Alinitapeli lakini kutokana na maisha yake nimeamua kumsamehe

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari za majukumu wakubwa na wadogo..

Nina siku sijapost chochote hapa lakini leo nimeamua nije nishee na nyinyi hapa.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu..
Nilikutana na mdada mmoja mtandaoni fb akanifata messenger na kunisalimia, lakini baada ya salam nikataka kumjua ni nani maana ilionekana kama ananifaham vile.

Ilikua ni siku ya sikukuu ikiyopita ya kiislam, kama ilivyo kawaida ya watu siku hiyo kuombana zawadi na mambo mengine,.. Yule mdada aliniomba sikukuu nami nikataka kujua huyu ni nani maana hakuwa ameweka picha...

Basi akanibu yeye ni wa kipemba ila kwasasa yupo Unguja anasoma Tunguu. Sikua na shaka nae nikajaribu kumuomba picha ili nifaham nae akanitumia,.. Maongezi yalinoga mpaka kufikia hatua ya kuwa wapenzi huku nikiwa namsaidia mahitaji ya chuo kwa mujibu wa maelezo yake,..

Kabla ya kuwa wapenzi nilimsaidia kama ndugu yangu vile kutokana na matatizo yake aliyonieleza maana yalinifanya niingiwe na huruma kumbe nachumia mwanaume mwenzangu.

Ikafikia hatua sasa nikataka tujuane kiundani lakini yeye tatizo lake alikua hapokei videocall wala sauti kwa kisingizio sim yake ni mbovu. Stori ni ndefu sana nimeamua kuifupisha maana nikisema niandike mwanzo mwisho itanichosha.

Sasa nikamshitukia kwamba huyu ananiibia sio bure kuna kitu hapa nikaamua kuingiza mwanampelelezi aifanye hiyo kazi ya kumjua ni nani na anatokea wapi.
Na kweli kazi ikifanyika ndani ya siku 5 nikapatiwa vithibitisho vyote ikiwemo namba za sim, picha yake, majina, nyumbani alikotokea na alipo kwa sasa.

Sasa nikasema ngoja nimpe onyo, nikamtumia sms na kumweleza utapeli alionifanyia nampa siku tatu arudishe hela zangu tofauti na hapo zikipita siku tatu bila kunijibu chochote nitamuanika mitandaoni.

Basi baada ya kuona ujumbe ule ilibidi aniombe radhi na kutaka kunilipa hela zangu lakini wakati huo hana kitu mfukoni. Basi baada kunambia sababu ya kufanya vile huruma zikanijia nikaamua kumsamehe na sasa amekua rafiki yangu tunasalimiana kila leo.

Lakini katika kitu alichonifanyia nimejifunza yafuatayo:-

* Msitiri mwenzio leo na wewe Mungu akustiri kesho yake.

* Samehe ulipokosewa maana hata sisi sote tuna makosa na Mungu anatusamehe tukiomba msamaha.

* Shida ni kwa wote hakuna ambaye amekamilika, leo yeye kesho mimi yatanikuta.
 
kwa hiyo unatushaurije mkuu

Na sisi tutapeli kama huyo binti ?

Tusiwe wapumbavu tunapotapeliwa .. Bora tufanye chochte hata kulipwa nyapu

Au tufanye huruma kama wewe ambazo kimsingi zitazid kulea huu upumbavu kwenye jamii hii

Akitoa jibu mnshtue jaman simu namwachia swalehe achat na bint wake wa kipemba messenger
 
tapeli ni wakiume ila alijifanya wakike
 
Habari za majukumu wakubwa na wadogo..

Nina siku sijapost chochote hapa lakini leo nimeamua nije nishee na nyinyi hapa.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu..
Nilikutana na mdada mmoja mtandaoni fb akanifata messenger na kunisalimia, lakini baada ya salam nikataka kumjua ni nani maana ilionekana kama ananifaham vile.

Ilikua ni siku ya sikukuu ikiyopita ya kiislam, kama ilivyo kawaida ya watu siku hiyo kuombana zawadi na mambo mengine,.. Yule mdada aliniomba sikukuu nami nikataka kujua huyu ni nani maana hakuwa ameweka picha...

Basi akanibu yeye ni wa kipemba ila kwasasa yupo Unguja anasoma Tunguu. Sikua na shaka nae nikajaribu kumuomba picha ili nifaham nae akanitumia,.. Maongezi yalinoga mpaka kufikia hatua ya kuwa wapenzi huku nikiwa namsaidia mahitaji ya chuo kwa mujibu wa maelezo yake,..

Kabla ya kuwa wapenzi nilimsaidia kama ndugu yangu vile kutokana na matatizo yake aliyonieleza maana yalinifanya niingiwe na huruma kumbe nachumia mwanaume mwenzangu.

Ikafikia hatua sasa nikataka tujuane kiundani lakini yeye tatizo lake alikua hapokei videocall wala sauti kwa kisingizio sim yake ni mbovu. Stori ni ndefu sana nimeamua kuifupisha maana nikisema niandike mwanzo mwisho itanichosha.

Sasa nikamshitukia kwamba huyu ananiibia sio bure kuna kitu hapa nikaamua kuingiza mwanampelelezi aifanye hiyo kazi ya kumjua ni nani na anatokea wapi.
Na kweli kazi ikifanyika ndani ya siku 5 nikapatiwa vithibitisho vyote ikiwemo namba za sim, picha yake, majina, nyumbani alikotokea na alipo kwa sasa.

Sasa nikasema ngoja nimpe onyo, nikamtumia sms na kumweleza utapeli alionifanyia nampa siku tatu arudishe hela zangu tofauti na hapo zikipita siku tatu bila kunijibu chochote nitamuanika mitandaoni.

Basi baada ya kuona ujumbe ule ilibidi aniombe radhi na kutaka kunilipa hela zangu lakini wakati huo hana kitu mfukoni. Basi baada kunambia sababu ya kufanya vile huruma zikanijia nikaamua kumsamehe na sasa amekua rafiki yangu tunasalimiana kila leo.

Lakini katika kitu alichonifanyia nimejifunza yafuatayo:-

* Msitiri mwenzio leo na wewe Mungu akustiri kesho yake.

* Samehe ulipokosewa maana hata sisi sote tuna makosa na Mungu anatusamehe tukiomba msamaha.

* Shida ni kwa wote hakuna ambaye amekamilika, leo yeye kesho mimi yatanikuta.
Doh u mpumbavu wa kiwango cha juu!
 
Back
Top Bottom