Alichotamka Augustino Mrema Kuhusu Oscar Kambona....

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246

Ndugu Zangu,

Historia ni mwalimu mzuri. Bado kuna umuhimu wa kukumbushana historia yetu. Kukumbushana tulikotoka ili tuelewe tulipo na tupate walau mwanga wa tunakokwenda.

Huko nyuma nimeuliza; kama kuna wanaokumbuka alichotamka Bw. Augustino Mrema. Ni mrema huyu aliyepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika kipindi cha Urais wa Mzee wetu, Ali Hassan Mwinyi.


Katikati ya vuguvugu lile la mageuzi ya kisiasa miaka ya 90 mwanzoni, Watanzania zikatufikia habari; kuwa Oscar Kambona, aliyekosana na Nyerere na aliyekimbila uhamishoni Uingereza, alikuwa njiani kurudi nyumbani. Ujio wa Oscar Kambona ukawa gumzo la mjini na nje ya jiji. Kuna waliojiandaa kwenda uwanjani kumpokea.


Usiku mmoja ikasikika sauti ya Bw. Mrema redioni. Sauti ya Waziri wa Mambo ya ndani. Mrema alitamka, kuwa kama Kambona angekanyaga mguu wake Dar es Salaam, basi, angekamatwa kujibu mashtaka ya uhaini.


Ni hofu ile ile ya Serikali hata wakati huo. Hofu ya kuimarika kwa fikra za upinzani na kukua kwa upinzani. Mrema akatumika au akajituma kuwatisha Watanzania. Kambona alikanyaga Dar, hakuwa na mashtaka ya kujibu. Ulikuwa ’ mkwara’ tu, kama wanavyosema mitaani.


Na Mrema, akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, aliifanya kweli kazi ya kuwa ’ Mbwa wa Serikali’. Alibwaka kweli kweli. Nakumbuka usiku mmoja mwanzoni mwa miaka ya tisini nilimsikia Mrema akitoa ’ mkwara’ redioni kutishia maandamano ya CUF. Maandamano yale yalikuwa yahitimishwe kwa mkutano viwanja vya Mnazi Mmoja. Mwenyekiti wa CUF, Bw. James Mapalala ndiye alikuwa aongoze maandamano hayo na kuhutubia.


Augustino Lyatonga Mrema akaaunguruma redioni usiku ule. Alirusha ’ mkwara’ mzito. Kuwa maandamano hayo si halali na yangekutana na nguvu za dola. Kesho yake, CUF waliingia mitaani. Ndio, Ungangari wa CUF ulianza siku nyingi.


Pale Mnazi mmoja FFU wakamwagwa, na farasi wao pia. Virungu vilitembea. James Mapalala, Mwenyekiti wa CUF, hakuonekana. Kukawa na taarifa, kuwa anatafutwa na polisi.



Dar ilikuwa ndogo wakati huo, lakini James Mapalala hakupatikana siku hiyo.
Ninazo taarifa za kuaminika za Kibalozi, kuwa James Mapalala alikuwa amejificha kwenye moja ya makazi ya rafiki yake, balozi wa nchi moja ya Kimagharibi. Ni balozi gani huyo? Na nini hasa kilitokea miaka 20 iliyopita?


James Mapalala yungali hai. Huu ni wakati kwa waandishi vijana kuwatafuta wazee veterani wa harakati za mageuzi ya kisiasa hapa nchini. Wazee kama akina James Mapalala.


Hawa ni watu muhimu sana watakaotusaidia kupokea simulizi zao. Kisha ziwekwe kwenye maandishi, na iwe kumbukumbu za kihistoria. Ni historia yetu, tusiionee aibu. Ni urithi tutakaowaachia wajukuu zetu ili nao waweze kujifunza. Waweze kujitambua na kujenga mioyo ya uzalendo.

Huu wangu ni mchango mdogo tu.

Maggid

http://mjengwa.blogspot.com
 
Nashukuru sana maggid mi huwa kila siku natafuta historia ya kweli ya nchi lkn siioni nadhani cku nyingine utupe kidogo historia ya tanzania
 
Kweli Historia itakosoa mambo yote na kama hawatajisahihisha wataumbuka, ule mchezo wa naibu waziri mkuu wakati huo kuwatisha watu walipe ndani ya siku 7 ulianzia Dodoma, ilianza kwa mhindi (M-Asia) alitakiwa apeleke faini yake mapema na walikutana nyumbani kwa Bw Shariff Jamal (marehemu ) ambapo shukrani za Waasia hao kumaliziwa kesi yao walitoa pesa na kujenga kituo kidogo cha POLISI cha kwanza kabisa nchini, na kuanzia hapo Mzee wa kikofia alikuwa akiripoti hapo jirani kkupokea mgawo wake. Ukisikia mtu kapewa siku 7, basi anaambiwa atangulie Dodoma kwa Sharif.
Kilichofuatia ni Tanga Mjini hatimaye Tz nzima vituo vidogo vya POLISI sina uhakika kama vinaendelea kufanya kazi
 
Na wapo wanaoamini kuwa Shushushu Augustino Lyatonga Mrema wakati huo Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani, kamanda Mkuu wa FFU dhidi ya wanamageuzi, mla rushwa mkubwa na ruga ruga nambari wani wa CCM, ndiye alikuwa kinara wa mageuzi !
 
Back
Top Bottom