Habari wana Jf.
Kuna imani imetanda miongoni mwa watu kwamba ukioa mwanamke bikira ni vigumu kusalitiwa (mwanamke huyo kuchepuka).
Mwaka 1998 nilihudhuria ndoa ya jirani yangu hapa mtaani ambapo alinihakikishia kwamba yeye ndie wa kwanza kukutana na mke wake kimwili.
Miaka ilisonga na ilipofikia mwaka 2013 jirani yangu huyu aliposafiri kikazi ktk mkoa jirani mambo yalianza kubadilika ambapo mpiga kinanda wa kanisani alianza kumnyemelea mke wa jirani na hatimae kufanikiwa kuvunja amri ya 6 ktk kitanda cha mmewe.
Siri hii ilifichuka baada ya watoto kumwambia baba yao kwamba anaposafiri huja baba mwingine na hulala chumbani kwake.
Mama jirani alikiri kosa na maisha yakaendelea kama kawaida ila ktk hali isiyotazamiwa mama jirani kaingia mtegoni tena na sasa anachepuka na boss flani ambapo mitego imeshategwa inasubiriwa kunasa tu.
Ushauri wangu:-
Kuoa mwanamke bikira sio kigezo cha uaminifu ktk ndoa ila mambo haya ni tabia ya mtu tu.