johnsonlinda650
Member
- Oct 27, 2014
- 9
- 1
Ndugu zangu naomba usaidizi, najua kuna wale wataikejeli shida yangu lakini nina imani kunae atakae elewa uchungu ninao moyoni, nina mpenzi wangu tulopendana sana, miezi ilopita mpenzi kaniita kule Malindi tuzungumze, ilibakia miezi 4 tufunge pingu za maisha kama tulopanga hapo mwanzo, lakini lo!
Nilodhani ndilo kumbe silo, mpenzi kanambia yamekwisha kati yetu kwani amemuona mrembo wa Nairobi, nilipata pigo la moyo ndugu zangu kwani sikumkosea kamwe, naumwa sana kwani mapenzi yetu,kazi niliwacha ndipo niwe na wakati na mpenzi,alikuwa asha nipeleka nyumbani kwa wazazi na ndugu zake.
Nilikuwa nimewajulisha jamaa na marafiki wangu, naona maumivu sana moyoni, naomba tafadhali ajuae daktari sugu wa kienyeji anisaidie kukirudisha kikombe changu,nimetafuta msaada kila mahali lakini Kenya matapeli tupu.
Nawaomba haswa ndugu zangu wa Tanga nisaidieni,kwani akufaae kwa dhiki ndiye rafiki, nitashukuru sana.
Asanteni.