Al-Qaeda wampa onyo kali mtoto wa mfalme wa Saudi Arabia

Man, ogopa sana nchi kama Saudi Arabia au Pakistan!!

Tofauti na Iran ambao ni political hardliners; Saudi Arabia na Pakistan ni religious extremists! Nchi za namna hii zinakuwa na extremists mpaka ndani ya system na ndio mana Marekani/CIA walipata shida sana kumpata Osama bin Laden!

Kwamba, ingawaje CIA na Pakistan Intelligence Service ni allies kwa miongo kadhaa na wote walikuwa wanamsaka Osama lakini some members of Pakistan Intelligence Service walikuwa wanatoa info kwa Osama!

Hii maana yake nini?

Of course a new prince anaweza kuwa kipenzi cha wengi especially vijana wa kileo lakini hiyo haiwezi kuwa guarantee ya usalama wake kwa sababu naweza kuwa traded na insiders ambao ni extremists!

Raia wa kawaida hawana ubavu wa kumlinda!!

Remember this post: kwa sera za huyu jamaa anahatarisha sio tu usalama wake bali ufalme mzima! Kwamba, anaweza kusababisha hata mapinduzi sawa na yale ya Iran in 1979 yatakayohitimisha utawala wa kifalme nchini Saudi Arabia!
sawa sheikh yahaya kwahiyo atauawa lini tujuze ,usije ukaanza wewe ukamuacha
 
we ndo pumba kabisa sasa hayo uliyosema kuna la maendeleo hapo

Ili uwe na maendeleo sawia lazima narudia lazima watu wako wawe huru,

Kwani mwanamke kuendesha gari au kuwatch football kunaharibu vipi imani ya kiislam?

Kugeuza msikiti kuwa cenema hall uislam unaathilika vipi? Je ingegeuzwa kua kanisa mngesema nn
 
nashangaa kwani kwenye hilo hall wameambiwa kutaoneshwa xxx je kama kutaoneshwa movie za mafunzo,dini nk na kuelimisha.
Ili uwe na maendeleo sawia lazima narudia lazima watu wako wawe huru,

Kwani mwanamke kuendesha gari au kuwatch football kunaharibu vipi imani ya kiislam?

Kugeuza msikiti kuwa cenema hall uislam unaathilika vipi? Je ingegeuzwa kua kanisa mngesema nn
 
Kwa karne nyingi mno Wasaudia wamefanywa kuwa "Misukule" ndani ya nchi yao wenyewe, wamenyimwa mambo mengi kibabe tu kwa kisingizio cha dini.

Mara kwa mara Wasaudia wamelazimika kwenda nje ya nchi yao ili ku-intaract na watu wa mataifa mbali mbali kwani nchi yao imekuwa "The Hermit Kingdom".

Wamelazimishwa wote waonekane ni jamii ya imani moja tu yaani Islam hata pale ambapo kiuhalisia sio hivyo, sasa wanaona ni muda muafaka wa kurejesha "Sanity" ktk hiyo nchi.

Kama kuna wachache wenye imani kali ya kidini "Fundamentalists" watakaojaribu kutaka kupindua mambo ili kulazimisha itikadi yao ya kale juu ya Wasaudia wa kileo, basi ndoto yao itazimwa haraka kwani hawatapata uungwaji mkono wa Wasaudia au hata jumuia ya kimataifa.

Watu wamechoka kuona wakilazimishwa kutii sheria za karne ya nane ktk zama hizi za kupigania haki za binadamu huku hao hao wanaolazimisha watu kuzitii hizo "Brutal and Archaic Decrees" wakizivunja mchana kweupe kwa kwenda kucheza kamari na kutanua na malaya Ulaya na Marekani.
 
kwani kuna muislam kalazimishwa kwenda hapo kuangalia movie au uhuru gani umeingiliwa mkuu

Humu JF naona watu huwa tunapishana uelewa. Yeye ameingiza taratibu za kitamaduni ambazo hazikuwa zimezoeleka ndani ya Saudi Arabia. Ni kweli hajalazimisha mtu kuzifuata. Laini kuzileta karibu katika nchi ambayo wengine wanaitambua kuwa imebeba utakatifu wa Uislamu ni kuwaingiza waaminio wa Uislamu lkatika majaribu makubwa. Ni sawa na kupanda mwendo kasi halafu unafungua container yako na kula chips na kuku wakati wengi mule ndani wamefunga. Yeye anahimiza uhuru lakini uhuru huo wake unaivuruga dini ya Uislamu. Huo ndiyo ukweli.
 
Unadhani ukiingia kwenye mwendo kasi ukifungua chips ukila kuna kosa ? Wala hutaulizwa ukitamani ni tamaa zako, mbona kwaresma waislam huwa mnakula popote, uhuru pia ni sehemu ya Amani, amani ni ibada
 
Mimi sio Muislamu ndugu. Mkiharibiana imani shauri yenu. Mkipoteza maadili yenu shauri yenu. Zanzibar wao ukilĺa hadharani ni kukiuka utaratibu wao. Kwani nawatetea inafaidi nini? Mimi Mkristo jina ninalotumia linashiria hivyo. Mimi kwangu sina shida hiyo? Alaah!
 
Kama kweli, huyo inawezekana kashagundua Mungu hayupo ndiyo maana anageuza msikiti kuwa cinema na anaalika wrestlers. Watu wale bata tu hapahapa duniani wamalize mambo.

Hakuna kusubiri mbingu.

Tengeneza mbingu yako hapahapa duniani.
Wewe unasema amegundua Mungu hayupo na wengine wanasema amempokea Yesu.

Kwa maana hayo matendo anayofanya yanaendana na Atheism na Imani ya Yesu.

Hivi kuna mahusiano gani kati ya atheists na Christians?
 
Back
Top Bottom