Ali Msham na Julius Nyerere

Hapo hapo usisahau waarabu ndio wafanya biashara wa kwanza wa utumwa.hebu pekua pekua vizuri bongo yako.kwa suala LA Dini sisi waafrica tumekurupuka.hakuna dini hata moja ambayo tulilitewa ikatusaidia.dini zote zilikuja kutupumbaza na mwisho kufanywa watumwa.
Waarabu walikua wanyama sana,wametesa sana babu na bibi zet,wakaja wazungu na wakayaendeleza yaleyale.
 
Mama Maria hakuwa na duka kwa Ali Mshamu au popote
Hapa ndipo historia inanipaga tabu ,sijui nimwamini nani au nisimwamini nani ,Japo historia sijaisoma kama somo ila kwanini mara nyingi hupotoshwa ??
 
Kama historia haikubadilishwa awamu ya nne kalagabaho...tugange yajayo
 
Kama historia haikubadilishwa awamu ya nne kalagabaho...tugange yajayo
Wanamajlis,
Hakika historia ya uhuru hii niliyoandika inawaumiza watu wengi.

Mimi sikutegemea wakati nakiandika kitabu hiki kabisa kama
itakuwa hivi.

Kwa kiasi fulani nataabika kidogo kwani sipendi kuona mtu anaumia
nafsi yake kwa ukweli ambao yeye hakuwa anaujua.

Katika ''review'' ya kitabu changu katika Cambridge Journal of African
History John Iliffe alighadhibika sana akanishambulia kama vile yeye
si profesa wa history.

Dr. Mayanja Kiwanuka katika kujibu makala yangu iliyochapwa na
African Events (London) mwaka wa 1988 kuhusu TANU yeye alinitukana
kabisa akaniita ''mbilikimo.''

Baadhi ya watu hawataki kulisikia jina la Kiyate Mshume katika historia
ya Mwalimu Nyerere.

Mwangalie Mzee Mshume na Nyerere walivyokuwa:



Wanafikia hadi kumkejeli Mzee Mshume humu JF.
Vipi utaukataa mchango wa mzee huyu katika TANU?

Mifano ninayo mingi sana.

Hiki kiduka cha mafuta ya taa naona nacho kimechoma nyoyo zetu
lakini ni katika vitu vidogo sana katika picha kubwa ya yale ambayo
wazee wetu walifanya katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ukweli hii ndiyo historia ya nyakati zile.

Huna lazima ya kuamini historia hii ya Mohamed Said.

Una haki na uhuru wa kuamini historia ya Chuo Kikuu Cha Kivukoni
iliyoandika historia ya TANU mwaka wa 1981 na hawa waasisi ambao
mimi nimewataja wakawa wote hawamo kabisa.

Hii pia ni historia ya TANU labda huenda waandishi hawakuwa watu
wa Dar es Salaam kwa hiyo imewawia tabu kujua nini kilipitika wakati
ule wa miaka ya 1950.
 
mwl. Said imenishangaza sana hii ya historia ya Sykes kutokuwepo pamoja na mikutano yote ya siri kufanyika nyumbani kwake. Labda tuseme tu na waliamua kufanya siri kutokumuandika kama ilivyokuwa asili ya mikutano yenyewe. haishangazi kuona bado kuna watu wamekomalia kubeza elimu unayotupa humu. binafsi naona ipo haja kwa watanzania kujisahihisha kuliko kupinga tu kila kitu.
 
umeshindwa kuelewa mada. hapa kinachoongelewa ni historia iliyoachwa kuandikwa iwe ni kwa kusahau, kwa makusudi au kwa wahusika kutokuwa na taarifa zake. hayo uliyoandika yote yameandikwa na yapo documented. elewa mada kwanza kabla ya kuchangia.
 
Ali Msham yuko wapi yeye kwa sasa?
 
umeshindwa kuelewa mada. hapa kinachoongelewa ni historia iliyoachwa kuandikwa iwe ni kwa kusahau, kwa makusudi au kwa wahusika kutokuwa na taarifa zake. hayo uliyoandika yote yameandikwa na yapo documented. elewa mada kwanza kabla ya kuchangia.
Ndugu yangu historia ni historia, iwe imeandikwa au haikuandikwa. Cha muhimu ni namna gani tunaitendea haki hiyo historia. huyo Mohamed Said ni mtu asiyetendewa haki, anatumia nguvu zake kuwapatia watu habari za miaka ya nyuma lakini mrejesho haswa wa vijana wa kizazi cha smartphone hauwi mzuri. Rais wa awamu ya tano kaongelea utalii kwa mapana yake, ikiwa historia iliyoandikwa inashindwa kutupatia watalii wengi vipi kuhusu ile ambayo haijaandikwa?. Ikiwa historia iliyo documented haitunzwi vipi kuhusu ile ambayo haipo documented. Nimeshawahi kuwashauri watunzi wa filamu kuhusiana na suala la wao kukaa chini na mzee Mohamed Said ili watengeneze series za filamu juu ya historia yetu ili iweze kuifikia jamii ya sasa na ijayo kwa faida ya utunzaji wa kumbukumbu za Tanzania. Mada nimeilewa, nilichoandika ni sehemu tu ya mawazo yaliyoibuka wakati mjadala ukiendelea.
 
Abunuwas,
Wakati wa kuandika historia ya TANU hilo swali kuwa mikutano ilikuwa siri
halikuwapo.

Mwalimu Nyerere alikuwa kakalia kiti na sisi wenyewe ndiyo tunajitawala.
Kitabu cha historia ya TANU cha Kivukoni College kimechapwa 1981.

Hebu ingia hapo chini In Sha Allah unisikilize:
Mohamed Said: NYARAKA ZA SYKES KATIKA KUIFAHAMU HISTORIA YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA 1

Zipo video clip 11 nazungumzia historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Zinatokana na mhadhara nilifanya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwaka 2010.
 
 
hap ni harufu ya udini tu inanikia na inachochewa nathing else
 
hap ni harufu ya udini tu inanikia na inachochewa nathing else
Troojan,
Unajitisha pasi na sababu.

Kama hofu yako ni kusoma majina ya Waislam katika historia ya TANU
na historia ya kupigani uhuru wa Tanganyika, hili bado halijawa udini.

Hakuna anaechochea kuni zozote hapa Majlis.
Tunaelimishana kuhusu historia ya nchi yetu.

Ikiwa umeliona jambo linakwenda kinyume na hayo basi ifahamishe barza.
 
Ilunga H. Ka
Ndg. Ilunga H. Kapungu
Kwa bahati mbaya sana utafiti wako wa kutaka kujua 'ukweli' wa historia umebubikwa na kutanguliza prejudice na prejudgement na hivyo kukosa uhalisia.
Najiuliza, Hizi photograph zenye matukio makubwa katka history ya nchi yetu ziko mikononi mwa watu binafsi? Kama ni hivyo, basi taasisi zetu za makumbusho ya kale zina walakini.
 
M-Kara,
''Prejudices,'' ''Prejudgements,'' ''and what have you,'' vyote hivi ni katika dhana pana ya ''Values.''
Hakuna njia ambayo mtafiti yoyote anaweza kuviepuka kwani ndivyo vinavyofanya mtafiti aamue
atafiti nini na kwa nini iwe somo hili lisiwe lile.

Msomaji haangaishwi na hivyo yeye atakwenda moja kwa moja kutaka kujua ukweli upo kwa kiasi
gani.

Hilo kuwa historia ya TANU iko mikononi mwa watu zikijumlishwa picha na nyaraka John Illife aliliona
mwaka wa 1968 wakati ule akisomesha Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Mimi nimeshuhudia tatizo hili wakati Ally Sykes aliponifungulia safe yake iliyokuwa imejaa nyaraka
na majalada ya TAA na TANU mwanzoni mwa miaka ya 1980.
 
Sheikh Mohammed,huoni kuwa mafile kufungiwa makabatini ndiyo kumechangia taarifa kukosekana kwa umma?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…