Akili za wanavyuo bhaana!

Kweli braza elimu ya mtaa ndio nguzo mama.
 
Dawa ni kufanya ajira yoyotee.. huku ukisubiri kazi ya ndoto yako.
 
Daah me ndoto yangu ilikuwa "nimalize chuo, niajiriwe, nimchukue mchumba angu tuishi nyumba nzuriiii" muda haudanganyi aisee, nilimaliza 2013 nikakosa hata tempo nikakomaa shamban mpakan kiteto na wilaya ya kongwa, nilikuwa kaz yangu kuhesabu maiti za wakulima na wafugaji kila asubuh...hatimaye nikaajiriwa, nalipa kodi nyumba ya "daraja la kati" na sina mpango wa kuoa.
 
Ni vizur kuwa na ndoto. Ila usiwe na matumaini makubwa ya kumtegemea mtu au ofisi. Bora uwe na malengo binafsi.
 
Hivi unadhania kusoma ni mchezoo, yan hapo madesa yamezidi thats why wanafunzi wengi wanakuwa na hamu ya kuajiriwa
 
kaazi kweli kweli..imebidi nishushe pumzi ndeeefu baada ya kusoma huu uzi na comments za wadau...alichokisema mleta mada ni kweli tupu kbs juu ya ndoto za wanachuo,I was one among those daylight dreamers,but now I can experience the reality of after school life. Ya Allah tusaidie!
 
Watu sio kwamba hawana fikra za kujiajiri!!! Wanazo saana, TATIZO NI MTAJI WA KUANZA KUJIAJIRI NDUGU. NINGEPATA MTU WA KUNISAIDIA KUPATA MTAJI, MBONA NINGEKUWA NIMESHA JIAJIRI
Wazo lako ndo mtaji wako,kama unajiamini ktk hicho unacho taka kukifanya anza na ulicho nacho badaye timia namba za simu ulizo nazo ktk simu yako kiimarasha mtaji wako.maana si rahisi kws mtu asiyekufahamu kukupa support kwa kitu asicho kiona.
 
Hahaha... ukiwa nje ni rahisi sana kumwona wa ndani anakosea na kumdharau. Na kusema ingekua mimi ningefanya. ila ingia wewe ufanye utaona ugumuu wake. Nahisi anajifunza jambo sasa. Akufuate umpe ushauri wa kusogeza maisha.
Nakumbuka kabla sijaweza kujiingizia kipato nilikuwa nikiwapiga ndugu na jamaa mizinga hasa mama wakiniambia hawana hela nilikuwa naona wananibania sasa ndo najua kwa nini.
Maisha yana changamoto hasa kwa mifumo ya kiafrika ambapo unafika mpaka miaka 25 hujui hata ni unahitaji kufanya maishani mwako
 
Hahahahah

Halafu wakati wa kuzunguka na bahasha hata upake lotion gani unapauka

Body spay ila bado jasho kila mahali litakutoka!
 
Hii hali si ya kufurahisha ni ya kuhudhunisha na kusikitisha pamoja na ukweli kuwa elimu inakupa uwezo wa kuzikabili changamoto lakini bado hatupaswi kuwalaumu watu kwa matarajio makubwa why? kwasababu wao hawajakuta na hali hiyo zaidi ya kuisikia kwa wale waliokumbana nayo. una haki ya kuwashangaa lakini kama una busara huwezi wacheka. kwanza mi nawapongeza pengine na wewe ungekuwa unawaza vitu vidogo vidogo usingekuwa hivyo. let people think big and rich. watafika vipi hiyo ni kazi ya kichwa. wenzetu walioendelea wana tatizo la ajira lakini sio kama kwetu. pamoja na kuwepo tatizo hilo wanathubutu kuwalipa posho raia wao na hakuna excuse na solution ndogo ndogo. lazima tukubali sio kila taaluma ni rais kujiajiri na sio kila mtu anaweza kuthubutu kuwa mjasiliamali. hii nchi ni changa na inahitaji wataalamu ili iende mbele inauma engineer,doctor,mwanasheria,mwalimu na wengine wakose ajira wakati waliopo kwenye ajira mmoja anatoa huduma kwa wananchi zaidi ya 10000. tutafika kweli hapa
 
Kumbe unajua nchi ni changa. engeneer una ajiriwa nini? Fungua kampuni za ujenzi, ufundi hauitaji ajira. Hakuna anaezuiliwa kuwa na matamanio makubwa.,ila yasiwe ya kutegemea kutoka kwa fulani au serikali au taasisi.,kuwa na matarajio yako utayofanya makubwa.
 
Kuna kijana mmoja alianza biashara kwa kutumia mtaji wa mkopo wa elimu alioupata kwa kuuza nguo za kijanja kwa wenzie na mitaani kwa washkaji zake mpaka anamaliza alikuwa ameshasimama kimtaji na hivi sasa anamiliki maduka kadhaa ya nguo na hapa jijini hajui kuomba kazi yeye anaendelea na biashara zake na ndoto zake ni kubwa ajabu.
 
Thats is what needed. Sio kumtegemea mtu makubwa fanya makubwa.
 
Kumbe ulikuwa IFM,mimi niko Block D.Natamani sana nikutafute ili unifundishe ndoto sahihi za kuota,,,,,,,,,,,,,,,huku tunaambiwa ukiwa muhasibu hukosi milioni tatu kwa mwezi,sijui ni kweli?
 
Mtoa Mada wee Ni wale wale Mkatisha watu tamaa Kila binadam Ana plans kichwani na ndoto Kwa nn umdiscourage sasa unapomsdicourage unapata nini.
 
Nimesoma Kila kitu ila kumbka kila mtu Ana malengo yake japo inategemea uwezo, nafasi,muda na mazingira na wale watu wanaomzunguka mtu husika so Acha kila stop discouraging acha apambane kulimga na hvo vigezo hapo juu then baadae muda utazungumza wenyewe.
 
Ukitegmea kuajiriwa utakuwa mtumwa maisha yako yote
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…