Alan Walker, msanii wangu bora wa EDM

Ngareroo

JF-Expert Member
Aug 11, 2019
2,049
2,249
Habari zenu wadau wa jukwaa hili. I hope mko njema kabisa hapo.

Mimi ni mmoja kati ya raia ambao nafuatilia sana aina mbalimbali za muziki duniani. Nafuatilia Bongo Fleva, Hiphop, Afro Beat, Trap, Emo Trap ile ya kina marehemu XXX Tentacion, Juice Wrld n.k. Reggae, Dancehall, Kwaito na vitu ka' izo.

Sasa bhana kuna muziki unaitwa Electro Dance Music/House (EDM). Huu ni muziki ambao mdundo/beat ndo inaongea zaidi kwenye nyimbo kuliko mashairi.

Aina hii ya muziki hufanya zaidi kina David Guetta, DJ Snake, Major lazer, DJ Black Coffee, Dimitri Vegas na wengne shazi.

Lakini chalii m'noma kabisa kwenye izi mbanga ni Alan Walker au DJ Walkzz. Huyu ni Muingereza aliezaliwa Norway mwaka 1997 (23 yrs). Ni DJ, Producer, Mwandishi wa nyimbo. Alianza kujiingiza katika industry ya music 2012 akiwa na miaka 15. Chalii nam'nyali kinyama kunako EDM music.

Alan Walker ndiyo huhusika kutengeneza beat, kuandika nyimbo pamoja na kutafuta muimbaji atakayefaa katika madude yake, but umiliki wa nyimbo unakua ni wake kulingana na mkataba na makubaliano kama afanyavyo DJ Khaled.

Ukiskiliza ngoma zote za mhuni ni kali, yaani akuna ngoma ya kiree 'ata moko. Ngoma kama Faded ambayo hadi saivi ina views zaidi ya bilioni mbili YouTube, pia ilienda Multi-platinum kwa mauzo kwenye zaidi ya nchi 20 duniani.

Ngoma zingine kali ni On My Way, Dark Side, Alone, Sing Me To sleep, Nothing At All, Diamond Heart na ninayoikubali zaidi inaitwa Unity.

Mwaka 2018 alikua nafasi ya 36 kati ya MaDj's/ Producers 100 bora kabisa kwa mujibu wa "DJ Mag's", ambapo pia mwaka huohuo (2018) aliachia album yake kubwa kichizi inayoitwa Different World.

Lakini pia hafanyi kazi peke yake; hushirikiana hasa katika uañdishi na dingilii m'bad kabisa anaitwa Gunna Greve ambae ni producer, muimbaji na mwandishi pia wa ngoma.

Huyu ndo father wa music industry ya Norway pia Sweden. Ndiye founder na manager wa kampuni ya muziki ya MER ambayo ndo ilimtoa pia chaliangu Alan Walker.

I feel like am done, but kama una chochote cha kuongeza kumhusu, karibu.

Halafu sijui kwanini often huwa anapenda kujifunika sura na mask ispokuwa macho?

@NgarenaroBoy.

220px-Alan_Walker.jpeg
FB_IMG_15798944800443046.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alan walker is the best. Marshmello najitahidi sana kumsikiliza coz nae ni mwana EDM lkn hajawahi nikosha.

Nikiwa nafanya coding midnight huku nasikiliza ngoma za Alan huwa nahisi niko dunia fln hv ambayo haielezeki kiukweli.

My playlist:
Faded
Lost control
Alone
Diamond heart
Alone II
Lily
Sing me to sleep
All falls down
Legends never die remix

etc...
 
Back
Top Bottom