[h=4]Comments
[/h]
12345
0
#72 pedro 2011-08-18 23:54 kila bajeti ya wizara vinajitokeza vitu ambavyo misingi yake ni ufisadi,rushwa na uzembe,mhusika mkuu ni serikali,sasa wananchi tunangoja nini,peoples power ndio jibu,wenzetu india wana hanger strike,mgomo wa kula,sis tuanze na maandamano tu kuwaondoa wezi hawa,hakuna msafi
Quote
+3
#71 ahmed00 2011-08-18 21:38 NAPE MNAUYE yupo wapi kujibu tuhuma za boss wake? NAPE!kazi imekushinda au yupo likizo?
Quote
+1
#70 cowiti jl 2011-08-18 21:30 viongozi wengi wa serikali wamekosa maadili ya uongozi hivyo inaitajika ujasiri wa hali ya juu kuwatimua chakusikitisha ni pale rais anaposhindwa kusimamia serikali yake kikamilifu anapaswa kujifunza kulingana na migogoro zinazokabili nchi zingine za kiafrika
Quote
+1
#69 Nchichikwe 2011-08-18 21:17 Mhariri wa Mwananchi nakushanga sana. Kuhusu ardhi walitajwa Mkapa, Mwinyi, Macelela, Sumaye na wengine. Lakini ukurasa wako wa mbele ukaacha kumtaja Mwinyi. Uliporipoti majumuisho ya Tibaijuka ukamuacha. Je una maelekezo ya Ikulu kuwa usimtaje? Tuambieni. Nani aliuza Loliondo pamoja na marehemu Mgumia kama sio Mwinyi? Nani mke wake alitorosha dhahabu kama sio Mwinyi? Nani aliendesha serikali kiholela kama hii ya awamu ya nne kama sio Mwinyi? Nani aliyetuletea Kikwete aliyeshindwa kazi kama sio Mwinyi? Serikali mbovu ya Ali Hassan Mwinyi ndio leo imetufikisha kwa Kikwete aliyeshindwa kazi kabla ya muda wake. Kazi mbovu ya Kikwete imetufanya tushindwe kusimama kifua mbele na kuinadi CCM yetu. Tumeambiwa hivi sana ananda muislamu mwenzake aendeshe nchi na tumetajiwa Asha-Rose Migire na Hussein Mwinyi. Anaitumia turufu ya CUF kuwatisha wana CCM kuwa wasipomweka muislam upinzani na hasa CUF itachukua nchi. Mwinyi kijana wako anakusikiliza mtatupeleka pabaya.
Quote
+1
#68 MTETEZI 2011-08-18 20:38 Huyo Maige hana sifa za kuongoza wizara hiyo, yeye yupo hapo kwa kulinda maslahi ya vigogo. Angalia vitalu vya uwindaji ambavyo ni vinono amewapa wazungu na kampuni za Tanzania zimeambulia vitalu vibovu.
Kwenye misitu ndo usiseme wamepewa wazungu ndio wasimamie, hivi Watanzania hawawezi kutunza hiyo misitu kweli wakati wameilea mpaka ikafika ilipo hivi sasa, ukataji wa miti unasababishwa na serikali mbovu ya ccm kwani wananchi wanakosa nishati mbadala badala yake wanaendelea kutumia kuni na mkaa.
Kuhusu wanyamapori kuibiwa serikali ya ccm ilianza zamani kuruhusu wageni kutorosha wanyama kuanzia enzi za Mwinyi hivyo hiyo ni kawaida yao
Quote
+5
#67 NAOMBE MNISOME. 2011-08-18 20:04 Wadau wangu nendeni blog ys MICHUZI mkaangalie clip ya hotuba ya Nyerere siwafichi ni nearly one hour ila imenitoa machozi na maneno aliyotuachia yameshakuwa reversed 90 degree.Bora angeondoka ameshajua kuwa ameandaa genge la walanguzi kuingia IKULU.God bless his soul.sijui kwa nini Mungu alituzawadia mtu huyu harafu yakafuata mashetani tupu.WATANZANIA TUAMUENI MOJA.
Quote
0
#66 hahahahah 2011-08-18 19:29 safi kabisa m!!!!, yaani sema siwezi kukufaham ila laiti ningejuwa uliponingekuzaw adia zawadi, kwamaana mimi nimuathirika wahilo hawa wahifadhi hakuna mwenye imani hata kidogo baba yangu amekaa SERENGETI MIKUMI MKOMAZI TARANGIRE SAANANE, yaani mpaka nimemamliza chuo kikuu na tena tena kwamsaaada wa mjonba wangu ndio leo baba anapata kanyumba kakumstir, kiukweli hawa askari nishida kwakwenda mbele kwanza wanaishi maporini hakuna kufuga hata kuku tena kwasasa ndio balaaa yaani kuna marupurupu kibao hawalipwi yaani tena kwaubabe wamuhifadhi tu anaaamuwa,tena mimi naona hao wanaowasema nimafisadi hakuna kitu kama hicho hawajamaa mimi niongemuomba waziri aunde tume ya uchunguzi wa MALI ZA WAHIFADHI HAWJAMAA NIMATAJIRI ASIKWAMBIE MTU ninanamashaka sana na zile permit zinazokusanywa kwenye mahifadhi kama hawazichakachuw i sijuwi, MH WAZIRI MAIGE chonde chonde chunguza hawa viumbe na wasaidie hawa askari TANAPA ITADUMU
Quote
0
#65 mh!!!!! 2011-08-18 19:11 kiukweli mimi kilio changu nikwawale askari wa TANAPA, ktk wizara hii hawa viumbe ndio wanaopata tabu ya kutaka kuuwa na majangili hawa ndio wanaokoswa koswa na wanyama,hawa ndio wanaotumwa nahao mafisadi kuteka na wanyama na ikigundulika wanaofukuzwa kazi nihawa askari,chaaajab u nikwamba fedha zilizokuwa wanalipwa kama vile 9t za fedha za kuuguliwa kulazwa, fedha za doria kwasasa kunabaadhi ya hifadhi kwao imekuwa historia, wakati huohuo wahifadhi wao wakiendelea kuwa matajiri nawakizidi kujenga majumba ya kifahari na kutembelea magari kuliko waziri,ninaaami n kamwe ujangili wawanyama hautaisha kamwe kwasababu yakuwanyima na kuwanyanyasa hawa wanaowalinda hawa wanyama, haiwezekana TEMBO 10 wauwawe kwakipindi kifupi namna hiyo, MH waziri maige wacha kuagiza kama majeshini hiyo hiyo niasasi ya kiraia wafukuze watu maofisin musikilze shida za hao askari wanamaisha magumu wakati wizara yao ndio wizara tegemezi kiuchumi, yaani askari wa TANAPA mshahara nikichekesho hembu kuweni na roho ya huruma kwahawa watu, naninyi wahifadhi musilete mambo ya kpmbav ebooo zulma kama hamtakufa wapeni posho zao wakianza kuwinda ooo doria oooo patrol kwataarifa yenu hata ningekuwa mimi ningewinda mpaka nione wanangu wanaunafuu wamaisha eboooooo
Quote
+1
#64 hainiingiii 2011-08-18 18:51 chonde chonde mueshimiwa rais wetu kipenzi tunaaamini kwamba wewe unamapenzi mazuri na watz,kama kweli na wewe unatupenda nakuomba hawa wazee fukuzia mbali,mumempa makamba ukatibu mkuu amekyumbisha chama nusura kisambaratike na hiii nikutokana na mawazo yake yakizee na yakizamani,mzee kama hyuy yupo serikalini miaka 40 wanini tena,hawa ndio wanaosema TANZANIA NIWATU NA WATU WENYEWE NDIO SISI,wakikaa na mahawara yao hayo ndio maneno yao rais wangu mpendwa wanahodhi mali za watanzania kama sadaka kweli?kisa alitembelea nchi yake akapokelewa vizuri anatowa zawadi mali za watanzania,bora lawama kuliko fedheha watanzania wengi wasomi wameikimbia nchi kwa u[NENO BAYA] wa hao wazee wanaojivunia kuwepo kwao serikalin muda mrefu, mimi naaamini bado chama hakijaharibu kuihivyo,MH rais ukiona wabunge wako pia wamechoka hunabudi kukanaa nao nakusikiliza mawazo yao kwalengo la wananchi na chama kwaujumla,hawa nikuwafukuza tu nahakuna kitakacho haribika wapo vijana lakini sio kama wakina nape yule nae hana mana nje ya nchi kunavijana wengi sana wasomi na wenye uwezo ukilinganisha na kazi wanazofanya huko kwenye nchi zawatu,
Quote
0
#63 Mpechetula 2011-08-18 18:32 LUHANJO,basi lake ni la akina Mramba,Marcela na abiria wengine wa aina hiyo,kwakuwa kaachwa na basi hilo,apande la saa hii aende akapumzike hajachelewa.Kweheri babu bye!
Quote
+1
#62 Beano 2011-08-18 18:24
@Mwongozo
Si kweli. In initial stages watalindana, lakini once wamepatikana wawili watatu wa ku-join upinzani still wakiwa ndani the systema changes. Sidhani kama umeshajiuliza hali ingekuwaje kama upinzani usingekuwepo. Ikiwa leo CCM wanachekeana kiasi hiki wanapoiba na kuuza mali ya nchi, nani angetuambia ubaya wao?
Unataka kuniambia umeshasahau mashinikizo ya upinzani yalivyoifanya serikali iachane na mpango wa kuilipa DOWANS wazi wazi?
Hili suala la ukabila na udini ni dhana ya kiupotoshaji inayotumiwa na CCM kulinda kitumbua chake. Kama si mjanja wa kushtukia mambo mapema siku zote utawatukuza CCM tena wakati wanakuibia. Nikukumbushe mwaka 1995 aliyekuwa mkuu wa jeshi la polisi Omar Mahita aliutangazia umma kuwa amekamata kontena la visu na majambia na kuwa polisi wana ushahidi kuwa vimeletwa na chama fulani ili kuleta vita nchini.
Mipini ya visu hivyo ilikuwa na rangi za bendera ya CUF na hiyo ilikuwa dhana ya kuwafanya wananchi wanyonge wa fikra waone kuwa CUF=VITA.
Leo hii kwa kutambua udhaifu wa kielimu wa watu wa mikoa ya pwani, CCM imekuja na sera ya UDINI. Hilo ni jambo lisilo na ushahidi kwani ukiondoa wao CCM hamna mpinzani aliyewahi kuwa na sura ya ki-DINI. Sasa wewe umepigia mstari kuwa VYAMA VINGI LAZIMA VITATUGAWA KWA MISINGI YA UDINI, UKABILA N.K
Inanishangaza huoni namna CCM imetugawa tayari, tena katika misingi mibaya na yenye kudhalilisha. Ndani ya CCM monopolization of power tuna two inhumane classes;
WEZI NA WAIBIWAJI.
Wanachofanya CCM ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinaishia mifukoni mwao huku wengine tukiwa tumetulia. Na hapo wanakuja na dhana ya
AMANI NA UTULIVU. Tunafundishwa kuwa wanyenyekevu tunapoibiwa na hayo unayoyaita maono yatakayoletwa na upinzani ni lubricants za kulainisha akili zetu ili zisifanye kazi kwa kelele.
CCM ni janga la Kitaifa.
Quote
+1
#61 Mossad 2011-08-18 17:55 Wakati Luhanjo akiwa katibu wa wizara ya maliasili alimuweka GM wa plantation moja hivi nyanda za juu kusini kutoka kabila fulani ambao wana tabia ya kuwekana kwenye idara ya misitu, ss inakuwaje watu wengine kama mwongozo unataka kudanganya watu kuwa vyama vingi vitaleta ukabila. Hicho alichofanya yeye kilikuwa nini kama siyo ukabila?
Quote
-1
#60 mwongozo 2011-08-18 17:47 @beano
upinzani ukiwepo unafanya chama tawala walindane. wakipambana wenyewe kwa wenyewe ktk bunge la chama kimoja, maendelo hupatikana kwa kasi.
kesho nitatoa orodha ndefu inayoonesha advantages na disadvantages za single party system. nitafanya hivyo kwenye multiparty system vilevile.
msukumo unatokana na upinzani nakubali lkn wakiwa ktk chama kimoja watafanya hivyohivyo. historia inaonesha hivyo. katika disadvantages za vyama vingi ni WABUNGE WA CHAMA TAWALA HULINDANA DHIDI YA WAPINZANI.
on my side najua kuwa upinzani ni chachu ya maendeleo lkn nachukia sana UKABILA, UDINI, UKANDA nk.... vyama vingi lazima vitupeleke huko. nina ushahidi wa 100% kwa tafiti nilizo zifanya hapa nchini na afrika kwa ujumla. thats why nashauri tuwe na chama kimoja na watu washindane na kupasua mabomu humohumo. U HAV TO NOTE IT THAT: NACHUKIZWA NA UFISADI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WATENDAJI SERIKALINI.
Quote
0
#59 Mossad 2011-08-18 17:44 Wizi na Ufisadi ni dhambi ambayo hakuna kiongozi yeyote wa CCM atakayeweza kuikwepa, na hiyo inatokana na mfumo uliojengeka ndani ya Chama hicho.
Nakushangaa wewe unayejiita mwongozo unaposema kuwa vyama vingi vitatugawa kidini, kikabila na kkanda..hizo ni fikra hasi zitokanazo na mgando wa fikra na mawazo pembenuzi. Hivyo vyote ulivyovitaja havipo ndani ya serikali ya CCM?. Hujui kuwa kila siku rais wako anahubiri udini au unadhani watu hawajui ni jinsi gani ukabila unavyotawala ktk nyanja mbalimbali ndani ya serikali ya CCM?. Mfano mdogo ni hicho kizee Luhanjo wakati akiwa katibu ktk wizara ya maliasili alimuweka General Manager wa kabila lake kutoka kanda fulani hapa Tanzania ambaye alikuwa anakusanya mapato na kiasi fulani kinatumwa kwake....U don need to use microscope to see how these pple ar stealing our Resources, use ur naked eyes Guy!.
Kwa Mtanzania anayeipenda nchi yake kwa sasa sio wakati wa kuhubiri ishu za ukabila, udini wala uchama, tunatakiwa tujaribu kutizama kipi ni kikwazo kinachoporomosh a uchumi wetu kila kukicha na nini chanzo kilichopelekea tuwe ktk umaskini huu tulio nao sasa na jinsi gani ya kutatua majanga hayo.
Tusitumie hili jukwaa kusambaza chuki zisizo na msingi.
Quote
+3
#58 Beano 2011-08-18 17:18
@Mwongozo
Vyama vingi kutugawa kikabila, kidini na vinginevyo huo ni mtazamo wako. Hujui unachoshangilia kitaishia wapi. Vyama vya upinzani ndio msingi wa vuguvugu lote hili unaloliona ndani ya bunge na nje kwenye utekelezaji.
Huu uthubutu wa wabunge wa CCM katika kusema mabaya ya wenzao ni hofu ya kupoteza majimbo yao kwa wapinzani, (Hususan CHADEMA) Sasa usifikie sehemu ukasahau kuwa wanasema kwenye vikao vyao vya chama na sio panapostahili kusemea. Kwa mtazamo wangu haitoshi kushangilia kwani yataishia kusemwa ili yasikike kuwa yamesemwa na fulani lkn utekelezaji wake usiwapo.
Vyama vya upinzani ktk nchi yoyote ndio chachu na changamoto ya kuifanya serikali iwajibike. Jinamizi la CHADEMA mgongoni mwa CCM ndio linawafanya wabunge wa CCM kunyoosheana vidole na kamwe usifikiri those were their primary intentions when entering the house.
Pongezi zangu kwa wabunge wa CHADEMA kwani ni uwepo wao ndio umeamsha hamasa ya kumulika maovu miongoni mwa wana-CCM wabunge ambao hapo kabla hawakuwa na uthubutu na nia ya kufanya hivyo. Hakuna kitu CCM wanaweza kuamua bila shinikizo toka nje, na ndio maana nchi yetu inaibiwa hadi TWIGA.
Quote
12345