Alinidhulumu, nimemuharibia. Je, nimekosea wakuu?

kijana mkimya

JF-Expert Member
Sep 10, 2015
277
121
Kijana mwezangu tulikuwa tuna mpango wa kufungua biashara pamoja ila mwisho wa siku akajifanya mjanja akachukua mtonyo wote akafungua biashara kwa jina lake akanikana. Nilijiona fala maana nilikuwa sina uthibitisho wowote kama tulichangia baishara, nilimuamini kupita maelezo coz tulitoka mbali.

Kwakweli aliniacha vibaya, kiaina nikashukuru Mungu, nikasema siendi kwa mganga wala vyombo vya sheria, nitatumia akili yangu ya kuzaliwa kumkomesha. Nimemfanyia figisufigisu kwenye biashara zake sasa wateja wote wamemkimbia. Biashara 1 amefunga hii nyingine mda si mrefu ataifunga vilevile maana anauza kimoja kimoja.

Jamaa asomeki kwa sasa afya mgogoro amekuwa mtu wa mawazo mawazo hawara amemkimbia amebaki na mkewe tu kwenye shida zake. Wakuu nimefanya vibaya kumharibia mtu kama huyu kumbuka aliniacha vibaya, nimefanya vibaya kumharibia?
 
Hujafanya vibaya aisee.

Ulichofanya ni kuhamisha stress kutoka kwako na kuzipesti kwake.

Kama mtu kakudhulumu na hukumfanyia neno baya kwa nini usimfanyizie bana.

Ila usijaribu kwenda kwa waganga maana ukishajiingiza engo hizo utakutana na wababe walio kwenye gemu kitambo, watakuumiza sana.
 
kweli kabisa mkuu kiaina nimefarijika moyo wangu. sikuwahi na sitothubutu kwenda kwa mganga!
 
Samehe 7×70.malipo ni hapa hapa duniani..
"samehe 7 mara 70" ni rahisi sana kuandika na kuutamka mdomoni ila ni vigumu kuutekeleza. binadamu tumeumbwa na kitu kinachoitwa kisasi. siku yakikukuta utaelewa namaanisha nini mkuu
 
Kwa hiyo kwa kumuharibia yeye, wewe umefaidika vipi Kimaisha? au ndio "bora tukose wote?"

Kumbuka sio kwamba namtetea huyo mzulumaji
 
Kwa hiyo kwa kumuharibia yeye, wewe umefaidika vipi Kimaisha? au ndio "bora tukose wote?"

Kumbuka sio kwamba namtetea huyo mzulumaji
nimepata nguvu ya ajabu ya kusonga mbele, we ulitaka nimuangalie akijagamba na kunufaika baada ya kunitapeli na kuniweka juani?? hakuna kitu kama hiko dunia ya sasa. ukija.mba wenzio wanaharisha!!
 
Back
Top Bottom