Albam ya Invincible ya Michael Jackson

Albam ya Invincible ya Michael Jackson

Dim Ray

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2019
Posts
320
Reaction score
249
Habari za muda huu? Matumaini yangu ni kwamba mko na afya njema. Kwa waliopata maswaibu Mungu awape nguvu, hata hayo pia yanapita.

Straight to the point, leo ninamzungumzia mwanamziki mashuhuri ambaye wengi bado wanamuita "King Of Pop", Michael Jackson aliyezaliwa mwaka 1958.

Kwenye familia yao walizaliwa watoto tisa, kaka 5, dada watatu na yeye, lakini pia yawezekana wangekua kumi sema kuna mmoja wa watoto wa Baba na Mama ake Michael aliyefariki tu baada ya kuzaliwa.

Mama yake Michael Jackson alikuwa ni Shahidi wa Yehova, na mwanamziki (ili kupata kipato) na baba yake alikuwa mpambanaji (hakuwa anafahamika sana, sijajua alipambana kimtaa au vipi)

Familia yao ilimezwa na ukata mkubwa wakiwa na vyumba viwili vya kulala kwa watoto tisa. Baba yao alikuwa na kipaji cha mziki kizuri na muda mwingi aliwafundisha wanawe muziki lakini kaka ake Micjael, Jermaine anathibitisha kwamba MJ alichezea sana bakora kutoka kwa babaye.

Kama familia ya kimziki kaka zake Michael Jackson akiwepo naye ,waliunda kundi la Jackson 5.............
Hayo sio yalio nileta jambo lenyewe liko hapo down 👇👇

Kuna albamu ya Invincible ya M.J inayotajwa kutumia $30 million kuiandaa inaonekana mkwanja mrefu ,ingawa ilipata msuguano latika kui 'release' kutokana na Sony ambayo ilikuwa record label ilokuwa na usimamizi wa kazi za M.J kutaka kupata MGAO mkubwa.
 
nitaisoma badae


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkuu, kwa mpangilio wa mawazo ulivyo kwenye uzi huu, ni lazima ulikuwa unapata sifuri kwenye uandishi wa essay. Yaani main point unaiweka kwe conclusion kabisa!😀😀😀
Hata ninachosomea saizi hakina mauzauza ya Essays
 
Hata ninachosomea saizi hakina mauzauza ya Essays
Mkuu uandishi una kanuni zake, hata kama ukiwa unasomea kuchanaganya makemili, unapohitajika kuandika kitu lazima ufuate taratibu za uandishi ili ueeze kueleweka. Ona sasa watu hawaelewi umeandika nini.
 
Mkuu uandishi una kanuni zake, hata kama ukiwa unasomea kuchanaganya makemili, unapohitajika kuandika kitu lazima ufuate taratibu za uandishi ili ueeze kueleweka. Ona sasa watu hawaelewi umeandika nini.
Angalia juu ☝️☝️☝️☝️
 
Main point ilikua ni Album ya Invisible,, lakini hujaelezea chochote kuhusu iyo album zaidi ya kubaniwa na Sony sijui,,Hujasema album ilikua na ngoma ngapi na zipi?ilitoka mwaka gani?mauzo yake yalikuaje?na vitu kaa izo man.
 
Maskini bana mnashangaa vitu vidogo vidogo sana,sasa hiyo $30M huwa naitumia kila weekend
 
Back
Top Bottom