Aliekuwa mbunge wa Chalinze azikwa

Aliekuwa mbunge wa Chalinze azikwa

mwarabua

New Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
3
Reaction score
0
Aliekua mbunge wa jimbo la chalinze said ramadhani bwana mdogo hatimae azikwa na maelfu, Marehemu amezikwa baada ya kusaliwa sala ya mwisho baada ya sala ya aljumaa. Mazishi hayo yamehudhuriwa na rais jakaya kikwete, makamo wa rais muhamed ghalibilali pamoja na mawazir na wabunge na akiwemo mbunge wa kambiya upinzani freeman mbowe.
 
Mbona siku hizi tunachukua siku nyingi kuzika. Utaratibu wa zamani, mtu akitutoka leo tunashirikiana kuzika leo kabla ya jua kutua. Au sio?
 
jk karudi lini?
 
Kwa taratibu za kislamu ndio wanafanya hivyo, ila kwa vingozi hata kama ni muislamu taratibu za kiserika
ri nazo hupewa nafasi kidogo

Mbona siku hizi tunachukua siku nyingi kuzika. Utaratibu wa zamani, mtu akitutoka leo tunashirikiana kuzika leo kabla ya jua kutua. Au sio?
 
Haya mmemaliza kuzika huyo nasikia kuna mwenyekiti wenu na yeye amefariki.

NB:
Magamba tubuni hasira ya Mungu inawaka juu yenu.
 
MBOWE karudi DAR kuhesabu faida ya makusanyo yatokanayo na fedha za OPD kwa kujikodishia helikopta kwa siku ya nne leo.
 
Leo, alikatisha ziala yake Uswiss kuja kuwahi mazishi alifika Nairobi asubuhi ndege ya serikali ikamfuata kumwaisha CAHALINZE kijiji cha Lugoba .

Kwa hiyo atarudi tena Davos au ndo amerudi Tz jumla?
 
Kwa hiyo atarudi tena Davos au ndo amerudi Tz jumla?

Kasho anarudi Davos kwani mkutano haujaisha na baada ya hapo ana ziara ya kiserikali Papua New Guinea!!! Akiatoka huko anaunganisha na ziara ya Australia kwa wiki mbili!!!
 
Aliekua mbunge wa jimbo la chalinze said ramadhani bwana mdogo hatimae azikwa na maelfu, Marehemu amezikwa baada ya kusaliwa sala ya mwisho baada ya sala ya aljumaa. Mazishi hayo yamehudhuriwa na rais jakaya kikwete, makamo wa rais muhamed ghalibilali pamoja na mawazir na wabunge na akiwemo mbunge wa kambiya upinzani freeman mbowe.

Nataka nijue kama Ridhiwani Kikwete alihudhuria!!!! Ni mwanapwani mwenzake at na mbunge wa kwao au nimekosea??? Mwana wa mfalme!!! Tehe Tehe!!
 
Kasho anarudi Davos kwani mkutano haujaisha na baada ya hapo ana ziara ya kiserikali Papua New Guinea!!! Akiatoka huko anaunganisha na ziara ya Australia kwa wiki mbili!!!

Rais Kikwete aalikwa Nigeria na Rais Jonathan

Rais wa Nigeria Mheshimiwa Goodluck Jonathan amemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria Mkutano wa Taasisi ya Uchumi Duniani Afrika (WEF-Africa) unaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria wa Abuja mwezi Mei mwaka huu.

Rais Jonathan ametoa mwaliko huo kwa Rais Kikwete wakati viongozi hao wawili walipokutana na kufanya mazungumzo leo, Alhamisi, Januari 23, 2014, kwenye Hoteli ya Intercontinental, Davos, Uswisi, ambako viongozi hao wanahudhuria wa Mkutano wa Mwaka huu wa Taasisi ya Uchumi Duniani –WEF.

Rais Kikwete amekubali mwaliko huo wa kuhudhuria Mkutano huo uliopangwa kufanyika Mei 7-9 mwaka huu mjini Abuja, Nigeria.

Mkutano huo kati ya viongozi hao wawili umehudhuriwa na Mawaziri wa Nigeria wa Mambo ya Nje na Fedha na Uchumi.

Nigeria inakuwa nchi ya nne katika Afrika kuandaa mkutano huo. Kwa miaka mingi, mkutano huo wa WEF-Africa ulikuwa unafanyika Cape Town, Afrika Kusini mpaka Tanzania ilipofanikiwa kuwa nchi ya kwanza ya Afrika nje ya Afrika Kusini kuandaa Mkutano huo mwaka 2010.

Tokea wakati huo, Ethiopia imeandaa mkutano huo na sasa Nigeria.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM.

23 January, 2014
 
Back
Top Bottom