Akasema hawaamini tena wanawake hebu pima hii

Akasema hawaamini tena wanawake hebu pima hii

Doyi

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2011
Posts
1,809
Reaction score
2,283
Habari zenu wana Mmu?
Natumai mu wazima sasa twende kwenye stori yenyewe.
Jamaa yangu mmoja mi namuita bro kwa maana amenizidi umri na maarifa na kipato kwa mbali.Anasema hana hamu tena ya kuoa kwa kipindi cha karibuni na ananishauri mimi nisifanye haraka ya kuoa...namuuliza kwa nini? anasema wanawake si viumbe wa kuwaamini hasa katika suala la mapenzi kivipi sasa? hebu tirirka nayo mdau wa Mmu

miaka michache iliyopita alikuwa na girlfriend wake walipendana sana na waliahidiana wakimaliza chuo basi wangeishi pamoja katika ndoa huyo bro alikuwa kamtangulia mwaka mmoja kimasomo msichana wake hivyo yeye alitangulia kumaliza na akajaaliwa kupata ajira katika kampuni binafsi na mshahara mzuri tu..maisha yakawa mazuri akawa anamsapoti msichana wake aliebaki chuoni mambo madodgomadogo ya gharama za chuo..wakaendelea na mapenzi yao vizuri tu good time kwa sana mpaka yule msichana wake naye akamaliza chuo.

Baada ya kumaliza Chuo yule msichana akatafuta udhamini wa kusoma masters akabahatisha kupata chuo nchini uingereza lakin kabla ya kwenda wapenzi hawa walishaanza vikao vya Harusi kwa maana hyo walikuwa washatambulishana kama wachumba na wazazi wa pande zote walikuwa wanafahamu uhusiano huu lakini sasa suala la elimu sio la kuacha likakupita kizembe wakakubaliana yule msichana aende huko uingereza kuanza masomo then ile likizo ndefu arudi bongo wafunge ndoa maisha yaendelee then likizo ikiisha msichana arudi kuendelea na Masomo yake ughaibuni...wakakubaliana hivyo na ikawa hivyo.msichana huyooo kwa mallkia kuanza shahada yake ya uzamili.

Kama ujuavyo mapenzi ya mbali simu kwa sana " i miss yu baby nyiingiii ooohh! nakuombea umalize shule fasta urudi bongo tuoane oohh usijali baby jamaani na mie ninaombea hvo" hayo ndo yalokuwa mazungumzo yao kila siku katika kupeana moyo wa penzi lao la mbali.

Muda ukaendaaa shetani kaingilia kati,kivipi??endelea kutiririka nayo
Yule msichana a.k.a my shemu wa ukwe-e upweke ukamshinda akaanza kudate lijamaa kule liingereza jeusi lilikuwa linampa mahaba mpaka shem akaanza kujisahau huku yule bro akashangaa mbona mawasiliano yamepungua simu sio kwa sana kama zamani akiuliza anaambiwa shule ishaanza kubana yaap shule ni kweli inabana lakini pia my shem ndo alishapagawa na mpododo wa hilo liingereza full malavidavi likizo.

Ilipokaribia demu akasema ataunganisha afanye vibarua kule asirudi bongo anataka akirudi arudi moja kwa moja bro huku bongo alishangaa sana huo uamuzi kwa kuwa mapatano yalikuwa aje bongo wafunge ndoa then shem arud kuendelea na masomo mbaya zaidi vikao vya harusi vilikuwa vinaendelea kwa matarajio kuwa binti muda si mrefu anarudi bongo kama ilivokuwa mapatano dooohh kwa shem.

Kumbe hali ilikuwa ni kinyume alitaka aendelee kukaa UK as alikuwa keshanogewa na penzi la wizi la huyo mdau wa UK penzi likawa penzi mwishowe binti akapata ujauzito daaahh balaaa hilo sasa anafanyaje? wakapatana aitoe ile mimba as yeye shem tayari ni mchumba wa mtu na anatarajia akirud bongo ni kuolewa akaenda kwa daktari kuweka apointment ili afanye abortion sasa sikia cha kuchekesha

Siku aloenda kufanya appointment daktari aliyekuwa zamu ni rafiki mkubwa sana wa bro wangu yani alitokomeaga bongo kitambo sana so anaishi kule na anafanya kazi kule ya uuguzi ile kumuona akakumbuka kuwa huyu msichana anamjua japo yeye msichana hamjuii huyo daktari kama ana urafiki na mchumba wake(yani bro) huku na walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya mitandao ya kijamii

Rafiki wa bro ambaye ndiye daktari akashangaa kwa nini msichana yule anataka kuitoa ile mimba..akatumia akili..akampangia kuifanya hyo kazi kesho yake ili ajue ukweli
msichana akaondoka akijua kesho yake ile mimba inaenda kutolewa
Jion ya siku ile daktari ikabidi amtwangie simu moja kwa moja bro wangu huku bongo
baada ya salam akaanza kumlaumu " kwa nini unataka mimba ya shem muitoe.si mzae tu kwa kuwa mnakaribia kuoana?"

daahh swali zito sana kwa bro wangu "kutoa mimba? mimba ipi ndugu yangu wakati unajua mie nipo bongo na shem wako yupo huko uk anasoma?" daaahh daktari hapa akawa ametoka nje ya miiko ya maadili ya kwa kutoa siri za mgonjwa wake lakini kwa kuwa alishateleza ikabidi afunguke"ebana shem kaja hapa kutoa mimba na nimempa appointment ya kesho ili nikuhoji vizuri na ikiwezekana niwashauri msiitoe""

duuuuuuhh dunia ilianza kuwa ndogo ghafla kwa bro akajua tayari wajanja washamtafunia mzigo wake.
Hapo hapo bro akamwendea hewan msichana wake"enhee mwanamama hebu nieleze vizuri. unaenda kutoa mimba? mimba hiyo ni ya nani? msichana kajifanya kubisha lakin haikusaidia kathibitishiwa hadi hospitali,jina na hadi maongezi yalikuwaje yaaani vithibitisho vyoote akawekewa akawa hana la kujitetea akabaki kulia asijue la kufanya daahh dunia ikawa ndogo tena kwake.

Bro alikaribia kudata akaenda kwa wazazi wa msichana na kuitisha kikao cha dharula kuwa anaomba vikao vya harusi visimame na hana tena mpango wakumuoa binti yao"heee we kijana umechanganyikiwa? hapana sijachanganyikiwa nipo timamu tu""sasa tatizo nini? mpigieni simu binti yenu awaambie alichofanya"daaah wazazi ikabidi wamwendee binti hewani"mama nini tena mbona mwenzio anatuambia maneno haya? kuna nin?" binti hana cha kueleza akabaki analia baadae ikabidi awaeeelezee ukweli ulivo

Anyway nsiwachoshe ile ndoa ikawa imeyeyuka inasemekana binti aliamua kuzaa ila aliporudi tena kwa yule mchepuko wake akamtosa vibaya kuwa ye alikuwa anafurahisha ujana tu kwa maisha ya kichuochuo nothing serious baada ya miakamichache bro wangu alikuja kukutana na yule binti haijulikan kama alikatisha masomo ili alee au alimalizia masomo yake kiujumla hakuna mawasiliano full chuki ila binti anajihisi vibya kwa alichokifanya hyo ndo sababu bro hawaamini wanawake.

Anasema atakuja kuoa kama kutimiza matakwa ya kibinadamu tu na siyo kwamba anafurahia tena mahusiano sipati picha ni ndoa ngapi zina watu wenye mitizamo ya aina hii nisameheni kwa makosa ya kifasihi na kiuandishi bado nina ushamba na keyboard

Happy New Year wandugu
 
Dah yaan nimesoma huku najiweka upande wa mAmA wa huyo binti asee dunia kigeugeu wewe ukiujua huu wenzio wajua ule wanawake tunajitiaga upof na ukiziw + ububu mtu anasahau shida mlizopata yaan anapata jitu linakuja ghafla analikubalia aseee dah hakua rizq ake huyo ilokua yake iko njian inakuja awe mpole tu
 
imeandikwa ktk biblia.mwanamke mpumbavu huvunja ndoa kwa mikono yake mwenyewe.mwanaume hakutajwa sababu zaidi mwanamke ndio mmbeba mahusiano.Atafute mke mwingine
 
Very sad indeed! Na ndio maana wanaume wengine huishiaga kuwachezea na waumiza tuu
 
Mwisho wa siku binti kaja gundua kama alitema BigG kwa karanga za kuonjeshwa,, Pole yake!!
 
Mpenzi wa kweli ni FEDHA tu, unaweza kumuweka hata Uswisi, na siku utayomuhitaji utamkuta vile vile.
Mapenzi kwenye pesa, mchezo kwa mwanamke.
 
Dah yaan nimesoma huku najiweka upande wa mAmA wa huyo binti asee dunia kigeugeu wewe ukiujua huu wenzio wajua ule wanawake tunajitiaga upof na ukiziw + ububu mtu anasahau shida mlizopata yaan anapata jitu linakuja ghafla analikubalia aseee dah hakua rizq ake huyo ilokua yake iko njian inakuja awe mpole tu

Inavoelekea una m-binti wa rika hilo (above 21) na bado hajaolewa! Ataolewa tu wala usitie shaka!
 
aisee duinia hadaa ulimwengu shujaa hakujua kuwa dunia ni ndefu na ni duara
jamani mwanamke mwenzangu amechezea dhahabu kwenye tundu la simbaaa>>>
 
chezea UK weye! hata mie sitaki kuolewa! hehehehe
 
wanawake ndo walivyo! I will marry when I want
 
Yule aliyepanga wanawake wawili hotelini wakati vikao vya harusi vinaendelea kwa mmoja mmemuona kidume... sasa hapa "wanawake bana" hata aibu huoni. Kunya anye kuku, akinya bata kaharisha... Kama huna cha kuchangia kaa kimya maana majanga ni kwa wote, hakuna mwanamke wala mwanamme. Inategemea umekutana na kubeli la aina gani.
WANAWAKE bana..!!
 
Back
Top Bottom