Inasadikiwa kuwa mwandishi mkongwe nchini, Alfred Ngotezi ambaye alifariki usiku wa Jumamosi iliyopita katika hoteli moja maeneo ya Mianzini Arusha, alipewa sumu.
Hivi sasa maofisa wa NSSF ambako Ngotezi alikuwa akifanya kazi kama meneja uhusiano wanahangaka kufanya postmoterm au autopsy kubaini chanzo cha mauti yake ya ghafla.
"Alikuwa mzima kama chuma cha pua, alisafiri mwenyewe kutoka dar hadi arusha kwa ajili ya mkutano wa kimataifa wa hifadhi za jamii (ISSA) na kabla hajaanguka na kupoteza uhai alikuwa anapata chakula cha jioni na wafanyakazi wenzake kisha akainuka kwenda kucheza muziki na alipokuwa narudi kuketi akapiga chini!" alisema mmoja wa wafanyakazi wa NSSF.
Wengi wanasema ni sumu lakini kama mhusika ni moja ya wale waliokuwepo si ajabu ukweli ukafichwa ili kusevu jina la NSSF