Alalamika kubadilishiwa Mtoto Aliyekufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alalamika kubadilishiwa Mtoto Aliyekufa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Nov 26, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Alalamika kubadilishiwa Mtoto Aliyekufa
  [​IMG]
  Wednesday, November 25, 2009 2:00 PM
  MWANAMKE mmoja Fatuma Mohamedi [26] amewalalamikia manesi wa hospitali ya Mwananyamala kuwa wamembadilishia mtoto wake aliyejifungua akiwa hai na kupewa mtoto mfu baada ya muda mfupi alipotoka kujifungua.Mwanamke huyo alilalamika na kusema kuwa alifika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kujifungua na alipokelewa na manesi kama kawaida na taratibu za kumuandaa mama mjamzito katika hali ya kujifungua kama kawaida.

  Alisema muda wa kujifungua ulipowadia alijifungua kama kawaida na alijifungua salama mtoto wa kike akiwa hai na manesi walimuonyesha mtoto wake.

  Alisema muda mfupi alipewa mtoto wake na alimnyonyesha na kumuona ni mtoto aliye salama kabisa ambaye hakuwa na kasoro yeyote.

  Alisema cha kushangaza mtoto alichukuliwa na manesi katika taratibu za kumpima na taratibu nyingine na yeye kwenda wodini kupumzika.

  Mara baada ya muda manesi waliwaita ndugu zake na kuwambia kuwa mtoto aliyejifungua ndugu yao amefariki na kuonyeshwa mwili wa mtoto huyo ukiwa na majeraha kichwani.

  Alisema ndugu hao walimwambia ndugu yao huyo kuwa mtoto aliyejifungua amefariki na kumtaka waende nyumbani, ndipo alipowaambia ndugu zake kuwa ametoka kumnyonyesha mtoto wake muda si mrefu na alikuwa mzima.

  Mzazi huyo alichachamaa na kuwataka manesi wamuonyeshe mtoto wake na kuonyeshwa mwili mfu wa mtoto huyo ukiwa na vidonda na majeraha kichwani na dada huyo kuchachamaa na kusema mtoto huyo hakuwa wake na kwenda kutoa taarifa kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo kwa malalamiko zaidi.

  Naye Kaimu Mganga Mkuu wa hospitali ya Mwananyamala, Sofia Ngonyani amesema tukio hilo linafanyiwa kazi kwa haraka zaidi na tarifa hiyo imekwishapelekwa kwenye ofisi ya mganga mkuuu wa manispaa ya kinondoni na tume imeundwa kuchunguza ukweli wa tukio hilo.

  Source:Nifahamishe
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Huko Mwananyamala vipi tena?

  haya tunasubiri taarifa ya DMO
   
Loading...