Albert Msando afunguka kuhusu Zitto Kabwe

Albert Msando afunguka kuhusu Zitto Kabwe

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,723
Reaction score
5,662
Mwanasheria ambaye pia ni diwani kupitia CHADEMA, Ndugu Albert Msando amehoji yafuatayo;

1. Amehoji je, kama
CHADEMA kinasema ni Cha Kidemokrasia kwanini kinaaamuru Afukuzwe tu kwa kuwa ameenda mahakamani?

2. Amehoji je, ni nani mwenye mandate ya kumvua mwanachama uanachama wake.

3. Je, uamuzi wa kumvua uanachama ulipaswa kutangulia kwa umma au kwa Zitto kwanza?

4. Amehoji je, imekuwaje mtu anayesimamia sakata la Escrow afukuzwe kwa sasa?

5. Amesema pia kuwa Zitto hana haja ya kubaki
CHADEMA kwa kuwa hata akiomba kubaki haitakuwa na mashiko. Pia ameuliza itakuwaje akae meza moja na Tundu Lissu,Wakati Tundu Lissu anatangaza amesema walishamfukuza toka mwaka jana. Naye anaona kuwa Zitto hahitajiki CHADEMA.

6. Pia amesema lengo la kumfukuza Zitto limefanywa kinafiki tu.

7. Amesema kuwa haoni haja ya kulazimisha kila mtu awaze kama Tundu Lissu au Mbowe au Slaa.

9. Pia amesema kuwa mgogoro huu ni funzo kwa Zitto, Wanachadema na Watanzania kujua aina ya viongozi walionao.Pia amesema kuwa migogoro hii isitumike kujenga chuki.

Chanzo: Clouds TV
 
Mwanasheria feki huyu. Mh tundu ametoa kwenye katiba ya CHADEMA hakutunga yeye yakwambaaa mwana CHADEMA yeyote atakae shitaki mahakaman moja kwa moja atakua amejivua uanachama so huyu mwanasheria Alienda shule kafanya nn? Da!
 
Swali la mdingi, nani mwenye mandate ya kumfukuza ZITTO?
 
Hakuna mwanasheria mzembe kama huyo Msando, anyway Zitto atakuwa m/kiti na yeye mwanasheria mkuu wa ACT ila wanasafari ndefu sana kuwaconvince watanzania wakubaliane na unafiki wao. Na ajue kwamba hakuna mtu aliyemfukuza Chadema but KATIBA DID, it has power over everyone.
 
Mwanasheria feki huyu. Mh tundu ametoa kwenye katiba ya CHADEMA hakutunga yeye yakwambaaa mwana CHADEMA yeyote atakae shitaki mahakaman moja kwa moja atakua amejivua uanachama so huyu mwanasheria Alienda shule kafanya nn? Da!

Alikwenda shule ili apige madili. Kichwani hakuna kilichoingia kama anauliza maswali ya kimaamuma namna hiyo.
 
"Huyu naye afukuzwe haraka msaliti tu",Wenye chama.

DEMOGHASIA IMESHIKA KASI.
 
Huyo msando Alberto asijitie umajinuni hiyo ndo katiba iliyomweka mabogini kama alijua sio ya kidemokrasia angeenda TLP mshamba sana huyo kama vipi aende nae ACT hatutaki virusi chadema
 
Last edited by a moderator:
Huyu ndiyo mnamuita wakili msomi?

Kuna kipengele ndani ya katiba ya CHADEMA inasema"mtu yyt atakaye kishtaki chama mahakamani atapoteza sifa ya kuwa mwana CHADEMA"
 
Kama kweli ZZK anahusika na ACT ni wazi kuna tatizo, huwezi kuanzisha taasisi ndani ya taasisi nyingine tena kwa siri.
Wanaolifahamu hili na kulielewa wanajua kuwa huwezi kukaa na mwanachama wa namna hii. Ndio maana Mh. Kafulila alivyotofautiana na chama chake 'hakufungua ofisi' FB/Twitter bali aliomba msamaha na akasemehewa na sasa anajenga taifa.
Alafu kama huyu wakili kayaongelea haya kwenye hiyo radio ni wazi lao ni moja!
 
Mwanasheria feki huyu. Mh tundu ametoa kwenye katiba ya CHADEMA hakutunga yeye yakwambaaa mwana CHADEMA yeyote atakae shitaki mahakaman moja kwa moja atakua amejivua uanachama so huyu mwanasheria Alienda shule kafanya nn? Da!

Nn maana ya demokrasia?kma swala haljapatikana muafaka ndan ya chama hachukue hatua gan?katiba ya chama ni ya kidikteta nafkria inapnga wanachama kwenda mahakaman il iwakandamize kwa maslai ya wachache.shame chadema
 
Naona taratibu fahamu zinaanza kuwarudia. Hayo hawakuyaona hapo kabla?
 
Huyu analipwa retainer fee na zitto, sitegemei aongee tofauti na hivi.
 
Back
Top Bottom