Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Namtaja Mzee Mwanakijiji kwa kuwa yeye ni legend wa 'uchambuzi wa mambo ya kisiasa' katika vyombo vya habari. Wapo baadhi ya watu hapa Jf na kwenye magazeti ambao walitumia matokeo ya uchaguzi mdogo wa madiwani juzi kuchambua uwezekano wa CDM kufanya vizuri au vibaya kwenye uchaguzi wa 2015. Ni jambo zuri, na wala siwapingi kwa kuwa ni mojawapoya namna ya uchambuzi wa kisiasa...
Sasa kama mtu anataka kujenga hoja na anataka hoja yake ieleweke, kuhusisha matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani na matokeo tarajiwa ya uchaguzi mkuu ujao, naomba afanye home work yake kama 'mchambuzi wa kisiasa' kweli na aje na data zilizokamilika. Maana mi Tuko nikiandika uchambuzi hapa, hakuna mtu atakayehangaika sana na kuangalia nimechambuaje, maana nani anamfahamu Tuko? (hapa Tuko anawakilisha undergrounds wengine wote wa uchambuzi wa siasa). Lakini nikiona uchambuzi umeandikwa na Mwanakijiji, au Slaa, au Zitto, au Mnyika, na wengine (Nape hayupo kwenye hili kundi tafadhali, ndio maana hata post yake iliyowekwa hapa juzi sikuisoma) ambao ni members wa JF, masupastaa wa kisiasa wanaojitokeza kwenye hoja za siasa hapa, haraka sana ntakimbilia kusoma post yake na kuirudia mara mbilimbili kutafuta 'point' iko wapi...
Sasa naamini Mwanakijiji na wenzake wana uwezo wa kufanya uchambuzi wa kisayansi zaidi, kuipima CDM sasa na uwezo wake sasa na kuuhusisha na 2015 kwa kutumia matokeo ya chaguzi ndogo za udiwani. Katika uchambuzi, nitaomba waje na data na majibu ya mambo yafuatayo...
Hata hivyo, naomba wazingatie confounding factors kama vile, impacts za daftari la wapiga kura mwaka 2004 kutengenezwa, na mwaka 2009/2010 kuboreshwa, impacts za demographical changes, impacts za kushuka ama kupanda kwa vyama vingine vya kisiasa, n.k...
Naamini hii ni kazi ndogo sana kwa watu ambao wapo kwenye tasnia ya habari na uchambuzi, lakini ina umuhimu sana ku-predict matokeo na mustakabali wa taifa letu baada ya uchaguzi wa 2015.
Naamini, ikifanyika kazi hii, matokeo ya uchaguzi ujao hayatatanguliwa na vichwa vya habari kwenye magazeti; ..."Katika hali ambayo haikutarajiwa, matokeo ya uchaguzi yanaonyesha kwamba"...
Kazi kwenu

- Mwaka 2005 CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya udiwani (tuiite R), na asilimia ngapi ya kura za udiwani (tuiite S)?
- Kati ya mwaka 2005-2010, kama kulikuwa na chaguzi ndogo za udiwani, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti hivyo (T), na asilimia ngapi ya kura zote (U)?
- Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya udiwani (V), na asilimia ngapi ya kura za udiwani? (W)
- Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya viti vya ubunge (X), na asilimia ngapi ya kura za ubunge (Y)?
- Mwaka 2010, katika uchaguzi mkuu, CDM ilipata asilimia ngapi ya kura za uraisi (Z)?
- Je, R, S, T, na U, zilikuwa na correlations zozote na V, W, X, Y na Z? Kama zilikuwa na correlations, watuambie zilikuwa za aina gani, na watupatie 'factors' za hizo correlation. Kwa kutumia factors za correlations ambazo wamepata, nawaomba ma-legends hawa wakokotoe matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015.