Ali kiba kasema hashindani na mtu

ALIKIBA - SITAKI MTU ANIINGILIE KATIKA MIPANGO YANGU, MIMI SISHINDANI NA MTU . . Mwanamuziki mahiri nchini Tanzania, Alikiba amefunguka na kusema kuwa yeye katika muziki wake hakuna mtu anayeshindana naye na kudai ila kama kuna watu wanataka kushindana na yeye basi atawaacha na kuendelea na mambo yake. . . Alikiba anasema katika maisha yake ya muziki hataki kuona mtu yoyote anamtoa katika njia yake, ndiyo maana watu ambao wanakuwa wakiongea ongea sana juu yake yeye na muziki wake hawapi nafasi, kwani anaamini akiwapa nafasi wanaweza kumtoa kwenye mambo ambayo yeye amekusudia kuyafanya hasa zaidi katika muziki wake. "Unajua kila binadamu ana tabia yake, kuna wengine wanajua kabisa kwamba wanakosea lakini wanafanya hivyo kwa sababu na wapo wengine wanakuwa wanaongea pasipokujua kama wanakosea, hivyo mimi kama msanii sitakiwi kusikiliza hivyo vitu sababu nakuwa na mipango na malengo yangu, hivyo sitaki mtu yoyote aniingilie kwenye mipango yangu kwa hiyo ukiwafuata unaweza kujiangusha" alisema. Mbali na hilo Alikiba amesema yeye haangalii ushindani na wala hashindani na mtu . . . "Mimi siangalii ushindani na wala sishindani na mtu ila kama wapo wanashindana na mimi nitawaacha washindane na mimi lakini mimi sishindani ila naangalia malengo yangu na mipango yangu katika muziki" aliongeza Alikiba. . . TOA MAONI YAKO HAPA
Huyo afanye muziki mashindano nani kamuuliza...hiyo tuzo ya huyo dogo imemfanya avimbiwe mpka akili
 
kwani nani aliwahi sema ana shindana na AK ?
halaf ni mwaka sasa hajatoa wimbo, huwez shindana na msanii aso toa nyimbo kabsa.
Ahahaaaaa anatafuta kiki. Maana alovyojidai kufuta vumbi kiti chake hakua anashindana na watu kweli. Leo anageuza kibao
 
Kiba kipaji anacho tatizo menejiment aliyonayo haina ubavu wa kumpelekesha bali yeye ndio anawapelekesha. Kama angetambua thaman yake na kuitendea kazi angekua mbali sana

mi huwa ana niacha hoi hapo tu, akijitahid huwa mwaka mzima anatoa wimbo mmoja. ila mashabiki wake huwa wana mbeba sanaa asipotee.
ni msanii mzur kiaina though
 
Alikiba yupo sahihi, na wanamfuata fuata wengi wanataka wanufaike kupitia yeye na sasa yeye hataki. Bongo kuna ujanja ujanja sana na ukiendekeza hupati chochote mfano halisi angalia saida karoli alivyotumika alafu akatemwa kama big G. Msanii anakuwa na lundo na watu wanaomnyonya huyu akidai meneja huyu msimamiz mkuu. Lazma uwe na meneja ambaye hategemei kunufaika sana kwako bali mnufaishane wote. Big kwa kuona mbali.
 
Nimejifunza kuheshimu msimamo wa mtu, hasa kwa masuala yake binafsi. Keep it up Ali Kiba...
 
Back
Top Bottom