Akiri kumuua nduguye, afungwa miaka miwili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akiri kumuua nduguye, afungwa miaka miwili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya imemhukumu mkazi wa Kijiji cha Kamsamba Wilaya ya Mbozi, Geofrey Christopher ( 22) kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.

  Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Batueli Mmilla alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka kwamba Mei 25 mwaka juzi, Christopher alimuua Oscar James.

  Alisema ametoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

  Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Christopher na James walikuwa na uhusiano wa kindugu.

  Siku ya tukio walitoka pamoja kunywa pombe katika kilabu cha pombe za kienyeji kiitwacho Mgusha.

  Mahakama ilielezwa kuwa, baada ya muda mfupi kutoka kwenye kilabu hicho wakienda nyumbani kwao, ulizuka ugomvi kati yao.

  Mwendesha Mashitaka Epafras Njau alidai kwamba James (aliyeuawa) alimmwagia pombe Christopher baada ya kunyimwa Sh 10,000 kwa ajili ya kununulia pombe ya kienyeji .

  Ilidaiwa kwamba, mshitakiwa alichomoa kisu mfukoni na kumchoma sehemu ya mgongo ambapo polisi walipomhoji, alikiri kumuua mwenzake bila kukusudia.

  Wakati huohuo Mahakama hiyo imemwachia huru, Abdallah Siraji (18) aliyekuwa akishikiliwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.

  Awali ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka, Faraja Msuya kuwa Juni 21 mwaka juzi, Siraji ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Totowe wilayani Chunya alimuua rafiki yake, Mashaka David.

  Ilidaiwa kwamba, Siraji alimpiga risasi kwa bunduki aina gobole katika kijiji cha Kambi Katoto wilayani Chunya wakati wakitoka kuwinda.
   
 2. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,921
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Iwe fundisho kwa wengine akina nani hao?? Kwasababu akina chenge wanaua lakini wanatozwa laki 7,...dah inauma kweli...wakubwa wengi wapo juu ya sheria tanzania hii...:frusty::frusty:
   
Loading...