Alinihisi nakula mkewe

Mr Natafuta

JF-Expert Member
Sep 26, 2016
1,670
760
Mwana Jamvi,

Habari yako niko na kisa flani hivi amizing ambacho ingekuwa ni mimi sijui ningefanyaje, kuna mpangaji hapa tuko wote kwanza aliwahi nihisi mimi nakula mke wake, nikamwambia bwana mdogo mimi utansamee ila sijawahi hata waza kula mkeo.

Asee jana nimechelewa kuja home, huu mji tunaishi wapangaji wawili tu get moja ila kila mmoja na uwa lake

Mimi sijaoa so siwahi home kivile, jana mishale ya saa sita nikarudi home ile sijapark fresh jamaa / mpangaji mwenzangu kanikimbilia broo naomba unisaidie tumuwahishe wife hospital ni mgonjwa sikumuuliza chochote tukamchukuwa mkewe mpaka hospital.

Mkewe pressure ilikuwa juu mno, wakati sisi tuko nje na jamaa naanza kumpa moyo chalii kama analia flani, namuuliza kulikoni ananiambia alimkuta mkewe CHUMBAN UCHI na kijana ambae muda wote yeye aliaminishwa ni kaka mtu yaani kaka wa mkewe.

Nilishtuka na kuweweseka kwa sekunde kadhaa mvinyo wote akilini ukaruka ila sikumuonesha, ananiambia hakuwasemesha ila mkewe amebaki kulia tu alijua jamaa kasafiri ghafla jamaa akarudi bila taarifa.

Huyu kijana ako na kama 29 yrs huu moyo wa kuhimili kiasi hiki sijui kautowa wapi, binafsi nazan ingekuwa kesi ya ajabu sana kwangu.

Wewe mdau wasemaje? Kwa fumanizi la namna hii?
 
Sasa si angemuacha ili presha ishuke yani unafumania halafu unampeleka hosp,kweli jamaa anamoyo wa chuma
 
Ashajua uzaifu wa mumewe!,Hana pressure Hana lolote,jamaa kakaliwa kichwani na mkewe Hana kauli...
 
Dunia INA mengi jaribu kumshauri jamaa asijefanya kitu cha hovyo kikamkosti
 
Yaani kawafuma live bila chenga, aisee! Kaka wa kuchonga! ,wanawake nimewavulia kofia
 
Back
Top Bottom