Akimbiwa akidhaniwa ni maiti imefufuka!

Kibirizi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2011
Messages
603
Points
195

Kibirizi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2011
603 195
Mnamo miaka ya 1980 kipindi hicho wakati wa shida ya usafiri, kuna gari moja aina ya landrover 109 ambalo nyuma lilikuwa wazi yaani "pickup" lilibeba jeneza la kuzikia maiti likielekea kijiji cha Milo mkoani Iringa, wakati gari likiwa njiani kuna bwana mmoja aliomba msaada (lift) kwani naye alikuwa anaelekea kijijini huko, wakiwa njiani mvua ikaanza kunyesha basi yule bwana akaamua kuingia ndani ya lile jeneza ili kujikinga na mvua ile kubwa ambayo ilikuwa inanyesha, basi baada ya kuingia ndani ya jeneza alilifunga ili hata manyunyu ya mvua yasimpate, baada ya muda kuna watu wengine waliomba msaada basi nao wakapewa msaada na gari liliendelea na safari, punde si punde yule bwana baada ya kuhisi mvua imeisha, alilifungua lile jeneza na kutoka ili kujiunga na wenzake, wenzake baada ya kuona vile wakadhani maiti imefufuka wakaruka kutoka kwenye gari na kuanza kukimbia basi na yule bwana baada ya kuona wenzake wanakimbia na yeye alianza kuwafuata kwa kufikiri kuna hatari ambayo yeye hajaiona, kwa hivyo ikawa ni riadha (mbio) isiyo na mwisho jamaa walimbizana mpaka wakazimia wakidhani maiti inawafuata, na jamaa anata kuwa pamoja nawe. Tehe tehe!
 

Forum statistics

Threads 1,390,018
Members 528,079
Posts 34,041,036
Top