yule mrembo, nikampungia tu mkono, huku moyoni nikiamini kwamba hapa sio bure, kukutanishwa nae tena huyu kiumbe.
Na yule jamaa yake aliyenipa ile sh elfu 5 alikuwepo, kwa kuonesha uungwana ili nizidi kumchanganya nikaamua kuinuka kwenda kumsalimia, nilipofika...kwanza kabisa jamaa hakuonekana kutambua uwepo wangu pale (dharau hizo) baada ya salamu sasa kilichofuata.
Mdada akanitambulisha kwa yule mshamba....unamkumbuka huyu mkaka.....jamaa akaniangalia juu mpaka chini halafu akatikisa kichwa kwa dharau kuwa hanifahamu, mrembo akasema huyu si ndo alinilipia nauli cku ile kwny daladala, nikaja nae ukampa sh elfu 5..... jamaa likauliza kwa kashfa sana, kwa hiyo na leo kaja nimpe elfu 5 nyingine......!!!!
Sio siri nilikasirika vibaya sana hadi nikajiuliza cjui nimfumue ngumi kalikali za kushtukiza huku nikichombeza kwa vipepsi vya hapa na pale, lakin kabla cjatimiza azma yangu hiyo, jamaa akainuka kwenda toilet, shati lake likajivuta kidogo
..heeee...!!! nikaiona bastola imetulia kiunoni, nikajua kumbe ndo maana ana dharau sana, hapo nikawa mpole
Jamaa lilipoondoka demu akaniambia:- huyu nae huwa ana mawivu ya kijinga sn, akatoa simu yake fasta akanipa nikawa nishajua cha kufanya muda huo, nikaweka namba zangu, akasema tutawasiliana, nikamalizia bia yangu nikaondoka, lakin bado najiuliza sana kwa upuuzi wa yule mshamba hivi nikimpigia demu wake nitakuwa na makosa kweli, namba ndo tayar nimempa nasubir tu kitakachotokea nitaleta mrejesho hapa.