Ala mkongoto na kulazimishwa kuoa

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Sep 22, 2009
1,282
247
Mwanaume mmoja wa nchini India ambaye alitaka kuvunja uhusiano na bi harusi kwenye dakika za mwisho kabla ya harusi, alipewa mkong'oto na kulazimishwa kumuoa bi harusi wake.Video iliyoonyeshwa na televisheni ya habari ya India ya News 9 ilimuonyesha mwanaume huyo toka mji wa Mysore akilia huku akionyesha kusikitika sana kwa kuzikuna nywele zake wakati alipokuwa akilazimishwa kumuoa bi harusi wake.

Taarifa zilisema kwamba mwanaume huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke huyo kwa miaka 10 lakini ghafla aliuvunja uhusiano wake wakati mwanamke huyo alipomtamkia kuwa anataka kufunga naye ndoa.

Mwanaume huyo alikataa kufunga ndoa na mpenzi wake huyo na ndipo alipolazimishwa kinguvu ahudhurie sherehe ya harusi ambayo mwanamke huyo aliiandaa.

Kundi la vijana walisikia kuwa mwanaume huyo amekataa ombi la kufunga ndoa na ndipo walipoamua kumlazimisha kinguvu ahudhurie sherehe za harusi.

Katika video hiyo mwanaume huyo anaonekana akisukumwa na kupigwa makofi wakati wa safari ya kutoka kwenye makazi yake hadi kwenye hekalu ambalo harusi hiyo ilikuwa inafanyika.

Pamoja na bwana harusi kuonyesha wazi kuwa hayuko tayari kuoa, bi harusi hakuonyesha huzuni yoyote zaidi ya uso wake kuonyesha tabasamu wakati wote wa sherehe ya harusi.

CHINI ni VIDEO ya tukio hilo.

VIDEO - Apewa Mkong'oto na Kuozeshwa Mke Kinguvu






 
jinga kweli kweli .. sawa sawa walivyofanya bora india bado kuna watu wenye utu .. hapa kwetu .. ingekua imetoka hiyo
 
Back
Top Bottom