#COVID19 Alichosema Hayati Magufuli kuhusu UVIKO-19 yametimia, sasa tutaishi nao katika jamii

Ugonjwa gani ambao hatukuwahi kuishi nao katika jamii?
 

Labda kama unataka kulazimisha kuyasahau aliyoyasema mwendazake:

1. Corona haipo Tanzania.
2. Corona ni vita vya kiuchumi dhidi ya Tanzania.
3. Chanjo za Corona ni biashara za upigaji kutoka kwa mabeberu kutaka pesa zetu kwa nguvu.
4. Chanjo ni sumu za kuwauwa watanzania.
5. Barakoa, sanitizers, PPEs zote ni biashara za mabeberu nk.

Corona tutaishi nayo labda kama una maana kama anavyoishi nayo sasa hivi pale Chatto.
 
Acha kumsingizia hayati na pia kuabudu binadamu mwenzio mpaka maiti yake, wa kuabudiwa hivyo ni Allah na mitume wake. Kinachokusumbua ni uvuvi wa kusoma na kujuelimisha, kama ungekuwa unaitumia simu yako na TV yako kuitafuta elimu, kama hukuipata shuleni & chuoni, ungeshajua zamani sana kwamba magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi huwa ni janga lisiloisha mara moja, especially kama hicho kirusi ni kigeni kwa wanayansi. Tabia moja kuu ya kirusi inayowatesa magwiji wa virology & vaccination ni ile hali ya kubadilika badilika. Mfano sasa hivi hawa covid 19 kwenye hili wimbi la tatu imekuja variant inaitwa Delta.... Narudia acha kabisa kuabudu binadamu mwenzako mwenye ubongo kama wa kwako, itafute elimu hata ikibidi kwenda Uchina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…