Albert Einstein amepoteza tiketi kwenye treni

Siku moja, Albert Einstein alikuwa ndani ya treni akitoka Chuo Kikuu cha Princeton. Kondakta akaanza kupita kukagua tiketi za abiria mmoja mmoja. Alipomfikia Einstein, mzee akaanza kupekua mifuko ya koti lake tiketi haipo.

Akaingia mifuko ya suruali, akatafuta ndani ya koti lake dogo la safari, wapi! Hakuna kitu. Mwishowe akaanza kuitafuta hata kwenye kiti alichokuwa amekalia.

Kondakta alipoona vile, akamwambia kwa heshima
“Dr. Einstein, mimi nakujua vizuri. Kila mtu hapa anakujua, na nina uhakika kabisa ulinunua tiketi. Usiwe na wasiwasi, achana nayo.”

Einstein akaitikia kwa kichwa na kumshukuru. Kondakta akaendelea na kazi yake ya kukagua tiketi za abiria wengine. Lakini alipokuwa karibu kutoka nje ya lile behewa, alipiga jicho nyuma na kumuona Einstein amepiga magoti chini, bado anatafuta ile tiketi uvunguni mwa kiti.

Kondakta akashangaa, akarudi tena na kumwambia:

“Kama nilivyokwambia, kila mtu anakujua wewe ni nani. Hakuna shida kabisa. Huhitaji kuhangaika kuitafuta hiyo tiketi.”
Einstein akainua kichwa chake, akatabasamu na kumjibu,

“Asante sana rafiki yangu. Mimi pia najua mimi ni nani. Lakini shida ni kwamba, sijui naenda wapi! Ndio maana naitafuta hii tiketi kwa udi na uvumba nijue safari yangu inaishia wapi.”

Story hii inatufundisha kuwa Hata uwe na akili gani ya kutatua magumu ya ulimwengu, bado unaweza kukwama kwenye vitu vidogo kama kujua kituo unachoshukia!
Haya mambo ya Einstein yananikuta sana siku hizi. Mfano leo mchana nilotoka nyumbani kwenda salon, nikiwa nimepanga nikitoka ninunue sundries, mkaa wa home kisha chakula cha kuku na drinker moja ya kuongeza bandani kisha nipitie kwa wanunua mali used niwaoneshe picha ya madirisha niliyoyabadilisha hivi karibuni, tukikubaliana bei waje wayachukue.

WAkati nimerudi nimepark home nayaona tena yale madirisha backyard ndio nakumbuka sijapitia kwa wale jamaa. Siku hizi nasahau sana vitu kwa style hii.
 
Dah inasikitisha sana, nimelia mno kusikia alikuwa hajui anakoenda 😭

Natamani Seran angekuwepo Miaka hiyo ili amchukue akampe hifadhi kwake mana Nasikia anapenda vibabu vyenye iq kubwa 😎
IQ kubwa napeleka wapi? hujui kutofautisha pesa na Iq kabisa :Agakakskagesh:
 
Baba yangu Mdinyakobe Kimario, ambaye ni mwanasaikolojia alinifundisha kitu kinachoitwa 'Halo Effect', yaani hali ya mtu/watu kuamini kuwa mtu akiwa expert kwenye kitu kimoja basi anakuwa expert kwenye vitu vingine vyote.

Kwa mfano, mimi ni expert kwenye masuala ya nyeto lakini Wana-JF wengi wanaamini kuwa Mimi pia ni expert wa vitu vyote, ndiyo maana wakati mwingine wananipa heshima nisiyostahili 😂.

Sasa hii story ya Albert Einstein imenikumbusha hili.

ShesRise_1,
Seran.
We are cooked:Agakakskagesh:
 
Haya mambo ya Einstein yananikuta sana siku hizi. Mfano leo mchana nilotoka nyumbani kwenda salon, nikiwa nimepanga nikitoka ninunue sundries, mkaa wa home kisha chakula cha kuku na drinker moja ya kuongeza bandani kisha nipitie kwa wanunua mali used niwaoneshe picha ya madirisha niliyoyabadilisha hivi karibuni, tukikubaliana bei waje wayachukue.

WAkati nimerudi nimepark home nayaona tena yale madirisha backyard ndio nakumbuka sijapitia kwa wale jamaa. Siku hizi nasahau sana vitu kwa style hii.
mbona hiyo ni kawaida ukiwa na mambo mengi kichwani!
 
Baba yangu Mdinyakobe Kimario, ambaye ni mwanasaikolojia alinifundisha kitu kinachoitwa 'Halo Effect', yaani hali ya mtu/watu kuamini kuwa mtu akiwa expert kwenye kitu kimoja basi anakuwa expert kwenye vitu vingine vyote.

Kwa mfano, mimi ni expert kwenye masuala ya nyeto lakini Wana-JF wengi wanaamini kuwa Mimi pia ni expert wa vitu vyote, ndiyo maana wakati mwingine wananipa heshima nisiyostahili 😂.

Sasa hii story ya Albert Einstein imenikumbusha hili.

ShesRise_1,
Seran.
kumbaf sana gentleman, dah 🤣
 
Hata humu JF kuna member,leo ataanzisha uzi akiwa yeye ni KE halafu baada ya siku kadhaa ataanzisha uzi mwingine akiwa yeye ni ME,

Kusahau kupo wakuu.
 
Haya mambo ya Einstein yananikuta sana siku hizi. Mfano leo mchana nilotoka nyumbani kwenda salon, nikiwa nimepanga nikitoka ninunue sundries, mkaa wa home kisha chakula cha kuku na drinker moja ya kuongeza bandani kisha nipitie kwa wanunua mali used niwaoneshe picha ya madirisha niliyoyabadilisha hivi karibuni, tukikubaliana bei waje wayachukue.

WAkati nimerudi nimepark home nayaona tena yale madirisha backyard ndio nakumbuka sijapitia kwa wale jamaa. Siku hizi nasahau sana vitu kwa style hii.
Ni hali inatokea mkuu.. ukiona inaanza kua mara kwa mara na haswa kwenye maswala ya msingi adi inaleta impacts chukua hatua.
 
Naona kama inakuwa too much. Mara nyingi natoka home napanga nifike carwash niache chombo changu kisha nitembee kwenda ofisini.

Nikisha keti kwenye kiti ofisini ndio nakumbuka chombo sijaiacha car wash kama nlivyopanga.
 
Back
Top Bottom