Akisimama Makonda Mungu kasimama, je akisimama Magufuli nani kasimama?

Abul Aaliyah

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
2,489
2,000
Wala tucmlaumu yy tumlaumu aliyempa hyo nafac ya dezo na kama anampigia CMU za pongez unategemea nn? Hii nch wapo weng ambao n wahanga Wa mosh Wa mwenge
 

Joto Balaa

JF-Expert Member
Sep 14, 2016
1,143
2,000
kuna link yeyote labda tusome au tuone clip Makonda akijifananisha na Mungu?
Sio kwamba kajifananisha mkuu ila kwa faida yako isikilize hiyo clip ili ujue uchangie nini. Clip imesambaa sana hata humu JF imewekwa kitambo tu.
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,433
2,000
Jamaa ana akili mbovu sana hata kuweza kujifananisha na Mungu. Cheo kimemtia wazimu huyu hata kujiona anaposimama yeye ni kama kasimama Mungu. Ana akili ya kushikiwa ya kuropoka kama cherehani matokeo yake kuongea maneno yanayotushangaza sana Watanzania wengi.
Juzi wenyeviti wa Tegeta,Kunduchi,mbezi,Mikochen,goba na kawe waliungana wakampiga kamati za Ufundi kali asipite huko akawaweka ndani kutokana na kuwa na kesi nyingi za uuzaji viwanja vya wazi na maeneo ya umma na watu binafsi, hivyo huenda makonda alipagawa kutokana moto wa hao wenyeviti wa serikali za mitaa wa huko.
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,433
2,000
Hata mitume na manabii hawakuwahi kutamka maneno hata. Heko watu wa Dar es salaam kwa kuwa na Mungu karibu yenu kupitia Makonda.
Mashehe, mapadre na wachungaji katafuteni kazi nyingine Dar sasa wakitaka toba au msaada wa Mungu watapitishia kwa Makonda kwani ndio njia rahisi maana alipo simama yeye hapo hapo ndipo alipo. Hili jambo litangazwe duniani na hakika ulimwengu utafurika hapa kuja kwa Makonda na nchi itanufaika kwa chanzo hicho kipya cha mapato
Mungu mtu kwa sasa ni makonda
 

ushuzi.1

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
8,433
2,000
Juzi makonda alikuwa kama kachanganyikiwa vile hakuwa ktk hali ya kawaida,Siri ya kupagawa ni nguvu ya kamati za Ufundi toka kwa wenyeviti wa serikali za mitaa ambao hawakutaka makonda aende kwenye maeneo yao kuwatia Aibu mbele za watu.
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,643
2,000
Kama mtakumbuka hotuba moja ya Mwl akiongelea muungano alisema '' kutenda dhambi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukianza kula utaendelea kula tu'

Hili la Makonda si geni labda ugeni wake ni namna linavyokaliwa kimya na wahusika
Ugeni wake ni jinsi anavyoungwa mkono 100% hata pale anapopotoka

Turudi katika historia kidogo sana

Makonda akiwa mwenyekiti Chipukizi alijitokeza wazi na kumsema sana Lowassa
Shambulio kama kada halikuwa na tatizo! tatizo ni lugha yake isiyovumilika kirahisi

Makonda akaenda Ubungo Plaza akiwa na kundi la 'wahuni' .
Tunajua kilichotokea kwa Mzee Warioba, Butiku na wengine.
Likaonekana jambo la kawaida kwasababu alisimama na chama

Makonda akatoa kauli ya Polisi wapige tu yeye atajibu. Bila kujali sheria za nchi na leo tunajua ni kwasababu ya ukaribu na mungu, hakuna,ikaonekana kawaida

Makonda majuzi kamshambulia kwa maneno kamanda wa kanda na wenzake wa chini
Hakuna aliyestushwa na ukiukwaji wa juu wa team work na collective responsibility
Hakuna aliyeona ufa alioutia akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa

Makonda kapita Kinondoni kutoa kauli ya 'ukaribu' na mwenyezi mungu ingawa hakuna vitabu vitakatifu vinavyoonyesha mungu akitoa matusi hata alipoudhiwa na wanadamu

Haya ni kwa uchache sana lakini yanalingana na kauli za Mwl ya kula nyama ya mtu

Katika hili kumlaumu Makonda pia ni kosa, hakuna anayemsaidia na hakuna anayeshtushwa. Makonda ni kijana mdogo kiumri na kisiasa, anahitaji malezi

Kwa haya, walezi wake kisiasa wanaomwacha atende atakalo, atukane watumishi, aamuru watu wafanyiziwe atajibu yeye n.k. ndio wanaobeba dhamana.

Wale waliompa fursa hii adhimu ya kutumikia umma na si kuudhihaki ndio wenye dhama ya ima kumweka kitako kama wanadhani anafaa au wamuondoe ili akajifunze kwanza

Nadhani Makonda hana makosa sana, ni yeye kama yeye, wapo wanaopaswa kutusaidia na hao ndio tunwashangaa hadi leo bado hawaoni tatizo
 

Mgango

JF-Expert Member
Oct 27, 2016
2,345
2,000
Mungu ninayemfahamu na kumhubiri ana nafasi tatu Baba Mwana na Roho Mtakatifu. Sasa huyo mnayemsema mimi simjui. Labda ni wa upande wa pili
 
  • Thanks
Reactions: PNC

Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,683
2,000
Huyu atapinda huo mdomo kama Seif Khatib siku sio nyingi

Ila mbona kama nimemuelewa Makonda ,Alisema mimi nikisamama mahali Mungu amesimama ,yaani kwamba alipo yeye Mungu yupo naye au mimi ndio sielewi ?

Hakuna sekta ilikuwa imeoza kama ardhi ,alitakiwa awatie vibao kabisa hao washenzi
 
Top Bottom