'Akina Mzee Mwanakijiji' ni wavivu kufikiri

naelewa na ninaheshimu maoni na busara zako kwa chadema na watanzania kwa ujumla.hata mimi natambua chadema kama iliivyo chama kingine cha siasa inahitaji kukosolewa sasa na baadae.natambua tabia ya wanasiasa ni ile ile.

Lakini naamani unatambua ni wakati gani wa kutoa maoni gani ,kwa lengo gani na kwa faida gani na ya nani?

Tukubaliane kuwa kama kweli tumedhamiria kuleta mabadiliko ni lazima tuchague kuusadia upande unaotaka mabadiliko.hatuwezi kuusaidia upande huo kwa kutoa maoni ya kuumiza na kusaidia adui huko ni kumpa nguvu adui.kwa maneno mengine tusilazimishe mtoto kwa kumpa matonge ya ugali(ndani ya mwezi mmoja) huku anatakiwa aendelee kunyonya kisa anatakiwa kula ugali baada ya miezi sita.
Kimsingi tumuwekee lengo la kula ugali ndani ya miezi sita huku tukimzoesha uji,matonge madogo madogo na hatimaye matonge makubwa.
Unachojaribu au ulichajaribu kufanya ni kumpa mtoto huyu ugali mkubwa na unataka aanze kuumeza from day 1 to six months!ili uweze kunyanyua kilo 100 ni lazima uanzie kumi!

Nasisitiza lengo la cdm kushika nchi ni 2015 leo wamenyanga'nya tatu kesho wayanyanga'nya kumi lakini 2015 ni lazima wafikie lengo.

Sio wakati wa Maoni ya kuwalaumu viongozi wa chadema na kuona wameshindwa ndio maana reaction ya watu hapa jamvini imekuwa kali dhidi yako.

Nadhani wewe(stand to correction) ni mmoja wa walioshauri cdm ipeleke nguvu zake mikoani na vijijini,chadema ilisikia na leo imepata matokeo haya,sasa unayabeza tukuelewe/tuwaelewe vipi?

Unajua kwanini watu hawawalamikii wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zaidi bali Rais na mawaziri wake? Kama umegundua mara tatu sasa Kikwete kalazimika kubadili baraza la mawaziri. Uongozi wa CDM unabeba moja kwa moja uwajibikaji wa matokeo yote ya uchaguzi kuanzia yale ya 2010 (ambayo kwa kweli hayakuwa mazuri sana kama watu wanavyoamini, ukiondoa yale ya Urais).
 
Tuko;4940226]Namtaja Mzee Mwanakijiji kwa kuwa yeye ni legend wa 'uchambuzi wa mambo ya kisiasa' katika vyombo vya habari. Wapo baadhi ya watu hapa Jf na kwenye magazeti ambao walitumia matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani juzi kuchambua uwezekano wa CDM kufanya vizuri au vibaya kwenye uchaguzi wa 2015. Ni jambo zuri, na wala siwapingi kwa kuwa ni mojawapoya namna ya uchambuzi wa kisiasa...
Kwahiyo tunakubaliana kuwa siyo wavivu wa kufikiri. Pengine ungeomba radhi kwa kutumia neno hilo mahali pasipostahili kama ulivyoshuhudia.
Sasa kama mtu anataka kujenga hoja na anataka hoja yake ieleweke, kuhusisha matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani na matokeo tarajiwa ya uchaguzi mkuu ujao, naomba afanye home work yake kama 'mchambuzi wa kisiasa' kweli na aje na data zilizokamilika.
Sasa hawa umeshawahukumu kuwa ni wavivu wa kufikiri, uwezo wa kuja na data wataupata wapi ili hali ni wavivu?
Maana mi Tuko nikiandika uchambuzi hapa, hakuna mtu atakayehangaika sana na kuangalia nimechambuaje, maana nani anamfahamu Tuko? (hapa Tuko anawakilisha undergrounds wengine wote wa uchambuzi wa siasa
Hivi ukiwa underground unapaswa kujifunza au kutukana?
Sasa naamini Mwanakijiji na wenzake wana uwezo wa kufanya uchambuzi wa kisayansi zaidi, kuipima CDM sasa na uwezo wake sasa na kuuhusisha na 2015 kwa kutumia matokeo ya chaguzi ndogo za udiwani
Haa! walioufanya si huo wa kivivu sasa unataka uvivu upi tena, wa kisayansi!!
Hata hivyo, naomba wazingatie confounding factors kama vile, impacts za daftari la wapiga kura mwaka 2004 kutengenezwa, na mwaka 2009/2010 kuboreshwa, impacts za demographical changes, impacts za kushuka ama kupanda kwa vyama vingine vya kisiasa, n.k...
Na pia impact za nguvu ilitotumika kwa miaka 20, impact ya migogoro ndani ya chama, impact ya kuwatangaza wagombea mapema, impact ya mikutano yenye watu wengi lakini wapiga kura wachache, impact ya uwajibikaji wa viongozi katika wilaya na mikoa.
Naamini hii ni kazi ndogo sana kwa watu ambao wapo kwenye tasnia ya habari na uchambuzi, lakini ina umuhimu sana ku-predict matokeo na mustakabali wa taifa letu baada ya uchaguzi wa 2015.
Kwa wavivu ni kazi kubwa, unaonaje kama utaifanya iwe rahisi zaidi kwa kuweka data ili kuwe na tofauti ya wivivu na underground.
Naamini, ikifanyika kazi hii, matokeo ya uchaguzi ujao hayatatanguliwa na vichwa vya habari kwenye magazeti; ..."Katika hali ambayo haikutarajiwa, matokeo ya uchaguzi yanaonyesha kwamba"...
Vichwa vya habari hutoka baada ya matokeo. Lakini pia kumbe unakubali kuwa mchango wa wavivu wa kufikiri una umuhimu eh!
Kazi kwenu
Kazi kwako mkuu Tuko
 
sasa kama hana data anaweza vipi kusema wengine tuna uvivu wa kufikiri. Angekuwa ameweka data na kuzinyambulisha tungeziangalia na kuanza kuzitorture...

point yangu ni kuwa inawezekana hana data lakini ameweka vipengele vya data muhimu za uchambuzi.
Ataridhika iwapo magwiji wa uchambuzi mtajadili kwa kutumia vipengele tajwa.ameamini mna uwezo wa kupata data husika.naomba tumuache mtoa mada na tutafute data hizo ili mjadala uwe mtamu.kama amekosea kuwasilisha tumsahihishe na turudi kwenye hoja ya msingi.
 
wewe umefanya research?

mm nimefanya research ya kutosha, watu wenye tabia ya uongo/umbea hata mtaani kwako unajua yanayowakuta. vilevile ziko kesi mahakamani watu wamefungwa na wengine wamepigwa faini kutokana na kusema uongo ulioleta madhara kwa serikali/watu wengine. nenda mahakama/polisi yoyote uliza utapatiwa
 
sisi ni wavivu wa kufikiri; angekuwa siyo mvivu wa kufikiri angekuja na hoja yake bila kebehi kwani amethibitisha uvivu wake. Sasa na wewe kutaka sisi tutafute hizo data unaonekana kuamini kuwa sisi siyo wavivu hivyo ndio maana hata wewe mwenyewe huendi kuzitafuta wakati tumeshaelekeza wapi zinapatikana - Tume ya Uchaguzi. Hapa hadi hivi sasa hakuna mjadala. Mjadala ungekuwepo kama kungekuwa na data ambazo mtoa hoja angezileta ili tuzijadili. Sasa mada aanzishe yeye sisi wengine ndio tutafute data. Akileta data tutamsaidia kuzichambua.
 
Kwa mtizamo wangu inawezekana namna Mwanakijiji alibeza kupita kiasi mafanikio haya ya CDM, Lakini mtoa mada TUKO nae kuonyesha cni mvivu wa kufikiri, ilitakiwa aje na data full akielezea namna CDM ilivoimarika (jambo ambalo naamini wameimarika compared to past) kuliko kuleta mambo ya X,Y nk
 
mm nimefanya research ya kutosha, watu wenye tabia ya uongo/umbea hata mtaani kwako unajua yanayowakuta. vilevile ziko kesi mahakamani watu wamefungwa na wengine wamepigwa faini kutokana na kusema uongo ulioleta madhara kwa serikali/watu wengine. nenda mahakama/polisi yoyote uliza utapatiwa

sasa kwanini usimsaidie mwenzio hapa kuleta hizo data ambazo wavivu kama sisi hatuwezi kuzipata? Kalete data tusaidiane kuzifanyia uchambuzi.
 
Kwa mtizamo wangu inawezekana namna Mwanakijiji alibeza kupita kiasi mafanikio haya ya CDM, Lakini mtoa mada TUKO nae kuonyesha cni mvivu wa kufikiri, ilitakiwa aje na data full akielezea namna CDM ilivoimarika (jambo ambalo naamini wameimarika compared to past) kuliko kuleta mambo ya X,Y nk

kwanini unaamini wameimarika kuliko in the past?
 
Unajua kwanini watu hawawalamikii wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zaidi bali Rais na mawaziri wake? Kama umegundua mara tatu sasa Kikwete kalazimika kubadili baraza la mawaziri. Uongozi wa CDM unabeba moja kwa moja uwajibikaji wa matokeo yote ya uchaguzi kuanzia yale ya 2010 (ambayo kwa kweli hayakuwa mazuri sana kama watu wanavyoamini, ukiondoa yale ya Urais).
umekubali kuwa kikwete ammebadilisha mawaziri wake lakini sio yeye kuwajibika!
Je kwa upande wa cdm ulitaka wawajibike kina mbowe,slaa,zitto,mnyika,lema and other top figures au wenyeviti wa matawi?(make it clear)kama ni wenyeviti wa matawi kwa nini maoni yako yalielekea kwa viongozi hawa wakuu wa chama?

2010 walifanya vibaya?kikata,kibunge au kirais?naona kama unalinganisha mambo yasiyolinganishwa mkuu.

Ungesubiri 2015 uwahukumu comprehensively!
 
Ntatumia matokeo ya kata kama 8 hivi as a Benchmark Ku msupport Tuko
Hii inaonesha kama ungekuwa ni uchaguzi wa Rais, CDM wangepiga Bao kubwa mno

KataCHADEMACCM
Kilema Kusini797736
Najara Rehan23701128
Mnero Miembeno818138
Myovizi17261498
Momba903310
Mahenge444710
Mtibwa30961372
Daraja Mbili21931324
SUM
123477216
 
Last edited by a moderator:

kama mtu hataki washinde anatakiwa kusubiri baada ya 2015; kama mtu anataka CDM ifanye vizuri anatakiwa kuanza jana kuwafuatilia..
 
Ntatumia matokeo ya kata kama 8 hivi as a Benchmark Ku msupport Tuko
Hii inaonesha kama ungekuwa ni uchaguzi wa Rais, CDM wangepiga Bao kubwa mno

KataCHADEMACCM
Kilema Kusini797736
Najara Rehan23701128
Mnero Miembeno818138
Myovizi17261498
Momba903310
Mahenge444710
Mtibwa30961372
Daraja Mbili21931324
SUM
123477216

tupatie na zile ambazo magamba walishinda.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom