Alikotokea Jenerali Defao

Alikotokea Jenerali Defao

Bingwaman

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
548
Reaction score
288

Wengi tunamfahamu mwanamuziki Defao kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, lakini ni wachache tunaofahamu wapi alikotokea kimuziki. Defao alianza kupata umaarufu mwanzoni mwa miaka ya 1980 akiwa na bendi ya Grand Zaiko Wawa iliyokuwa ikiongozwa na mchawi wa solo Felix Manuaku Waku. Hapa Defao na kundi zima la Grand Zaiko Wawa wanaporomosha ‘live’ kibao Salima katika studio za televisheni ya taifa ya Zaire mwaka 1984. Amini, usiamini, Defao ni huyo mwimbaji wa kwanza kushoto. Shimita ni huyo wa pili kushoto aliyevaa nguo za bluu.
 
Last edited by a moderator:
Waimbaji kutoka kushoto: Defao, Shimita, Djo Nickel na Djeffard Lukombo. Mpiga solo ni Felix Manuaku Waku 'Pepe Fely' ambaye pia alikuwa ni mwanzilishi na kiongozi wa bendi. Manuaku ni mmoja wa waanzilishi wa bendi ya Zaiko Langa Langa, ambayo aliachana nayo mwaka 1979 na kuunda Grand Zaiko Wawa.
 
Hapa Defao (wa kwanza kushoto) anaonekana vizuri zaidi. Mwaka ni 1984 na kibao ni Ma Jolie.

 
Last edited by a moderator:
Huyu ndiye Defao wa sasa tunayemfahamu wengi. Dah! Watu wanabadilika jamani.

 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom