tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Timu 30 kutoka mataifa kama Marekani, Brazil, Ujerumani na Ureno zinajiandaa kwa mashindano ya kwanza ya dunia ya roboti, ambapo roboti hao wenye akili bandia (AI) watashiriki kwenye mechi za soka za wachezaji watano kwa upande mmoja bila msaada wa binadamu.
Soma pia: Kufika mwaka 2030 mwanadamu ataweza unganisha akili yake na akili bandia AI
Timu ya Shanhai kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China — ambao walikuwa washindi wa pili kwenye RoboCup mwezi Juni huko Brazil — walionekana wakifanya mazoezi Jumatatu.
Roboti hao wenye sensa za kuona wana uwezo wa kuona mpira, kutembea, na kujirekebisha wanapoanguka — yote kwa kutumia AI.
Ingawa roboti wengi wametengenezwa China, kila timu imeandika mfumo wake wa maamuzi kwa roboti wake.
Chanzo: Global tv