[ILIKUA NI LIFTI - VIJANA OCHESTRA(Hamza Kalala)]
Haikua jambo baya kwangu
Kwa yule kijana kumpatia lifti
Kama unavyohamu yapata wiki ya tatu
Gari langu lina matatizo ya kuzimikazimika ooo Mume wangu eee
Kutoka nyumbani Oyster Bay kufika Salender
Gari langu lilinizimikia eeee
Yule kijana alinisaidia kusukuma Mume wangu eee ooo ooooo oooooo
(CHORUS)
Kilichonishangaza sio lifti Mama Watoto
Ni tabasamu na vicheko mlivyokuanavyo ndani ya gari
Nilichanganyikiwa midomo ilianza kunicheza
Mithili ya mtu aliyemeza kipande cha moto Mama watoto
je huyu bibi leo angejiteteaje?????