WAKUU KILE KISA CHA MSHANGAZI AMBACHO NILIWAAHIDI NDIO HIKI HAPA.
Hiki kisa kinanikumbusha kipindi Mama yangu mzazi alipo gundua kuwa nimeanza kuingia kwenye ulimwengu wa mapenzi (kushenyenta) aliwahi kunikalisha chini na kuniambia, katika kufanya ujinga wangu wote niogope sana watu wa aina mbili wanafunzi (mabinti) na wake za watu.
Japo Mama hakuwa akiongea na mimi mambo yanayohusu jinsia lakini hii siku alinichana kibabe tena macho makavu kabisa.
Hapa kwa mabinti wa shule nahisi nimefanikiwa kwa asilimia zisizopungua 98, shughuli ni hapa kwa wake za watu.
Kwa mabinti nimesema nimefanikiwa kwa asilimia hizo kwasababu kadhaa
● sijawahi kuwa na mahusiano nae hata mmoja.
● sijawahi kufanya hata jaribio moja la kumnyemelea hata mmoja.
● sijawahi kuingia kwenye majaribu yoyote kiasi cha kuona naweza kushindwa kujizuia na kushawishika kutafuna gozi.
● Kwa sasa nikiwaona akili yangu inaniambia ni wadogo zangu tu siwahesabu kabisa kwamba ni kundi la wanawake.
Hizo asilimia chache nimeziacha kwa kuto kuukana ukweli kwamba mimi ni mwanaadamu naweza kuteleza sekunde moja tu nikalitenda hata ambalo sikuwahi kulitarajia.
Hapa kwa wake za watu nimesema ni shughuli kuwakwepa kwa sababu,
● anaweza kukuficha kwamba yupo kwenye ndoa na usijue.
● (ni watu wazima) anaweza kukuhitaji akakutia kwenye mitego ambayo ni ngumu kunasuka hasa Kama mnaishi karibu au mnakuwa pamoja muda mwingi kwa kuunganishwa na kazi au kwa namna nyingine.
Kiufupi ni kwamba sijawahi kungonoka na mke wa mtu na ninakwepa kila niwezavyo ila hiki kikombe ni kigumu sio kitoto yaani ni kigumu mno. kuna siku kidogo nimle muuza vipodozi bila kutarajia (hawa wakupiga hodi majumbani) akili ilivyonijia nilijilaani sana kwa kitendo kile maana ilibaki kama dakika tu tuingie kwenye mtanange. (Hii siwezi kusimulia kwa mapana hata nihakikishiwe ulinzi na jeshi la U.S.A na Russia kwa pamoja🤣🤣🤣)
Kinachonifanya nisijihusishe na wake za watu ni wosia wa bimkubwa kwa asilimia kadhaa, lakini sio kwa asilimia zote maana wosia wa bimkubwa ulilenga zaidi usalama wangu kuliko kuwaza maumivu atayopitia mwenye mke wake atakapo tom.ewa.
huwa najiambia 'hivi huyu mumewe akijua atajisikiaje' yaani hata kama anaonekana ni mnyonge na dhalili kiasi gani na akili yangu inaniambia hana cha kunifanya (wapo hawa ambao anaweza kuchapiwa tena na mtu anaemfahamu roho ikamuuma na asifanye chochote) ila huwa navaa viatu vyake, nawaza vile wanaume tunavyopambana kuwatunza wanawake, nawaza vile wanaume tunavyowekeza muda, moyo akili na kila kitu kwa hawa viumbe wenzetu.
Mwisho nasema kama huyu jamaa atapata maumivu kupitia upumbavu wa mkewe basi sababu ikawe ni wanaume wengine na sio mimi.
Kifupi ni kwamba kabla sijawaza usalama wangu huwa nawaza maumivu atakayopitia Shujaa mwenzangu nitakae mgongea.
NIMEWACHOSHA EEE!
Hiko kilikuwa kisa tu kama muvi za kihindi twende kwenye stori yenyewe sasa.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
MWANZO..
Hii ni mwaka jana mwishoni kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa.
Kama ilivyo utamaduni wangu wa kuficha majina ya wahusika na sehemu halisi ambayo tukio limefanyika, kwamfano stori ni ya Mbagala rangi tatu naweza kuipeleka buza kwa mpalange.
Kwenye simulizi hii nitachukua kisa na mpangilio wa matukio tu vitu vingi nitaweka bandia hadi kazi maana hii ni ya karibu tu hapa.
Japo kuweka vitu vingi bandia inaondoa ladha na hamu yangu ya kuandika lakini nitafanya hivyo kwa sababu dunia ni kiganja, kwa mfano kuna siku nilikuwa napita kwenye uzi wa kula tunda kimasihara nikakuta jamaa alivosimulia alivyomla beki tatu ambae alitoka huku mtwara, nikafatilia kwa makini sana sifa za huyo binti kiumbo nikaishia kutukana kimoyomoyo tu (.... la mama.. huyu mngese 🤣🤣🤣) ukiniuliza hapo chini kuhusu hii nitakujibu.
________________________
Simu yangu ilikuwa inasema saa 3:24 nikatuma meseji kwa muuza chai ambae ndiyo Mshangazi wetu tumwite TATU au MAMA ZAWADI.
'leo niwekee chapati nne supu niwekee ya buku mbili'
Nikaweka simu mfukoni na kuendea kupiga dawa buti kubwa la ngozi linalojulikana kwa jina la Travolta, muda huo kiredio changu pembeni kiki nibless magoma ya Dizasta vina.
Japo kuna makelele sana nje ya kiwanda hiki cha Dangote cement kilichopo mkoani Mtwara lakini huwezi kuniweka mbali na redio muda wa kazi.
Baada ya dakika chache nikaitoa simu yangu na kukuta meseji ya Mama Zawadi.
'Poa David inaonekana leo umeamka na njaa'
MIMI 'Saana'
Nikaendelea kufua na kusafisha kiatu kimoja Baada ya kingine katika goli langu la kushona na kusafisha viatu ambapo pia nauza bidhaa kama vile wallet mikanda kofia soksi singland na bidhaa nyingine zinazotumika na wanaume.
Kimsingi kipato changu kipindi hiki kilikuwa kinacheza kati ya 15 elfu hadi 30.
Ilipofika saa 4 nikafunga goli na kwenda kupiga chai kama ilivyo kawaida yangu.
Nilipofika mgahawani ARAFA (mshirika wa mama Zawadi) akaniletea chai na vyote nilivyoagiza.
Nikaanza kubonda msosi huku tukipiga stori mimi Arafa na Mama zawadi ambae yupo jikoni ninamsikia tu sauti.
Ni utaratibu wangu kula mgahawani kwao muda wa asubuhi tangu nimeanza kufanya kazi katika kijiji hiki cha Hiyari.
Pia wao huwepo mgahawani asubuhi tu kuanzia saa sita huwa wanawapisha wamama wengine ambao hukaa hadi jioni.
Tuna mawasiliano ya kawaida na Mama zawadi ambae nimemtambulisha kama Mshangazi japo sijajua kama ni sahihi kwa mimi kumwita mshangazi maana kwa umri ananizi miaka 7 yaani kama mimi ni 23 yeye 30, kama mimi ni 33 yeye 40.
Kusema kweli nimekuwa nikivutiwa na umbo la mama huyu japo kulingana na hadhi/heshima niliyompa akili ilikuwa inanikataza kabisa kumtongoza japo ni miaka isiyopungua minne sasa tangu tumefahamiana.
Umbo lake ni mnene mwili umejitenga, ni mweupe kidogo ana shepu flani hivi kama mwimbaji Keisha (uvumilivu umenishinda baby alaavyu.. bebi alaav.. bebi alaavyu..) ila Mama Gift ni mrefu kidogo, lakini zile hipsi kishundundu na miguu ya kushiba ni vile vile, sema Mama Gift ana tumbo kubwa kidogo.
Sababu nyingine ni kwamba sina uzoefu wa kungonoka na wanawake walionitangulia umri kufikia miaka mitano na kuendelea, pia Sababu nyingine ni Mama Gift kuwa na mipaka katika maongezi, yaani kuna wale wamama mkiwa na mazoea kidogo tu anaweza kuongea maneno hadi wewe mwanaume/kijana ukaona aibu kama unajiheshimu na ukiwa kijana wa hovyo ukaona anawasha taa ya kijani, haikuwa hivyo kwa mwana Mama huyu mwenye watoto watatu.
MIMI "Kwani zawadi leo mbona simuoni nimtume juisi hapo nje"
MAMA G "anaumwa nimemwacha kwa bibi yake"
MIMI "Ahaa anaumwa nini"
MAMA G "malaria yaani hapo alipo hana raha mnyonge hatari mwanangu hapa kuna watu wawili tu walioagiza ndiyo tunawasubiri hapa tuondoke"
ARAFA "Naenda kukununulia, juisi gani nichukue?"
Arafa ni kama 20 na 5, 6, 7 hivi.
MIMI "Chukua parachichi ya mia tano. Mama G nitapita kwenu jioni kumcheki rafiki yangu"
Ki Gift chenyewe kina miaka mitatu tu.
MAMA G "Sawa itakuwa vizuri na yeye ajione mtu Mamaangu"
MIMI "Hahahaha kwani sasa anajiona paka?"
"Hapana lakini si unajuwa mtoto akiishi na mzazi mmoja kuna muda huhitaji faraja ya Baba lakini anakosa, ila utakapofika anko wake mwenyewe ukajifanya kumjali jali hata kwa dakika tano tu kuna kitu atajisikia cha tofauti"
Nikaendelea kugonga chai yangu nikashushia na juisi ya parachichi kisha nikaingia mzigoni kuendelea kukimbiza.
Harakati za watu zilizopo hapq zinafanya eneo hili kuwa ni miongoni mwa maeneo mazuri mno kibiashara katika mkoa huu.
Nikaendelea kupiga kazi hadi ilipofika jioni ya saa 10 nikapanga vyema vitu vyangu ili kujiandaa kufunga ofisi.
Hadi inafika saa 10 na nusu nikatuma meseji kwa wateja wangu kadhaa ambao bado wapo ndani ya jengo la kiwanda lakini nina viatu vyao, nilipojiridhisha hakuna mteja nina deni nae nikafunga ofisi yangu na kuanza safari kuelekea nyumbani kwetu kijiji jirani kutoka hapa Hiyari kinaitwa Likonde.
Ni mwendo wa baiskeli ya kubadilisha gia hapo katika barabara ya Lami inayoelekea kwenye kijiji chetu.
Kumbu kumbu ya kupita nyumbani kwa Mama Zawadi ikanijia, Mama zawadi anaishi katika kijiji hiki hiki cha Hiyari lakini ni mbali kiasi kutokea hapa Dangote.
Nikaachana na barabara ya Lami na kuingia katika njia nyembamba ambayo inaingia ndani ndani huko ambako ndiko anaishi Mama Gift.
Nikafika nyumbani kwa Mama Gift na kubisha hodi, ni nyumba ya udongo ambayo imeezekwa na makuti, ina vyumba viwili jiko na sebule.
Mama G akaitikia na kunikaribisha hadi uwani ambako alikuwa akifua.
Akani tengea kiti nikakaa kisha yeye aka kaa katika ndoo kubwa, tulikuwa tunatazamana lakini ni Umbali kidogo.
Nikamuuliza kuhusu binti yake Gift akaniambia amelala. tukaanza kugonga stori za maisha siasa kidogo na mambo mengine mengi.
Muda huo Mama G alikuwa akifua na kisha kuanika nguo kwenye kamba hali iliyonifanya niinjoy kivutio hiki cha bure kabisa, gharama ni kumtazama mgonjwa tu.
tuliongea sana na Mama G hadi kimawazo nikaanza kujipa umwamba na kusahau kabisa vikwazo vinavyonizuia kuweka mkeka wangu kwa Mama G ambavyo ni heshima na tofauti yetu ya umri.
Yule shetani wa 'Mwambie Mwambie' akashika nafasi moyoni mwangu baada ya kumpiga teke moja takatifu Malaika wa 'usimwambie utavunja heshima yako baada ya kukupiga nyundo'
Akili ikakubaliana na shetani kwa kusema 'aaa kwanza akinikataa si basi, kuna nini cha ajabu'
Mwisho nikafungua mdomo na kumwambia Mama Gift kwamba ninampenda na ninahitaji kuwa nae katika mahusiano.
Mama G aliipokea habari hii kama jambo la kustusha mno na kusema ni jambo ambalo haliwezekani kwa namna yoyote ile.
Nilipo muuliza kwanini haiwezekani alikomaa sana na sababu ya kuzoeana kwetu akisisitiza suala la sisi kuonana miili yetu ni jambo ambalo haliwezekani hata kidogo.
Nilishindwa kung'amua kwamba hiki anacho kisema Mama G ni halisi au ndiyo majaribu kama ilivyo kawaida ya hawa Mama zetu. muhuni nikaumbisha mmama huu hadi mwisho ukaingia kwenye reli. Ukweli wangu ndio kitu kikubwa alicho kisisitiza wakati anausaini mkataba wa kuwa mimi.
Nilimuahidi nitakuwa mkweli kwake kwani ni maamuzi yangu kuwa nae katika mapenzi hivyo sitakuwa na mambo mengi katika penzi letu.
Tukaendelea kupiga stori za mikakati ya mahusiano yetu namna tutakavoyadumisha.
Mama G alikuwa anapanga mipango kama sio yeye aliye nikataa dakika kadhaa tu hapo nyuma😂
Mambo yakanoga bhana penzi shata shata, penzi jipya.. penzi la moto bila kifaa maalum huwezi kuligusa.
Muda huo akili yangu yote ilikuwa inawaza ngono tu dhidi ya Mama G ambae baada kuwa wapenzi tumekubaliana nitamwita TATU jina lake la kuzaliwa, kama yeye anavyoniita David jina langu, (mimi ni nani hadi nisimwite Tatu bebi wangu! Kuwa wewe kuweza?😂)
Muda huu sasa jua lilikuwa nikielekea kuzama, tulitoka uwani na kuingia ndani huku akili moja inanishawishi niombe shoo akili nyingine inaniambia nitaonekana nina papara.
Nikaona bora nivunge tu ili kulinda brand.
Baasi bwana... mwanangu mpya (Gift) akaamka kutoka usingizini Mamaake akaenda kumchukua na kumleta sebuleni ambapo tulikuwa tumeketi kwenye mkeka.
Akamwambia kwamba anko David amekuja kukuona dogo akanifahia hivyo hivyo tu na wenge lake la usingizi miksa homa.
Mamaake akampeka msalani kisha akamrudisha ndani nikampakata na kuendelea kupiga stori na Tatu wagu.
Muda huu alikuwa ashaziwasha taa za haya makampuni ya kukopesha vifaa vya umeme wa jua.
Nilipoona muda umeenda sana Nikamuomba anisogelee ili nimuage, Akanisogelea hadi takagusana nikamshika shingo kama nataka kumnong'oneza kitu sikioni hivi, nikamchapa busu moja zito la ghafla huku nikizama moja kwa moja mdomoni mwake kutafuta kinywaji changu pendwa cha muda wote.
Alitaka kujitoa kwa kutumia nguvu ila ghafla akapoa nahisi ni baada ya kuona mwanae atastuka kinachoendelea maana bado alikuwa amelala kimya mapajani mwangu.
Nilikilia mate kama sekunde 20 hivi, nikaanza kuhisi bwana David anataka kuleta shida kwenye suruali yangu nikamuacha Tatu mara moja.
Akanitandika kofi zito la mgongo huku akicheka, mzee nikakausha tu tuli (enzi za utoto tulikuwa na msemo kofi la mpenzi haliumi moyo 😂😂😂)
Mwisho nikampa mwanae ambebe kwani ilikuwa tayari nataka kuondoka.
Akanisindikiza hadi nje tukaongea kidogo theni nikampiga kibao chepesi cha kalio na kukimbia na kibaiki changu (nyumba yao ipo jirani na majumba mengine ila kulikuwa na kiza tayari muda huo)
Baasi bwana nikafika nyumbani na siku ikapita.
Asubuhi pakakucha kama ilivyo kawaida, nikaamka na kushuka kitandani nikajinyoosha mwili na kugundua nilikuwa na afya tele, nikaanza harakati za maandalizi ya kuingia kazini.
Siku hii nilikuwa na hamu mno ya kwenda kazini ili niwahi kumwona Mama watoto mpya.
Hadi panakucha nilikuwa tayari kazini naweka vitu katika mpangilio.
Ilipofika mida yangu ya chai niliibuka mgahawani kwa Mama Gift kama ilivyo ada.
Leo Mama G alikuwa anakwepa kabisa kunitazama usoni.
Nililetewa msosi wangu na kubonda kisha nikalipa na kusepa.
Nilipofika golini nikapokea meseji ya Mama G, tukaanza kuchat na baadae tukakubaliana jioni nitakwenda kwao kama ilivyo kuwa jana.
Jioni Ilipofika mzee baba nikaweka mambo sawa na kufunga ofisi.
Leo nilikuwa naenda huku nimedi.da asee japo nilikuwa najaribu kuitoa akili katika mawazo machafu.
Nilipofika nilipiga hodi kama kawaida nikakaribishwa nikaingia ndani.
Nikamkuta mwenyewe na watoto wake wawili huyo G na dadaake wa miaka kama 9 hivi.
Baada ya kuwasalimia akamtuma huyu mkubwa aende kwa bibi yao sikumbuki alimtuma nini, tukabaki wenyewe na ki G chetu.
Leo tulikuwa ni kama wapenzi kabisa, asee wamama wanajua kunyenyekea na kuheshimu mwanaume wakiamua. Tulikaa kama dakika kadhaa sebuleni baadae akaniambia twende chumbani maana wa mama wa jirani huwa wanakuja kuongea hivyo akiwa chumbani atawapa sababu yoyote watageuza.
Ilikuwa saa 11 hiyo.
Tulikwenda chumbani kisha nikajitupa kitandani nae akaja, kiko ki G sasa kilikuwa kinasumbua sana siku hiyo utadhanikilikuwakinaelewa mchongo, Kilikuwa kimepata hafadhali kiasi basi kila tukikapea mia kikanunue pipi chenyewe badala ya kumumunya pipi kinatafuna na kuja kudai hela nyingine😄
Mama G alipokuja kitandani nikampisha upande wa ukutani ambako ningembananisha vizuri kwa shughuli yangu maalum, nyiie nyiie nyiie wanawake wanene watengewe sehemu yao maalumu huko mbele za haki, yaani paja tu la moto utadhani ni ikulu yenyewe.
Ngoja niishie hapa bhana nitaendelea.
Kisa hiki ni kifupi tu pengine hiyo sehemu ya pili ikawa ndiyo mwisho au kama itazidi ni sehemu ya tatu.