Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,143
- 79,573
Kwema Wakuu!!
Jana nikiwa Maeneo ya Posta pale mwendokasi, kabla sijavuka ili nipande Mwendokasi, Gari jeusi nafikiri ni Toyota Fortunes ya kijivu ikasimama pembeni yangu.
Kisha ikanipigia honi kutazama alikuwa ni Carlos rafiki yangu WA siku nyingi Sana. Nilipotezana naye tangu tulipomaliza Darasa la Saba miaka 17 iliyopita. Alikuwa kabadilika mno, Sura yake na ngozi yake iliendana kabisa na Gari lile.
Basi tukasalimiana, huku akitaka kujua ninaishi wapi na nafanya shughuli gani. Siku zote Taikon ni mkaidi na ambaye hataki kuonewa huruma za kipuuzi. Nikajitetea hapo wee ungedhani ninaongea kujihami na kifo.
Baada ya mazungumzo akaniambia nipande Kama ninaelekea Makumbusho kwani yeye anaenda Bunju, nikakataa nikamwambia kuna mtu natakiwa kumuona Kimara Kwanza, kumbuka awali nilimdanganya naenda Makumbusho.
Nikamwambia ngoja niwahi Basi mwendokasi Ile inakuja, anashangaa! Akaniuliza; Bado tuu una-join the Chaini?
Nikakumbuka join the chain ya CHADEMA, nikamwambia mbona sijihusishi na mambo ya Siasa Mimi.
Basi akacheka mwenyewe,
Akaniambia nenda Bwana uka-join the chain na wenzako.
Tukaachana, nikavuka nikaenda, sasa nilipopanda mwendokasi sikupata siti kutokana ilikuwa mida ya Jioni. Nikajiunga na wenzangu kwenye laini. Hapo ndipo nikaelewa Carlos alikuwa anamaanisha nini kusema sija-join the Chain.
Sasa nakuambiaje Carlos na watu wa Aina yako;
Join the chain kwetu ni umoja
Join the chain kwetu ni ushiriano Kwa pamoja
Join the chain ni ukakamavu
Ingawaje tunapojoin the chain tunasukumana na kukanyagana Kama NG'OMBE lakini hiyo kwetu inatufanya tuwe wakakamavu.
Join the chain inatupa uvumilivu kwani wapo watu wachafu wasiooga wanaonuka tukiwa kwenye laini.
Join the Chain ndio Utanzania wenyewe. Nakuambia Carlos na Kundi lenu, Sisi ndio Watanzania.
Join the Chain wakati mwingine hutukutanisha na warembo wakali ambao tunasukumanana nao wakati wa kuingia, lakini tukisha-settle tunabadilishana namba.
Taikon kupitia join the chain nimeboresha mahusiano ya kimataifa na jumuiya za madola ambazo ni wasichana warembo lakini wapendao pesa.
Carlos na wenzako, tunajua mnatudharau pindi mkiona tunasukumana tukiwahi laini kwenye join the chain.
Nakukumbusha tuu Carlos, wapo wenzako wenye Gari Kama lako tukiwa kwenye foleni hututazama Sisi wana-join the chain Kwa macho ya Dharau, Wakituona Kama maisha yametushinda, wengine hututazama Kwa Dharau Kama vinyesi.
Carlos, najua ninyi ni rafiki Sana wa Madrafki wa barabarani Kwa sababu ninyi ndio mnawachangia vihela vya hapa na pale. Sisi wana-join the chain iwe wa mwendokasi au wadaladala za kawaida ni nadra Sana kusimamishwa na ndugu zetu Drafki.
Carlos, Yule demu niliyekuona naye kwenye Gari lako Jana ni Manzi wangu, sikujua Kama mnafahamiana, nilivyomuona alivyoketisha makalio yake na kuuegemeza mgongo wake ni Kama mtu aliyefika na kuridhishwa na mazingira Yale.
Yule Demu mara Kwa mara alikuwa aliniambia hivi; Taikon nimechoshwa na Join the Chain, kila siku kusukumana, kuparurana, alafu Mimi kushika bomba kwenye laini nachoka Sana. Si unajua Mimi ni mwanamke mrembo na laini"
Alikuwa akisema hivyo, sikatai Wadada wengi wenye matumaini ya kitoto huwapenda watu Kama wewe Carlos. Mnamagari ya kuwatembeza huku wakipulizwa na viyoyozi; muziki laini ukiwabembeleza.
Hoja zako za kusema join the chain ni uhuni kwani inazalisha Dungadunga bado sijaiafiki, watu wengi tunao-join the chain ni waungwana Sana. Kwani ninyi wenye magari ni wote mnaoyageuza magari yenu Guest Bubu na kufanya ufuska ndani yake? Jibu sasa! Hivyo Carlos uache kujumuisha watu. Sisi ni watu wenye heshima hata Kama ni fukara.
Hata hivyo nimefurahi kukuona Sana Carlos.
Acha nika-join the Chain niende kazini Mkuu.
Huyo demu nimekuachia na wala sina kinyongo. Nakuahidi mpaka jioni nikiingia kwenye Daladala nitapata demu mwingine mkali kuliko huyo. Hiyo ndio Raha ya join the chain kila kitu kipo Carlos.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Ka-join the Chain anaelekea Posta.