Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,452
- 34,004
- Thread starter
-
- #21
Allen,Mzee Mohamed Said nakubaliana kama Ofisi ilikuwa haina meza bora kama hiyo na Ally Mshamu (Bila shaka ni mmatumbi) akaitoa Meza hiyo bila shaka ulikuwa ni mchango mkubwa sana, lakini kwa Mwalimu mwenyewe kwenda kuipokea badala ya kumtuma mtu mwingine inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa anathamini mchango wa kila mmoja. Lakini kwa wakati huo pia kama Mama maria alikuwa na duka hapo kwa Mshamu na lazima aende kulala kwake Magomeni Majumba sita si ajabu kwa mtoto wa Mshamu kumsindikiza bi mkubwa huyo.
Hv unawajua ma selfish ama unapiga Kelele !!Dah, mbona hawa watu hawasemwi kwenye historia kabisa, somewhere nyerere alikuwa selfish sana
Ulitaka uwasome ktk historia ya darasani!?Dah, mbona hawa watu hawasemwi kwenye historia kabisa, somewhere nyerere alikuwa selfish sana
Troojan,
Linawekwa jina la yeyote yule aliyehusika katika historia ya uhuru wa nchi yetu iwe awavyo.
Ali Msham hakutoa meza peke yake.
Ali Msham aliunga mkono harakati za uhuru kwa kufungua tawi la kwanza la TANU nyumbani
kwake Magomeni Mapipa.
Akiuza kadi na fedha akipeleka mwenyewe kwa Iddi Faizi Mafongo aliyekuwa Mweka Hazina
wa TANU New Street.
Hapana ubaya kuihifadhi historia hii.
Maofisa wa polisi waliosaidia TANU walikuwapo mmoja wapo alikuwa Hamza Aziz wakati ule
ofisa wa ngazi ya chini katika Jeshi la Polisi la Waingereza.
Hamza ni mdogo wake Dossa Aziz.
Huyu TANU walimtumia sana kupata mikakati ya Waingereza kuihujumu TANU.
Alikuwapo Amri Kweyamba na Kitwana katika Special Branch.
Huyu Amri Kweyamba aliwashughulisha sana wana TANU.
Mara kadhaa alivamia nyumba ya Ally Sykes Mtaa wa Kipata kutafuta makaratasi ya ''uchochezi,''
ambayo Ally akiyasambaza kuanzia Dar es Salaam, Morogoro nemda hadi mwisho wa reli Kigoma
na Mwanza.y of
Mimi nimeandika historia hii katika kitabu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes,'' (1998) na
haijavuruga chochote katika historia ya Tanganyika bali imeleta changamoto kubwa kwa wanahistoria
si wa Tanzania tu bali ulimwengu mzima.
Leo kitabu hiki kinasomeshwa kote wanakosomesha, African History na kipo Library of Congress,
Washington.
Kituko,Mzee Mo Saidi, wewe huyo Mshamu ulikuwa ukimfahamu?, mbona kwenye kitabu chako hakuna hata sehemu moja unapozingumzia hilo tawi la Magomeni-Jaribu str? Wewe kisa cha TANU kukabidhiwa meza wala haukuwa na taarifa nacho kwa sababu Mshamu hakuwa Mmanyema, ila Kiyate kumpa Nyerere kitoweo imekuwa story kwa sababu ni Mmanyema mwenzio
Wewe unapolalamika kuwa Wazee wako wa Kimanyema wameshahaulika basi na Historia yako pia imewaacha wengi ambao sio Wamanyea
Allydou,Hii ndio tofauti ya kizazi cha sasa na cha zamani
Ingawa mm si Wazamani kivile, but nashukuru mungu kwa kunipa akili iliyotulia
Ukiona mtu /watu wanachukulia kirahisi michango muhimu ya wenzao, tambua kwamba Kuna walakini mkubwa kwenye fikira zao, and yet, wanajiita wasomi
Haikuwa jambo rahisi, na bado si jambo rahisi kufanya jambo alilofanya ally msham , ingekuwa Leo, lazima angekuwa ni mtu anaetaka madaraka, udiwani, ubunge and the like.
Nadhani ni sahihi sana ulichofanya mohamed said kwa kuandika historia halisi ya uhuru wetu kwa kuwataja na kuwatambua kwa namna moja ama nyingine wale wote waliohusika katika kupatikana uhuru wa nchi yetu, na sio one man army , na ni vema kitabu chako kifundishwe hapa tanzania.
Ikumbukwe, nyerere alikuta harakati za uhuru tayari zinaendelea, tena zikiwa na kazi ya kutosha tu, hata hiyo tanu aliikuta, hata waraka alio peleka umoja wa mataifa pia aliukuta, alifanya kupokewa tu na kuendeleza harakati ambazo kimsingi zilikuwa zipo mwishoni kabisa, amehusika kwenye harakati hizo for less than ten years.
Tatizo la afrika ni kwamba, our history is taught more by the whites, and not by ourselves.
Hapa naona tatizo kubwa sana kila mtu kutaka aonekane kimchango wake.muanze kuawakumbuka na waliopigana vita majimaji basi na walionyongwa na wakoloni.watu walijitolea adi roho zao sembuse mtu katoa meza tu mnataka awekwe kwenye kumbukumbu y uhuru.jaman tuache kulalamika.we ukimkumbaka mtu kwa maudhui yake muweke kwenye kitabu au chapisho lako tutamjua¡¡¡hapa watu wanataka kuleta suala flani la udini na ukabila.mbna vitabu vipo vingi na vinaelezea watu tofauti tofauti.labda cjaelewa linakaziwa wap ili suala.Hii ndio tofauti ya kizazi cha sasa na cha zamani
Ingawa mm si Wazamani kivile, but nashukuru mungu kwa kunipa akili iliyotulia
Ukiona mtu /watu wanachukulia kirahisi michango muhimu ya wenzao, tambua kwamba Kuna walakini mkubwa kwenye fikira zao, and yet, wanajiita wasomi
Haikuwa jambo rahisi, na bado si jambo rahisi kufanya jambo alilofanya ally msham , ingekuwa Leo, lazima angekuwa ni mtu anaetaka madaraka, udiwani, ubunge and the like.
Nadhani ni sahihi sana ulichofanya mohamed said kwa kuandika historia halisi ya uhuru wetu kwa kuwataja na kuwatambua kwa namna moja ama nyingine wale wote waliohusika katika kupatikana uhuru wa nchi yetu, na sio one man army , na ni vema kitabu chako kifundishwe hapa tanzania.
Ikumbukwe, nyerere alikuta harakati za uhuru tayari zinaendelea, tena zikiwa na kazi ya kutosha tu, hata hiyo tanu aliikuta, hata waraka alio peleka umoja wa mataifa pia aliukuta, alifanya kupokewa tu na kuendeleza harakati ambazo kimsingi zilikuwa zipo mwishoni kabisa, amehusika kwenye harakati hizo for less than ten years.
Tatizo la afrika ni kwamba, our history is taught more by the whites, and not by ourselves.
kwa hiyo wewe unataka na diallo atajwe kwa kuwa tu alimsaidia magufuli kuingia ikulu?!Harakati za kudai uhuru huwezi kufananisha na swala la ada,maana hata huyo nyerere kungekuwa na mtu kamlipia ada watu hawawezi kulalamika kwa kutomzungumzia huyo mfadhili wake wa ada,hapa swala ni harakati za kudai uhuru kuna watu hawatajwi kabisa kila jambo nyerere kitu ambacho sio kweli,nyerere hasingeweza kufanya chochote bila msaada wa hao watu.huo ndio ukweli hata kama hupendi kusikia habari za namna hiyo.
Yaaan ni shidaa aiseee.kwa hiyo wewe unataka na diallo atajwe kwa kuwa tu alimsaidia magufuli kuingia ikulu?!
mkuu, kwa hiyo tumedanganywa!Mama Maria hakuwa na duka kwa Ali Mshamu au popote
Sexer,mkuu, kwa hiyo tumedanganywa!
sawa mjuajiHujui kitu,subiri ugali ukiiva huitwe ukale
inaweza kuwa huyu Andrew Nyerere alikuwa hajazaliwa, mkuu Andrew tambua mama alikuwa na duka kwa mzee msham sawaSexer,
Mimi sina sababu ya kusema uongo.
Historia ya TANU ni maarufu kwa wazee wengi wa Dar es Salaam ya 1950 ambao wakati ule
walikuwa vijana wengine katika Bantu Group 1955 kabla haijawa TANU Youth League 1958.
Mama Maria alikuwa pia na duka la mafuta ya taa Mtaa wa Mchikikichi jirani na nyumba ya
Mwalimu Fatina.
Kama ninavyopenda kusema siku zote si lazima uamini historia hii.
Kuwa wewe umesoma haya niliyoandika na ukakutana na haya ya akina Ali Msham ambayo
kabla ya leo hukuwa umeyasoma popote au kuyafahamu kwangu mimi inatosha sana.