Alinisaliti, nifanyeje?

Kwani kaka tangu alipokutana na huyo ex na wewe ulivyoreact baada ya kukwambia ameshafanya kitu kama hicho tena? Je kuna kingine ambacho kinaweza kuwa kimeashiria kutokuwa muaminifu?

Kwanza mimi ninaamini kabisa mpaka akwambie wewe ukweli kuwa nilikutana na ex wangu juzi huyu ni mwaminifu sana kwako kwa sababu angeweza kukwambia kuwa hajakutana naye miaka wala hajui alipo. Kaka wanawake huwa tuna tabia ya kupenda kuonekana wasafi so kwa kitendo hicho nampa pongezi wifi kwa kuwa mkweli kwako.

Chunguza kama hakutani naye tena na wala hana dalili ya kutokuwa muaminifu kwako. Kama kosa hilo la kukwambia ukweli ndio doa pekee, please think twice before dumping her kwa kosa hilo

nashukuru lakini hawa ni watu ambao kwa maelezo yake ni kwamba huyo jamaa wake alikuwa mpangaji wao na mpaka sasa ni mpangaji wao. kwahiyo ni watu ambao kwa kuonana tu ni daily kwa sababu wanakatiza korido moja. Ila tu kwa sasa jamaa kaoa. Ila kilichoniumiza sana ni suala la yeye kupokea michango ya harusi ya huyu bwana kutoka kwa waliokuwa shemeji zake hapo nyuma kabla ya kuwa na mimi. Halafu pia wakati wa graduation huyu bwana alikuwepo na hadi kwenye picha za ukumbini ame-appear, nilivyomuuliza akasema Mama yake ndie alieyemualika kama mpangaji wake. Anway kaalikwa na mama yake kwanini akaacha hiyo picha iwepo kwenye albamu yake ambayo mimi lazima ningeiona. Akakosa jibu.
 
wakati tupo chuo niliingia kwenye mahusiano na binti mmoja ambaye tulikuwa tunashare baadhi ya masomo (options). Tulianza mahusiano mapema tu, ila siku moja tukiwa mwaka wa pili likizo ndefu mimi nikiwa nimeenda nyumbani-mkoani. Mwenzangu kwao ni hapa DSM akawa anaendelea na mahusiano ya kimapenzi na bwana wake wa zamani. Baada ya likizo kwisha siku moja ikawa tunapiga story kawaida ikatokea tu tukaanza kuongea kuhusu wapenzi wetu wa zamani. Sijui ilikuwaje tukaanza kuulizana siku za mwisho kukutana nao. SIKUAMINI PALE GIRLFRIEND WANGU ALIPONIAMBIA KUWA NI MWEZI WA SABA, kumbuka hicho kumbuka ndio tulikuwa likizo na tulikuwa tunawasiliana sana hata kuandikiana meseji za TAKE CARE EEH! Nilipomuuliza akaniambia ni kwasababu anajua hatoishi naye, kwahiyo haina athari zozote. Sio siri iliniuma sana ila kwakuwa nilikuwa nampenda tuliendelea hivyo mpaka tulivyograduate. Sasa umefika wakati wa kuanza kufikiria ndoa napata shida kweli kama nitaweza kuishi na mwanamke huyu kwa kuwa yale maumivu bado yapo moyoni mwangu bado. Ingawa yeye anasisitiza kuwa ameshaacha kukutana naye toka kipindi kile kutokana na reaction niliyoonyesha.

Naombeni mnisaidie
Nifanye nini kwani bado inaniuma sana hasa nikikumbuka wakati mimi niko likizo tulikvyokuwa tunawsiliana PLEASE TAKE CARE MY LOVE kumbe mwenzangu inawezekana hata wakati anaandika hizo messeji alikuwa kwenye kifua cha huyo mwanamume!
naona kesi umeivutia kwako pekee. Ingawa mwenzi wake anayo haki ya kusikilizwa nadhani tunaweza kujenga picha ya mwanzo wa mahusiano yenu.
Inaonesha wewe ndiye uliyemshawishi akaachana na bwanake. Kwa hiyo usiumie anapokumbushia pa zamani. Kama ulimkuta idle ungesema wazi ila ktk mwanzo wa statement yako unakiri mmefahamiana kwa kuwa mnasoma pamoja hivyo mojawapo ya malengo yako kwenda chuo ni kusaka mchumba (how nive).

Sasa kwa gia aliyoingia kwako ndiyo gia anayoingia nayo kila mahala vivyohivyo na wewe unatumia gia hiyo hiyo. Nakushauri ujifikirie upya kuhusu mahusiano yenu ukianzia msingi wake...
 
nashukuru lakini hawa ni watu ambao kwa maelezo yake ni kwamba huyo jamaa wake alikuwa mpangaji wao na mpaka sasa ni mpangaji wao. kwahiyo ni watu ambao kwa kuonana tu ni daily kwa sababu wanakatiza korido moja. Ila tu kwa sasa jamaa kaoa. Ila kilichoniumiza sana ni suala la yeye kupokea michango ya harusi ya huyu bwana kutoka kwa waliokuwa shemeji zake hapo nyuma kabla ya kuwa na mimi. Halafu pia wakati wa graduation huyu bwana alikuwepo na hadi kwenye picha za ukumbini ame-appear, nilivyomuuliza akasema Mama yake ndie alieyemualika kama mpangaji wake. Anway kaalikwa na mama yake kwanini akaacha hiyo picha iwepo kwenye albamu yake ambayo mimi lazima ningeiona. Akakosa jibu.

Kaka sipo kwa maelezo yako ni wazi kuwa uhusiano wenu unamiss kitu kiitwacho mawasiliano (communication). Kama mngekuwa na communication kiasi cha wewe kumwambia vitu unavyovipenda na usivyovipenda au vinavyokuumiza ni wazi angechagua moja.

mwambie sipendi unavyoendelea kuhusiana na Ex- wako na ikiendelea hivyo basi hakufai kwani bado atakuwa anamfeel huyo ex.

Relationship yenye communication husaidia kutatua na kuzuai matatizo mbalimbali inawezekana wewe unabakia kuumia ndani kwa ndani ukimwona anaendelea kuwasiliana au hata kusalimiana na huyo ex huku yeye (wifi) akiamini wewe ni very understanding kwa kumruhusu kuendeleza communication na ex (hujamwambia unavyofeel).

Wengine relationship zetu zinakwenda mpaka the extent ya kutosalimiana na ex au waliokuwa wifi/mashemeji zako hata kama mmekutana msibani. Hii sio kwamba tunafanya kwa kuwa tu dhaifu la hasha bali kwa kuwa tunajua (tuliambiwa) kwa kufanya hivyo wenzi wetu hawajisikii vizuri (na kwa nini umwumize mtu umpendaye kwa expense ya alopita?)

Communicate, communicate and communicate more
 
Ni kweli inaonekana kuwa maelezo yangu yanamkandamiz sana huyu binti, ilo siwezi kulipinga hata kidogo. Lakini nasema yale ambayo ni ya kweli kwa upande wangu pasipo kumkandamiza. Ila kuhusu kumuondoa kwa bwanake wa zamani sio kweli. Mimi wakati namtongoza aliniambia alikuwa hana mtu.

...hapo sasa! ...kama uliamini hakuwa na mtu, wewe una mapungufu gani mpaka awe na uhusiano na huyo jamaa sasa? :D
 
Ni kweli inaonekana kuwa maelezo yangu yanamkandamiz sana huyu binti, ilo siwezi kulipinga hata kidogo. Lakini nasema yale ambayo ni ya kweli kwa upande wangu pasipo kumkandamiza. Ila kuhusu kumuondoa kwa bwanake wa zamani sio kweli. Mimi wakati namtongoza aliniambia alikuwa hana mtu.
wewe ni mwanaume na unajua au ushawahi kushuhudia namna mbavyo wadada wanavyosaliti mahusiano yao kwa kutamani makuu. Ulihakikisha vipi kama ameachana na huyo switi wake? na pia alikueleza ni lini waliachana and ukafanya comparizoni ya muda kabla ya kumrecruit inn? Na kingine kiwango cha elimu ya bwanake wa kale uliulizia??? maana siku hizi wanawake wengi wakishamzidi mwanaume kielimu basi kibuti kinatembea wanasaka wa kufanana nao kielimu kitu ambacho ni wrong.

Ila sijasema kwamba unamkandamiza sana ila nilitaka tu jamii ifahamu mambo machache ili tukitoa maoni tujue tunachangia nini tusije tukawa tunadandia mkuki kwa mbele (ulio kwenye mwendo),

Inawezekana amegundua kuwa humpi yale mambo ambayo alikuwa anayapata kwa kisiki chake cha kale hivyo anaamua kukumbushia sega la zamani.
 
Isije ikawa umepata mtu mwingine kwa hiyo unataka kuanza kumzingua dada wa watu,mambo ya chuoni bado tu unayo moyoni we kweli unatisha,ukitaka kufanikiwa katika maisha yako acha kuweka vinyongo ndani ya moyo wako,maana naona tatizo ulilonalo ni kinyongo kinakusumbua utapata shida sana katika maisha yako.

Na pia kama utaoana na huyo dada inawezekana ukaja mtesa sana dada wa watu kwa hiyo tabia yako ya kukaa na vitu vya mwaka 47 ndani ya moyo,maana anweza kufanya kitu mdomoni ukasema nimekusamehe lakini moyoni una sononeko,angalia sana Brother.
 
Kama kuna jamabo linalosumbua akili za watu nikiwemo mimi ni kuacha mke wakati umeshakuwa na watoto. Haya maswali unayojiuliza sasa majibu yake utauapata tu baada ya kuoana mna mtoto au watoto na mkeo akatembeza nje na ukajua kama ulivyojua sasa.

Huyo atakuja kukufrastrate baadae tu . Wamekuwa vicheche kupindukia mkuu. Achana nae sasa hivi. Tafuata mke , huyo siye.
 
Kama kuna jambo linalosumbua akili za watu nikiwemo mimi ni kuacha mke wakati umeshakuwa na watoto. Haya maswali unayojiuliza sasa majibu yake utayapata tu baada ya kuoana mna mtoto au watoto na mkeo akatembeza nje na ukajua kama ulivyojua sasa.

Huyo atakuja kukufrastrate baadae tu . Wamekuwa vicheche kupindukia mkuu. Achana nae sasa hivi. Tafuta mke , huyo siye.
 
Kaka, kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga...... bora uwe peke yako na mpweke kuliko kuwa katika mahusiano na BADO uko mpweke....Kwa ushauri wangu mimi...TIMUA...kuanza upya C ujinga !
best of luck!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom