al masry wako fair play

al masry wako fair play

WARBOYy

Member
Joined
Mar 19, 2025
Posts
68
Reaction score
84
salamu ndugu zangu..!?

al masry kwa nilivyowaona wanacheza mchezo mzuri wa fair play.

katika mchezo uliopita pengine unaweza kusema walikuwa na uhitaji wa magori mengi lakini hili nakataa nakataa kwasababu wao hawakuwa wamiliki wa mpira tena kwa yale mashambulizi ya simba ni wazi wangekuwa wanapoteza mda na kulizika na walichokipata.

kuna wale madogo wanaopelekeza mipira walikuwa wanafanya kazi vizuri sana, nilikuwa nategemea mipira kuingia uwanjani hovyo lakini hawakufanya hivyo.

hivyo tutegemee mchezo mzuri nyumbani warabu hawatafanya mambo ya ajabu(al masry)


na hilo ni funzo zuri kwa timu zetu hasa magoli kipa, unakuta mtu anapoteza mda dakika tu za mwanzoni huo mda ataujutia akitanguliwa goli, sikuona sababu za camara kupoteza mda dakika zile.

kwanza kuna madhara ya kimabadiliko ya kifikira kwa mpinzani, mwazo alikuwa anawaheshimu kwa kujua kwamba hawa ni miamba wameongoza kundi,wazoefu wa haya mashindano na sifa nyingine nyingine lakini kutoka na kile kitendo teari wanaanza kuwaza yao kichwani

na ingetokea simba anahitaji ushindi tu na akafunga goli dakika ya 2 si ajabu kumuona camara na baadhi ya tuchawa twake kuanza kupoteza mda na baadhi ya mashabiki kwenye kibanda umiza ukisikia "lalaaaa" shenzi kabisa.. majamaa yanasawazisha pale kwenye 80 alooo...!! mtajuta. kiufupi wakati wa kupoteza mda ni pale kwenye 75 napo ndio mnaanza anza.

hizo nyingine zote niza kupambana kufunga magoli ili hata mkishitukizwa kamba bado kunakuwepo mda wa kutosha kuwapelekea mto wapinzani

anyway..! good luck to my club and god help them to achieve their goal to qualify the quarter final.

thanks
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom