ALIFUMANIWA, AKAFUKUZWA, ANADAI TARAKA, MUME AGOMA.

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,318
Reaction score
7,984
Mwanaume mmoja anayefahamika kwa Nina la Stanford(34), mkazi Wa wilayani Mbarali amefikishwa mahakamani na mke wake kwa kukataa kutoa taraka. Akimweleza hakimu Wa mahakama ya mwanzo, Bi Victoria aliiambia mahakama kuwa mwezi July alifumaniwa akiwa na mwanaume mwingine guest.

Ameendelea kudai kuwa baada ya tukio hilo mumewe alimtimua nyumbani na kumtishia kumjeruhi iwapo atarudi. Mwanamke huyo amesema aliomba msamaha kupitia vikao na ndugu ili arudi kwa mumewe lakini bwana huyo alikataa, ndipo alipofika ofisi ya kijiji kuomba suruhu hata huko jamaa alikataa. Mwezi September alifika baraza la kata kuomba suruhu au apewe taraka. Mwanaume aliendelea kushikiria msimamo Wa kutokurudiana na mkewe ndipo kesi imefikishwa katika mahakama ya mwanzo.

Hakimu alimuuliza iwapo anadai taraka au amefika kuomba suruhu? Amejibu kuwa bado anampenda hivyo kwanza ni kuomba arudi na ikishindikana basi apewe taraka. Hakimu ameshauri mlalamikaji atafute mtu anayeufahamu mgogoro wao vizuri afike mahakamani ili kuangalia namna ya kuumaliza.

Ifahamike wanandoa hao wamedumu kwa muda Wa miaka 8 na wanawatoto 2. sababu ya mwanaume kutokutoa taraka ni kuwa anahisi siku au miaka ya mbeleni huenda akamuhitaji tena kwenye malezi ya watoto. Hivyo anataka akae kwa ndugu zake kwa muda ambao anahisi mwanamke atakuwa amejifunza vyakutosha.

UNGEKUWA WEWE NDIO JAMAA UNGEFANYAJE,?

NDOA TAMU JAMANI ZIHESHIMUNI.
 
Fyekelea mbali, naingiza mzigo mpya Maisha yanaendelea.
 
Mm nadhani mwanaume anahofia kugawana mali na mwanamke so anataka abaki hewani lkn pia anampenda mkewe pia
 
Huenda raha alizokua anapata kwa mkewe hawezi kuzipata kwengine, au anahisi akimuacha mwenzie ataoa na atamtambia
kwahiyo anaona bora waonje tu ila kuolewa kwa sasa asahau,ila jamaa anajipa stress sana.
 
Hapo stress anapata zaidi huyo mwanamke. SI unaona anavyohangaika kama kuku anayetaka kutaga. Btw ile kesi yako ulimaliza?
 
Back
Top Bottom