Alioyasema Ahmedinejad kuhusu 9/11 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alioyasema Ahmedinejad kuhusu 9/11

Discussion in 'International Forum' started by Issaya Kandonga, Sep 25, 2010.

 1. Issaya Kandonga

  Issaya Kandonga Member

  #1
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hotuba ya rais wa Iran kuhusu what was claimed a terrorist attack ya 9/11 huko US yanaweza yakawa na ukweli wowote kweli?

  Sijui huyu jamaa anawaza nini katika cmments zake kuhusu mambo yanayohusu siasa za ulimwengu huu usioisha vita kwa sababu za watu kama yeye wasiotaka maridhiano ya amani bila kuoneshana mbavu ya kijeshi.

  Mmhm me ssemi chochote kwa leo nawaachia nyinyi!
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,465
  Trophy Points: 280
  Rais wa Iran aliyasema hayo ili tuu kuwaprovoke wamarekani na yeye kujionyesha Irani pia ni super power.
   
 3. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Issaya achana nao hao, unaufahamu msemo "Waarabu wa Pemba wanajuana kwa vilemba?" Basi ndio hao Iran na Marekani. Leo hii Iran wakitaka kununua zana za kivita, basi Marekani watawauzia kama vile hakukutokea lo lote vile.
   
 4. Issaya Kandonga

  Issaya Kandonga Member

  #4
  Sep 28, 2010
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hawa jamaa kweli wanajuana kwa vilemba but we have 2 learn from their mistakes tusije laaniwa kama wao!
   
 5. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo ambayo yanatia shaka kuhusu suala zima la kuanguka kwa majengo siku ile na wachambuzi wa majengo na mambo ya milipuko wameshindwa kuelewa ni kwa namna gani majengo yalivyoweza kuanguka kwa style ile tena kwa wakati mmoja,pia kuna mashaka kuhusu mabaki ya ndege zile na nyingine iliyokuwa inaelekea Pentagon kutoonekana wala hakuna mwenye data kuhusu hilo.Mambo hayo ndio yanatia shaka na raisi wa Iran naye ni mmoja wa watu ambao wana shaka na namna ya suala zima lilivyokwenda na kwa kuwa ana uwezo wa kusema kuliko wengine ambao ni waoga mbele ya taifa kubwa kama Marekani.
  Kwa sisi ambao tunaamini kuwa siku ile ni magaidi ndio walifanya vile ni vigumu kuamini aliyoyasema Ahmadinejad ila kwake na wengine bado wana maswali magumu ambayo majibu yake mpaka sasa hayajapatikana.
   
 6. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  hakuna raisi aliyeingiwa na shetani kama ahamadinejad, kwanza kabisa al quaeda wanakiri kwamba wao ndo wamelipua, afu yeye anasema hajalipua kitu...wajerumani wote walishuhudia kuwa holocost ilitokea mbele ya macho yao, yeye anasema haikutokea, hivi ni akili ya aina gani hiyo...wana shida waliompata rais wa aina hiyo. macho ni yetu kuona rais huyu wa iran anapoenda kuteka kaburi la mtume kule wanakoenda kuhiji watoto wa mamamdogo...nuke ikipatikana tu, mandege ya saudia ambayo nchi ya saudia ilinunua Germany kwa kujilinda na iran sidhani kama yatafanya kazi. yetu macho.
   
Loading...