PreGE2025 ALAT yawataka madiwani kufanya mikutano ya hadhara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Murshid Nzege, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa madiwani nchini kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wananchi kuhusu maendeleo yaliyofanikishwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya mikutano ya hadhara kuanzia vitongojini, vijijini, na mitaani.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Nzege amebainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu Rais Samia aingie madarakani, yakiwemo ujenzi wa madarasa, ajira kwa madaktari na walimu, pamoja na ufanikishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Alisema ni jukumu la madiwani kuwahabarisha wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

"Hili litawasaidia wananchi kutambua jinsi Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyotekelezwa kwa vitendo, kwani yapo maendeleo yanayoonekana na mengine ambayo hayajaonekana moja kwa moja, kama vile ajira mpya kwa Watanzania," amesema Nzege.

Akitoa mfano, amesema kuwa katika Halmashauri ya Bukoba, kulikuwa na vijiji 94, lakini wakati Rais Samia anaingia madarakani, vijiji 40 vilikuwa na upungufu wa watendaji. Hata hivyo, hadi sasa, hakuna kijiji kisicho na mtendaji. Aidha, upungufu wa walimu na wahudumu wa afya pia umepungua kutokana na ajira mpya zilizotolewa na serikali.

Screenshot 2025-03-19 174521.png
 
Alikuwa wapi huyu mbwiga? Diwani ni mwakilishi wa wananch katika eneo husika je kuna kipindi cha kufanya mikutano au ni muda wote wa uongozi wao kwa ajili ya feedback
 
Wakuu,

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT), Murshid Nzege, amesema sasa ni wakati mwafaka kwa madiwani nchini kuhakikisha wanatoa taarifa kwa wananchi kuhusu maendeleo yaliyofanikishwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kufanya mikutano ya hadhara kuanzia vitongojini, vijijini, na mitaani.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Nzege amebainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu Rais Samia aingie madarakani, yakiwemo ujenzi wa madarasa, ajira kwa madaktari na walimu, pamoja na ufanikishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Alisema ni jukumu la madiwani kuwahabarisha wananchi kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.

diwani .png

"Hili litawasaidia wananchi kutambua jinsi Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inavyotekelezwa kwa vitendo, kwani yapo maendeleo yanayoonekana na mengine ambayo hayajaonekana moja kwa moja, kama vile ajira mpya kwa Watanzania," amesema Nzege.

Akitoa mfano, amesema kuwa katika Halmashauri ya Bukoba, kulikuwa na vijiji 94, lakini wakati Rais Samia anaingia madarakani, vijiji 40 vilikuwa na upungufu wa watendaji.

Hata hivyo, hadi sasa, hakuna kijiji kisicho na mtendaji. Aidha, upungufu wa walimu na wahudumu wa afya pia umepungua kutokana na ajira mpya zilizotolewa na serikali.

"Serikali imeenda mbali zaidi kwa kupanga kuhakikisha kila kijiji kinakuwa na mhudumu wa afya aliyepata mafunzo, ili kusaidia jamii husika pale kunapotokea changamoto za kiafya," ameongeza Nzege.

Ameeleza pia kuwa, kwa sasa wananchi wanatoa maoni yao katika halmashauri kwa uhuru zaidi, huku kipato cha wananchi kikiongezeka kutokana na maboresho katika mifumo ya masoko nchini.

Source: Nipashe
 
Ila Tz kuna makolokolo mengi sana. Huyu naye katoka wapi😅😅
 
Back
Top Bottom