Alijua amemkomoa

Alijua amemkomoa

madala mujipa

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Posts
1,421
Reaction score
864
amani kwenu wadau
Nina jamaa yangu kama miaka miwili na nusu nyuma alikumbwa na kisanga cha mwaka baada ya mkewe kuja kumuachia mtoto mdogo wa mwaka mmoja na yeye kutokemea kusikojulikana

Baada ya hapo tulimpa moyo na ushauri ampeleke mtoto kwa bibi yake au kwa ndugu ili wamlee lakini wapi jamaa aligoma kabisa akawa asubuhi anamuandaa mtoto wake na chupa ya maziwa na uji wa ulezi tunapiga nae mishe kama kawaida baada ya muda anambadilisha pampers muda unakwenda

Hivi sasa mtoto amekua na anavutia sana chini ya uangalizi wa jeshi la mtu mmoja baba mtu eti ghafla juzi yule mwanamke ametokea kusikojulikana eti anataka kumuona mtoto na aondoke nae ,muda aliofika pale mtoto na baba yake walikua wamepata abiria wa kumpeleka safari yake tukamshauri amsubiri mzazi mwenzake

basi yule mwanamke akasema kuna sehemu anakwenda lakini hatochelewa...mara yule jamaa na mwanawe wakarudi tukamueleza ujio wa mama mtoto..nikamuona jamaa amebadilika sura ghafla na kusema si alijua amenikomoa sasa anataka nini tena..tukajaribu kumshauri amsikilize..yule mwanamke akarudi pale wakakutana lakini jamaa hakumtoa mtoto mama mtu amuone kiasi cha kutokea mzozo mkubwa tulichomshauri yule bibie ni kuwa aondoke aepushe shari lakini aligoma na jamaa nae kuona gozi gozi akamtia mtoto wake kwenye usafiri wakaondoka na hakurudi tena ,yule mwanamke kuona hakuna anaemjali akajiondokea zake.

Asubuhi jamaa anatuambia yule mwanamke ana kichaa yeye alimuachia mtoto mdogo alijua atashindwa kumlea lakini si huyo amekua

Dah dunia ina mambo yeye alijua amemkomoa lakini jamali amekua kwa kudra hata sisi wenyewe kijiweni hatuamini

jamani mkitupiwa watoto msipaniki ni kushukuru tu
 
nimemsifuuu sana yaani awe mwanamke au mwanaume anayetelekeza mtoto hastahili kujisogeza tena hapo sio kama anataka mtoto tu life la usawa huu limemkomesha wenzie wanamshangaa anataka kurudi hapo kinamna hahaa it has eaten to her yaan imekula kwake
 
mbona nyie mnaacha watoto wenu mkija kuomba msamaha tunawasamehe?
 
Wanawake wengine hawaoni hata aibu kukimbia mtoto wake aliyemzaa kwa uchungu!? Aiseee pongezi kwa huyo mwanaume maana kutunza mtoto si kitu kirahisi!!!

Ningekua ni yeye, hakyamungu huyo mwanamke angejuta kurudisha 'matendego' yake kuja kumuona mtoto!!!!
 
Jamaaa alikosea angemnasa huyo bint vibao vya
Maana dadek atavuna alichopanda

[Color= yellow]Triple A[/color]
 
Wanawake wengine hawaoni hata aibu kukimbia mtoto wake aliyemzaa kwa uchungu!? Aiseee pongezi kwa huyo mwanaume maana kutunza mtoto si kitu kirahisi!!!

Ningekua ni yeye, hakyamungu huyo mwanamke angejuta kurudisha 'matendego' yake kuja kumuona mtoto!!!!
Ktk hiyo avatar, wewe ndio yupi hapo?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Wanaume wengi ni wanafiki sana! Hapa wanaona kumnyima mama mtoto ni sawa maana kamtelekeza mtoto. Ila wao hutelekeza mimba na bado hutaka kumuona mtoto kirahisi
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa anakuja kazini na Mtoto wake, anawapa wale wafanya usafi wanamuangalizia na jioni anaondoka nae, Mtoto kakua

spend less, save more
 
Safi sana,,

Jamaa yupo vizuri sana,,,
kiasi cha kutelekezewa mtoto na kuendeleza kupiga hustle za maisha si wa kisport sport,,
salute
 
Wanawake wengine hawaoni hata aibu kukimbia mtoto wake aliyemzaa kwa uchungu!? Aiseee pongezi kwa huyo mwanaume maana kutunza mtoto si kitu kirahisi!!!

Ningekua ni yeye, hakyamungu huyo mwanamke angejuta kurudisha 'matendego' yake kuja kumuona mtoto!!!!

Hahahahaaa ila huyo jamaa ni kauzu kweli, sijui ni askari jeshi huyo, nahc alishapitiaga jwtz Tantaw madala mujipa
 
Back
Top Bottom