Mathayo Fungo
JF-Expert Member
- Nov 13, 2018
- 319
- 510
Mh. Zitto, tuwekane sawa kidogo; Suala la CAG na Spika lisiwe la ‘kisiasa’.
Nimesoma barua yako kwa Katibu Mkuu wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola. Pia niliona umesema wewe na wabunge wenzako mmeamua kwenda Mahakamani ili kupata tafsiri kuhusu kinga ya CAG.
Nadhani umeamua kulitumia suala hili ‘kisiasa’ badala ya kusaidia kuliweka sawa kila mmoja alielewe. Hili usilifanye mtaji wa kisiasa.
Wengi tulitaharuki kumsikia Spika akitoa amri kwamba CAG aende akajieleze mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Taharuki ilikuwa kubwa kwa sababu Spika alienda mbali kidogo na kusema ingawaje Bunge halina polisi lakini linaweza kutumia pingu endapo mtu atakaidi amri ya kuitwa.
Kwa upande wangu nadhani hakukuwa na sababu ya ‘tone’ aliyotumia Spika kwenye Press ile kwa kuangalia nafasi ya CAG kama ofisi. Na hapo ndio mwisho wa ‘kosa’ la Spika. Haya mengine unayakuza kwa sababu zako za kisiasa.
Maswali ya kujiuliza hapa ni 1. Je CAG ana kinga ya kutokuhojiwa kwa kauli inayosemekana imedhalilisha Bunge kwa mujibu wa Katiba’?. 2. Je Spika amekosea kupeleka suala hilo kwenye Kamati?
Hili sio suala gumu sana kama utaamua kuliangalia bila ushabiki. Majibu ya maswali yote ni HAPANA. CAG hana kinga na Spika hajakosea kulipeleka suala hilo kwenye Kamati kwa uchunguzi.
Zitto wewe kama Mbunge unajua fika hakuna mtu yeyote ambaye anaruhusiwa kulidharau Bunge au mwenendo wa Bunge au Kamati. Kosa hilo dhidi ya Bunge kwa kiingereza ni ‘contempt’.
Mtu yeyote isipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano anaweza kuitwa na Bunge endapo atatenda kosa hilo. Hakuna mwingine mwenye kinga au ruhusa ya kutenda kosa hilo.
Kwa upande wa CAG Katiba haimlindi dhidi ya makosa au mashtaka yeyote isipokuwa tu kutokuingiliwa kwenye utekelezaji wa majukumu yake ya kisheria.
Maswali kwamba 1. Je kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu ni utekelezaji wa majukumu yake? na 2. Je kauli hiyo imelidhalilisha Bunge? Yatajibiwa na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge baada ya uchunguzi na kumsikiliza CAG na Spika.
Majibu hayo hayawezi kupatikana bila CAG kwenda mbele ya Kamati. Na kwenda huko haimaanishi Katiba imevunjwa.
Nimalizie kwa kusema kwamba Mahakama au chombo kingine chochote ndani au nje ya nchi haiwezi kuzuia Kamati kutekeleza majukumu yake ya kisheria.
Kauli ya CAG kwamba Bunge ni dhaifu haipo kwenye ripoti yake yoyote. Hakuna ‘uchunguzi’ wowote alioufanya akitekeleza wajibu wake na kugundua kwamba Bunge ni dhaifu. Hajawahi kutoa taarifa rasmi kuhusu udhaifu wa Bunge. Angefanya hivyo angekuwa ametekeleza wajibu wake na asingeingiliwa.
Hakuna sababu yoyote ile kupindisha suala hili kwa sababu tu Spika alitumia kauli ya pingu au alitoa taarifa kabla ya wito wa Kamati. Masuala haya mawili hayaondoi ukweli kwamba CAG hana kinga dhidi ya kauli yake aliyoitoa alipohojiwa.
Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iachwe ifanye uchunguzi na kuamua kama 1. Kauli hiyo ni udhalilishaji wa Bunge 2. Kauli hiyo ilitolewa wakati CAG anatekeleza majukumu yake.
Alberto Msando.
10.01. 2019