X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,700
- 14,767
Wengi tunajua kuwa masomo ya sekondari vijana wengi huanza kupevuka akili hapo kuna jamaa mmoja anaitwa STUNTER kipindi anasoma kidato cha kwanza shule moja hivi st. kayumba alimpenda binti mmoja mrembo sana anaitwa Evelyn Salt . Tatizo la STUNTER alikuwa hajawahi kuzungumza na wasichana yani hakuwahi kufunguka mazungumzo ya kihisia kwa wasichana. Hivyo ilimuwia vigumu sana kumueleza hisia zake Evelyn Salt . STUNTER alivumilia hadi walipofika kidato cha tatu Ndipo STUNTER akamfungukia mrembo Evelyn Salt lakini bahati haikuwa nzuri kwa STUNTER kwani Evelyn Salt alimkataa, STUNTER alihuzunika sana alichanganyikiwa akajiona ana mkosi mkubwa sana. STUNTER Alikuwa na marafiki zake watatu ambao ni Kurutamjanja , Majestic wolf na Gobe.
STUNTER Aliwaeleza marafiki zake hao juu ya Evelyn Salt kumkataa Gobe akamwambia STUNTER achana na mapenzi kuna dawa nitakupa itakusababisha usiwaze kabisa mapenzi Kurutamjanja akaongezea tena hiyo dawa itakufanya ufauru vizuri darasani. STUNTER hakuwa na hili wala lile muda wa mapumziko akafatana na akina Majestic wolf ambao walikuwa ndio desturi yao kila muda wa mapumziko ukifika huwa wanaenda nje kidogo ya shule ambako kulikuwa na jumba bovu. Walipofika huko Gobe akatoa kiberiti na sigara kubwa wanaitaga msuba a.k.a ganja. Majestic wolf akawasha akapiga pafu mbili tatu akampa Gobe kisha Kurutamjanja, Majestic wolf akamwambia STUNTER vuta kidogo hiyo itakusaidia kupunguza mawazo. Bila ubishi STUNTER akavuta moshi wa ganja ghafla akapaliwa wenzake wakamcheka ila walimsisitiza aendelee kuvuta STUNTER alivuta ile ganja hadi macho yakawa mekundu.
STUNTER Alikithiri uvutaji ganja akajikuta anashindwa kusoma kabisa hivyo maendeleo yake darasani yalishuka sana. Sky Eclat na Nifah ambao walikuwa walimu wa STUNTER walipoona STUNTER anashuka sana kimaendeleo waliamua kumwita na kumweleza kuwa mwendo anao enda nao utamfanya asifaulu mtihani wake wa mwisho. mwalimu Sky Eclat na Nifah walimshauri STUNTER mambo mengi sana Nifah akamwambia " STUNTER mwanafunzi wangu shukuru wewe umepata wazazi wanaokusomesha kuna vijana wenzako hawana wazazi na wengine wanao ila hawana uwezo wa kusomeshwa ila wewe unapata bahati unaichezea shauri yako" mwalim Sky Eclat akadakia "sijui unamatatizo gani wewe STUNTER tunakutegemea sana na tulizani utaitangaza vyema shule yetu ila siku hizi umebadilika sana sasa tunakuomba ubadilike au una mpango kuja kuwa kibaka? maneno ya walimu yalimchoma sana STUNTER
STUNTER Aliwaza mengi sana alijilaumu sana kujiingiza kwenye uvutaji wa ganja kwa sababu ya kutoswa kwenye mapenzi. Aliamua kuacha kuvuta na akaamua kujitahidi kwenye masomo kwani aliamini kuwa akifauru kila kitu kitakuwa rahisi kwake. Alijitahidi kusoma japo moyoni alikuwa anaumia sana kumuona Evelyn Salt akiwa na mvulana mwingine anaeitwa chakii . Roho ilimuuma sana STUNTER lakini alijitahidi sana kusoma kwa bidii walifanya mitihani ya mwisho. atimae majibu yalitoka STUNTER alifaulu vizuri sana alifanikiwa kuendelea na masomo ya juu. Mambo yalimnyookea sana STUNTER. Hatimae alimaliza chuo kikuu huku akiwa na mkataba wa ajira na kampuni moja ya mawasiriano.
STUNTER Alifanya kazi kwenye hiyo kampuni kwa bidii na uaminifu. pale offisini STUNTER alikutana na mrembo Beauty Eva . STUNTER Alimpenda sana huyu mrembo wakaanzisha mahusiano hatimae wakaoana. Harusi yao ilifana watu walikunywa na kula hadi wakasaza. walihudhuria watu wengi wakiwemo Juma chief , Karakwende hujambo BAK great queen na wengine wengi.... STUNTER na Beauty Eva walifanikiwa kupata watoto mapacha nameless girl na mshana jr watoto hawa walipendwa na kila mtu mtaani. lakini punde Evelyn Salt alianza kumtafuta STUNTER akimweleza kuwa anampenda sana STUNTER alimweka wazi Evelyn Salt kuwa ameshaoa. Evelyn Salt Alilia sana kulikosa penzi la STUNTER
.....Itaendelea
{story hii ni ya kubuni haihusiani na wenye majina yaliyotumika humu, mniwie radhi nyote niliotumia majina yenu bila ridhaa yenu lengu ni kuelimisha jamii sikuwa na nia ya kuwachafua}