Alielielewa Tamko la Mkullo?!

Kabengwe

JF-Expert Member
Oct 20, 2009
240
47
Jana kwenye taarifa ya habari ya TBC - Habari za biashara, Mh Mkulo alisema kuanzia sasa furniture za wizara zote zitanunuliwa kutoka nchini!

Sasa sikuelewa (Au inawezekana nilisikia vibaya) kwamba watu waimport na kuiuzia serikali au watengeneze na kuiuzia serikali?!

Kama itakuwa ni kutengeneza hapa nchi kwa kutumia mali ghafi tulizonazo na kuiuzia serikali, then hiyo ni step kubwa sana katika kuongeza mzunguko wa fedha hapa nchi. Naipa serikali heko kwa hilo. Itazalisha kazi nyingi kwa hilo.

Ila kama ni tofauti na nnavyo fikiri (kuruhusu watu waimport na kisha kununua toka kwao), then sioni kama kuna la maana.
 
Maagizo ya moja ya kamati za bunge yanataka samani zote zitokane na mali ghafi za ndani, hivyo serikali isinunue samani zilizotengenezwa toka nje. Yaani wakanunue pale keko, magereze, JKt nk
 
Maagizo ya moja ya kamati za bunge yanataka samani zote zitokane na mali ghafi za ndani, hivyo serikali isinunue samani zilizotengenezwa toka nje. Yaani wakanunue pale keko, magereze, JKt nk

Lets wait and see if this will be possible.
 
Kama hii ni kweli basi ni vizuri sana. Step inayofuata ni kuelekeza nguvu kwenye viwanda vidogo vya mafuta ya alizeti ili baada ya miaka mitano angalau 90% ya mafuta yote ya kupikia yatokane na alizeti/karanga/ufuta/nk inayozalishwa na wakulima wa Kibaigwa, Buyagu, Ng'wawaza, Idukilo, Maganzo, n.k tusinunue mafuta kutoka malaysia/indonesia tunayo ardhi ya kutosha kutulisha!!!
 
Maagizo ya moja ya kamati za bunge yanataka samani zote zitokane na mali ghafi za ndani, hivyo serikali isinunue samani zilizotengenezwa toka nje. Yaani wakanunue pale keko, magereze, JKt nk

Nadhani hiki ndicho alichomaanisha. Well, ni tamko zuri of course ambalo limekuja a bit late kwani jirani zetu Kenya its more than 3 years walipiga maarufu fanicha za serikali kununuliwa toka nje. Its interesting kwa kweli kwani Kenya ni wateja wetu wazuri wa mbao kwamba waliliona hilo mapema kabla. Lakin pia of all the countries miti yote hii tuliyonayo sisi pia wa kuagiza uchafu wa china kwa jina la fanicha? Vijana wazuri katika utengenezaji wa fanicha tunao wa kutosha na of course majeshi yetu, magereza na JKT wana vitengo vizuri sana vya kutengeneza fanicha.

Angalizo hapa ni kwamba tunaomba basi hii kitu ifuatiliwe maana tumezoea kusikia maazimio kibao ambayo huwa hayatekelezwi lakini still hakuna kinachofanyika na kuwa kusihia kuwa ni porojo tu za vijiweni.
 
Haya mawazo walitakiwa waje nayo pindi walipokuwa waningia madarakani.

It's not too late though to do the right thing, kuliko wasingefanya kabisa!

Hilo wazo la Alizeti kutoka kwa Mkuu Ntemi kazwile ni la msingi sana! Serikali walifikirie
 
Kama nimemuelewa vyema ni kuwa Tanzania inajaribu kuongeza thamani za mali ghafi inayopatikana humu nchini. Hili lingekuwa kwa bidhaa zote na isiwe kwa samani pake yake. Kuna masuala ya madini, mazao mbalimbali ya kilimo nk.
 
Back
Top Bottom