Alinidhulumu, nimemuharibia. Je, nimekosea wakuu?

Alinidhulumu, nimemuharibia. Je, nimekosea wakuu?

"samehe 7 mara 70" ni rahisi sana kuandika na kuutamka mdomoni ila ni vigumu kuutekeleza. binadamu tumeumbwa na kitu kinachoitwa kisasi. siku yakikukuta utaelewa namaanisha nini mkuu
Acha kudanganya watu wenye akili zao eti umemharibia.Sasa kama umemharibia kwa nini usiseme ulichokifanya kama sio kuendekeza ushirikina?Kwa maelezo yako tu ulienda kwa washirikina wenzio unless utuambie ulimharibia vipi.
 
HV kijana mkimya mbona hujibu hili swali kwamba ulitumia njia. gani?????????????, wewe ni mlozi tu.na umekosea kutojibu hili swali na umekosea kwenda kwa mganga kumtia nuksi kiumbe mwenzio.
 
Hapa sangoma anahusika 100% tunakuuliza ulitumia njia gani kumharibia mpaka watu wamehama kwake wanamuona kama kinyesi hutaki kutoa jibu unarukaruka tu
 
Amebaki tu na mkewe.
Haaa haa haaaaa.
Hapo ndo umemuharibia zaidi
 
Kuna rafiki yangu alimuharibia kijana mmmoja kwa bosi wake ambaye ni mzungu anaishi London, kidogo afukuzwe kazi, hadi akamuomba msahaha yaishe.

Ilikuwa hivi; Huyo rafiki yangu alikuwa na rafiki yake kutoka nchi ya jirani, huyo rafiki aliomba ashukie nyumbani kwake (malazi, chakula, pamoja na hela taslimu laki tano.
kwa kumuahidi kwamba angemrudishia hela zake pamoja na gharama zote za chakula na malazi ikiwa pamoja na kumlipa deni lake pindi bosi wake atakomlipa.

Cha kushangaza jamaa aliondoka bila hata kuaga, rafiki yangu kumtafuta anasema nimehamia hotelini, alipomuuliza kuhusu hela zake akamruka kabisa. Uzuri rafiki yangu alikuwa na contact za yule bosi wake ambaye anaishi London. Akamwandikia email kumueleza hali halisi na kumuelezea jinsi ambavyo jamaa hataki kumpa hela zake.
Baada ya muda yule bosi wake akamuandikia jamaa arudishe pesa za watu pamoja na kumlipa gharama zake zote kwenu huko ni kuharibu image ya kampuni. Jamaa kwa kuogopa kupoteza kazi ilibidi amuombe rafiki yangu msamaha na kumlipa hela zake zote.
 
1467133505932.jpg
 
Umefanya vizuri sana hasa hapo uliposuka mpango mchepuko/hawara wake akamkimbia!
 
kama mjamaa wako sahiv afya mgogoro nawaswasi na izo figisufigisu zako..
na sasa kwa mfamo mjamaa akafa kwa stress si umeua hapo
 
Umenikumbusha Jamaa yangu alikuwa "mkuu wa idara ya Computer" ktk Taasisi flani....

Ikatokea zabuni ya kusambaza IT equipment.... Jamaa akaniambia nimpatie 8M ili aweze kulazimisha niipate hiyo tender...

Aliniambia kuwa hizo hela ni Manager anataka... Ameshaweka mambo sawa.

Kupenda mteremko nikampatia hiyo hela kwa kumuwekea ktk account... Mwisho wa siku nikaikosa tender.... Kila nikimuuliza ananiambia tender bado... Kumbe zoezi limekwisha..

Nikaamua kumfuata boss wake nikiwa na Bank Statement inayoonyesha malipo niliyomfanyia......

Boss alikubali kunilipa hela yangu na jamaa akanitimuliwa kazi....

Ubaya unalipwa kwa Ubaya.
 
Kijana mwezangu tulikuwa tuna mpango wa kufungua biashara pamoja ila mwisho wa siku akajifanya mjanja akachukua mtonyo wote akafungua biashara kwa jina lake akanikana. Nilijiona fala maana nilikuwa sina uthibitisho wowote kama tulichangia baishara, nilimuamini kupita maelezo coz tulitoka mbali.

Kwakweli aliniacha vibaya, kiaina nikashukuru Mungu, nikasema siendi kwa mganga wala vyombo vya sheria, nitatumia akili yangu ya kuzaliwa kumkomesha. Nimemfanyia figisufigisu kwenye biashara zake sasa wateja wote wamemkimbia. Biashara 1 amefunga hii nyingine mda si mrefu ataifunga vilevile maana anauza kimoja kimoja.

Jamaa asomeki kwa sasa afya mgogoro amekuwa mtu wa mawazo mawazo hawara amemkimbia amebaki na mkewe tu kwenye shida zake. Wakuu nimefanya vibaya kumharibia mtu kama huyu kumbuka aliniacha vibaya, nimefanya vibaya kumharibia?

Yaani umeniudhi ungeniambia umemtoa roho kwa kamati ya ufundi ningekupongeza lakini kwa hapo atategua na atajipanga tena na kisha atakuanzishia dozi mpka akutoe uhai kama huamini subiri
 
Nakumbuka miaka mingi nyuma... Nilikuwa na rafiki yangu... Ndo nlikuwa naanza maisha nakaa kwa bro... Sehem ya kwa bro ndogo... Rafiki yangu yy alikuwa na chumba analipla 15000 kwa mwez, chumba kikubwa na hakuwa na vitu vingi kwake. Alikuwa na kagodoro kagodoro kadogo kama ulimi.
Mungu alini bariki na vicent. Nkanunua godoro la kuanzia maisha kwa hela yangu laki na themanin.. Sina pa kuliweka nkasema mwana we unalala kwenye ka godoro kadogo hili weka kwako tumia ila ntunzie.. Kipindi hicho homethieta ndo zinaingia nkaenda nkanunua nkasema rafiki yangu ntunzie.. Sababu yy alikuwa tu nyumban nkapata kama mtaji wa laki nane.. Kipindi hicho sim xa mkonon ndo zinaingia.. Yy na vijana kama 3 nkawa nanunua simu kariakoo kwa sh 23000 wanasafirisha kupeleka tanga na yeye anauza kwa sh 35000 mpk 40000.. Ivyo biashara ikiisha tunatoa hela ya mzigo na faida tunagawana.
Awamu ya kwanza ilienda vzr na faida nzur na hela yake nkampa..
Awamu ya pili nkaenda nae kariako akayajua machimbo.
Alivyoondoka ndo sikupata hata sumni. Nilidhurumiwa vyote vitu vya ndan na mtaj na faida...
 
Kwa hiyo ukamsamehe saba mara sabini?
 
Back
Top Bottom