Albert Einstein amepoteza tiketi kwenye treni

Albert Einstein amepoteza tiketi kwenye treni

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
698
Reaction score
1,632
Siku moja, Albert Einstein alikuwa ndani ya treni akitoka Chuo Kikuu cha Princeton. Kondakta akaanza kupita kukagua tiketi za abiria mmoja mmoja. Alipomfikia Einstein, mzee akaanza kupekua mifuko ya koti lake tiketi haipo.

Akaingia mifuko ya suruali, akatafuta ndani ya koti lake dogo la safari, wapi! Hakuna kitu. Mwishowe akaanza kuitafuta hata kwenye kiti alichokuwa amekalia.

Kondakta alipoona vile, akamwambia kwa heshima
“Dr. Einstein, mimi nakujua vizuri. Kila mtu hapa anakujua, na nina uhakika kabisa ulinunua tiketi. Usiwe na wasiwasi, achana nayo.”

Einstein akaitikia kwa kichwa na kumshukuru. Kondakta akaendelea na kazi yake ya kukagua tiketi za abiria wengine. Lakini alipokuwa karibu kutoka nje ya lile behewa, alipiga jicho nyuma na kumuona Einstein amepiga magoti chini, bado anatafuta ile tiketi uvunguni mwa kiti.

Kondakta akashangaa, akarudi tena na kumwambia:

“Kama nilivyokwambia, kila mtu anakujua wewe ni nani. Hakuna shida kabisa. Huhitaji kuhangaika kuitafuta hiyo tiketi.”
Einstein akainua kichwa chake, akatabasamu na kumjibu,

“Asante sana rafiki yangu. Mimi pia najua mimi ni nani. Lakini shida ni kwamba, sijui naenda wapi! Ndio maana naitafuta hii tiketi kwa udi na uvumba nijue safari yangu inaishia wapi.”

Story hii inatufundisha kuwa Hata uwe na akili gani ya kutatua magumu ya ulimwengu, bado unaweza kukwama kwenye vitu vidogo kama kujua kituo unachoshukia!
 
Attachments

  • Albert.jpg
    Albert.jpg
    7.7 KB · Views: 13
Dah inasikitisha sana, nimelia mno kusikia alikuwa hajui anakoenda 😭

Natamani Seran angekuwepo Miaka hiyo ili amchukue akampe hifadhi kwake mana Nasikia anapenda vibabu vyenye iq kubwa 😎
Baba yangu Mdinyakobe Kimario, ambaye ni mwanasaikolojia alinifundisha kitu kinachoitwa 'Halo Effect', yaani hali ya mtu/watu kuamini kuwa mtu akiwa expert kwenye kitu kimoja basi anakuwa expert kwenye vitu vingine vyote.

Kwa mfano, mimi ni expert kwenye masuala ya nyeto lakini Wana-JF wengi wanaamini kuwa Mimi pia ni expert wa vitu vyote, ndiyo maana wakati mwingine wananipa heshima nisiyostahili 😂.

Sasa hii story ya Albert Einstein imenikumbusha hili.

ShesRise_1,
Seran.
 
Baba yangu Mdinyakobe Kimario, ambaye ni mwanasaikolojia alinifundisha kitu kinachoitwa 'Halo Effect', yaani hali ya watu/watu kuamini mtu akiwa expert kwenye kitu kimoja pia anaweza kuwa expert kwenye vitu vingine.

Kwa mfano, mimi ni expert kwenye masuala ya nyeto lakini Wana-JF wengi wanaamini kuwa Mimi pia ni expert wa vitu vyote, ndiyo maana wakati mwingine wananipa heshima nisiyostahili 😂.

Sasa hii story ya Albert Einstein imenikumbusha hili.

ShesRise_1,
@ seran.
Ukiwa mpiga nyeto, automatically unajua mengi
 
Baba yangu Mdinyakobe Kimario, ambaye ni mwanasaikolojia alinifundisha kitu kinachoitwa 'Halo Effect', yaani hali ya mtu/watu kuamini kuwa mtu akiwa expert kwenye kitu kimoja basi anakuwa expert kwenye vitu vingine vyote.

Kwa mfano, mimi ni expert kwenye masuala ya nyeto lakini Wana-JF wengi wanaamini kuwa Mimi pia ni expert wa vitu vyote, ndiyo maana wakati mwingine wananipa heshima nisiyostahili 😂.

Sasa hii story ya Albert Einstein imenikumbusha hili.

ShesRise_1,
Seran.
Baba yako anaitwa mdinya kobe sasa nimeelewa kwanini una hizo akili😅

Hiyo picha nyingine naona kivuri 😢
 
Back
Top Bottom