Akasema hawaamini tena wanawake hebu pima hii

Akasema hawaamini tena wanawake hebu pima hii

Kila kitu kinapangwa na mwenyezi mungu. tunapanga kwa vile tumezoea lakini mungu ndio muamuzi. hakuna wa kulaumiwa hapa, haikupangwa iwe. everything happen for a reason.
aisee duinia hadaa ulimwengu shujaa hakujua kuwa dunia ni ndefu na ni duara
jamani mwanamke mwenzangu amechezea dhahabu kwenye tundu la simbaaa>>>
 
Mimi mwenyewe kama nataka mwanamke huwa siangalii kama ana mtu wake , nambeba tu na kula naye maisha kwa raha zetu.
Huyo jamaa naye ni pimbi tu , kwani alimzaa yeye?
 
Nyie wanaume ni watakatifu... Huwezi oa mapema maana hata wewe tabia chafu.

Tabia chafu ndo ikoje mpendwa? na umejuaje mim nina hiyo tabia chafu? hehehee afu unaoneakana una 'mihasira' sana. Punguza gadhabu mama, manake umeng'aka as if nimekuambia wewe. Nothing seriouz here, we just killing the time na kurefresh mind as well. chill
 
Mhh mbona hii stori inafanana ya braza wa shemeji yangu.?
 
Inasikitisha sana daaaaaaaaaah kamtenda mwenzake vibaya

Hivi hawa kinadada kwanini wana roho mbaya kiasi hiki yaani unamchumba mipango ya ndoa inaendelea bado hata haya huna unaachia papuchi iliwe. Bado unataka umpotezee haki ya kuishi kiumbe kilichopatikana wakati unachepuka.
 
Kila kitu kinapangwa na mwenyezi mungu. tunapanga kwa vile tumezoea lakini mungu ndio muamuzi. hakuna wa kulaumiwa hapa, haikupangwa iwe. everything happen for a reason.

Hapana mkuu mengine unafanya mwenyewe halafu unasema ni mipango ya mungu au ilikuwa ni shetani hivi hapo mungu amehusikaje? Kwa mfano wale wanaoamini kwa bible inasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" hapo mdada kakosa maarifa/busara wala siyo mpango wa mungu
 
Mpenzi wa kweli ni FEDHA tu, unaweza kumuweka hata Uswisi, na siku utayomuhitaji utamkuta vile vile.
Mapenzi kwenye pesa, mchezo kwa mwanamke.

ndivyo unavyojidanganya? Kwan huyo jamaa aliyesalitiwa anahali ngumu kimaisha
 
Hapana mkuu mengine unafanya mwenyewe halafu unasema ni mipango ya mungu au ilikuwa ni shetani hivi hapo mungu amehusikaje? Kwa mfano wale wanaoamini kwa bible inasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" hapo mdada kakosa maarifa/busara wala siyo mpango wa mungu

Una akili sana wewe.MUNGU anasingiziwa hapa maana imeandikwa kila mtu hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.MUNGU hamjaribu mtu aisee.Tatizo tabia mbaya ya uzinzi ndo inazaa yote haya,mtu anajifanya mjanja kufanya mambo kisirisiri mwishowe anaumbuka na kuharibu kila kitu.
 
Matatizo yapo kwa wote wanawake na wanaume. Siku yakikutokea ndiyo utajua uchungu wake. Hakuna mwanadamu aliyekosa tamaa, sema wengine arobaini zao zinakuwa hazijafika bado. Hata uwe mjanja vipi linapokuja swala la mapenzi wengi ni wajinga.
 
Wanawake mlio wengi hamuaminiki na huo ndio ukweli...!

Yule aliyepanga wanawake wawili hotelini wakati vikao vya harusi vinaendelea kwa mmoja mmemuona kidume... sasa hapa "wanawake bana" hata aibu huoni. Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha... Kama huna cha kuchangia kaa kimya maana majanga ni kwa wote, hakuna mwanamke wala mwanamme. Inategemea umekutana na kubeli la aina gani.
 
Kama unacheat na najua una mtu, hakika sitakuoa hata uwe mzuri kama jini. Maana najua ipo siku utanifanyia na mimi hivyo.
Pia wanawake jueni kuwa sisi twajua kuwa mna watu twawafata for fun, mkitukubalia jueni pia tuna wetu
 
Pole yake sana. Lakini asikate tamaa, atampata tuu aliye wake. Watakaofaana.
 
Mpenzi wa kweli ni FEDHA tu, unaweza kumuweka hata Uswisi, na siku utayomuhitaji utamkuta vile vile.
Mapenzi kwenye pesa, mchezo kwa mwanamke.

hahahaa hapana bwana,, hata hela ukiweka kule kidogo ukitoa utapata imepungua wamekutoza riba riba flani hiviiii.lols
 
Habari
zenu wana Mmu?
Natumai mu wazima sasa twende kwenye stori yenyewe.
Jamaa yangu mmoja mi namuita bro kwa maana amenizidi umri na maarifa na
kipato kwa mbali.Anasema hana hamu tena ya kuoa kwa kipindi cha
karibuni na ananishauri mimi nisifanye haraka ya kuoa...namuuliza kwa
nini? anasema wanawake si viumbe wa kuwaamini hasa katika suala la
mapenzi kivipi sasa? hebu tirirka nayo mdau wa Mmu

miaka michache iliyopita alikuwa na girlfriend wake walipendana sana na
waliahidiana wakimaliza chuo basi wangeishi pamoja katika ndoa huyo bro
alikuwa kamtangulia mwaka mmoja kimasomo msichana wake hivyo yeye
alitangulia kumaliza na akajaaliwa kupata ajira katika kampuni binafsi
na mshahara mzuri tu..maisha yakawa mazuri akawa anamsapoti msichana
wake aliebaki chuoni mambo madodgomadogo ya gharama za chuo..wakaendelea
na mapenzi yao vizuri tu good time kwa sana mpaka yule msichana wake
naye akamaliza chuo.

Baada ya kumaliza Chuo yule msichana akatafuta udhamini wa kusoma
masters akabahatisha kupata chuo nchini uingereza lakin kabla ya kwenda
wapenzi hawa walishaanza vikao vya Harusi kwa maana hyo walikuwa
washatambulishana kama wachumba na wazazi wa pande zote walikuwa
wanafahamu uhusiano huu lakini sasa suala la elimu sio la kuacha
likakupita kizembe wakakubaliana yule msichana aende huko uingereza
kuanza masomo then ile likizo ndefu arudi bongo wafunge ndoa maisha
yaendelee then likizo ikiisha msichana arudi kuendelea na Masomo yake
ughaibuni...wakakubaliana hivyo na ikawa hivyo.msichana huyooo kwa
mallkia kuanza shahada yake ya uzamili.

Kama ujuavyo mapenzi ya mbali simu kwa sana ” i miss yu baby nyiingiii
ooohh! nakuombea umalize shule fasta urudi bongo tuoane oohh usijali
baby jamaani na mie ninaombea hvo” hayo ndo yalokuwa mazungumzo yao kila
siku katika kupeana moyo wa penzi lao la mbali.

Muda ukaendaaa shetani kaingilia kati,kivipi??endelea kutiririka nayo
Yule msichana a.k.a my shemu wa ukwe-e upweke ukamshinda akaanza kudate
lijamaa kule liingereza jeusi lilikuwa linampa mahaba mpaka shem
akaanza kujisahau huku yule bro akashangaa mbona mawasiliano yamepungua
simu sio kwa sana kama zamani akiuliza anaambiwa shule ishaanza kubana
yaap shule ni kweli inabana lakini pia my shem ndo alishapagawa na
mpododo wa hilo liingereza full malavidavi likizo.

Ilipokaribia demu akasema ataunganisha afanye vibarua kule asirudi
bongo anataka akirudi arudi moja kwa moja bro huku bongo alishangaa sana
huo uamuzi kwa kuwa mapatano yalikuwa aje bongo wafunge ndoa then shem
arud kuendelea na masomo mbaya zaidi vikao vya harusi vilikuwa
vinaendelea kwa matarajio kuwa binti muda si mrefu anarudi bongo kama
ilivokuwa mapatano dooohh kwa shem.

Kumbe hali ilikuwa ni kinyume alitaka aendelee kukaa UK as alikuwa
keshanogewa na penzi la wizi la huyo mdau wa UK penzi likawa penzi
mwishowe binti akapata ujauzito daaahh balaaa hilo sasa anafanyaje?
wakapatana aitoe ile mimba as yeye shem tayari ni mchumba wa mtu na
anatarajia akirud bongo ni kuolewa akaenda kwa daktari kuweka apointment
ili afanye abortion sasa sikia cha kuchekesha

Siku aloenda kufanya appointment daktari aliyekuwa zamu ni rafiki mkubwa
sana wa bro wangu yani alitokomeaga bongo kitambo sana so anaishi kule
na anafanya kazi kule ya uuguzi ile kumuona akakumbuka kuwa huyu
msichana anamjua japo yeye msichana hamjuii huyo daktari kama ana
urafiki na mchumba wake(yani bro) huku na walikuwa wakiwasiliana kwa
njia ya mitandao ya kijamii

Rafiki wa bro ambaye ndiye daktari akashangaa kwa nini msichana yule
anataka kuitoa ile mimba..akatumia akili..akampangia kuifanya hyo kazi
kesho yake ili ajue ukweli
msichana akaondoka akijua kesho yake ile mimba inaenda kutolewa
Jion ya siku ile daktari ikabidi amtwangie simu moja kwa moja bro wangu
huku bongo
baada ya salam akaanza kumlaumu ” kwa nini unataka mimba ya shem
muitoe.si mzae tu kwa kuwa mnakaribia kuoana?”

daahh swali zito sana kwa bro wangu ”kutoa mimba? mimba ipi ndugu yangu
wakati unajua mie nipo bongo na shem wako yupo huko uk anasoma?” daaahh
daktari hapa akawa ametoka nje ya miiko ya maadili ya kwa kutoa siri za
mgonjwa wake lakini kwa kuwa alishateleza ikabidi afunguke”ebana shem
kaja hapa kutoa mimba na nimempa appointment ya kesho ili nikuhoji
vizuri na ikiwezekana niwashauri msiitoe””

duuuuuuhh dunia ilianza kuwa ndogo ghafla kwa bro akajua tayari wajanja
washamtafunia mzigo wake.
Hapo hapo bro akamwendea hewan msichana wake”enhee mwanamama hebu
nieleze vizuri. unaenda kutoa mimba? mimba hiyo ni ya nani? msichana
kajifanya kubisha lakin haikusaidia kathibitishiwa hadi


ataoa tu.labda hajapata toto linapenda mbaya mtoto anamfanyia mambo
makubwa ambayo hajawaifanyiwa. afu ulifanyiwa wew si bro wako. ok atulie
soon atapata nakwambia
 
luckyline kama imenitokea mimi si nasema tu kwan kutendwa ni kitu cha ajabu au mimi ndo niwe wa kwanza kutendwa?? namuogopa nani hapa kusema ukweli?? alichapiwa mandela na dunia nzima ikajua...itakuwa mimi ?? haya kariri hvo kuwa imenitokea mimi uridhike....ya nini kuwekeana ligi kama tunalipwa hapa?? ..get off my site
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom