Akamatwa na TRA kwa kupinga Ufisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akamatwa na TRA kwa kupinga Ufisadi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kamende, Nov 12, 2008.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2008
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Amani iwe nanyi
  Habari nilizozipata hivi punde na ambazo nimeridhika kuwa zinafaa kuwekwa hapa jukwaani kwa taathira yake ni kuwa Mwl. Basil Lema ambaye ni Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Moshi (Mhe. Philemon Ndesamburo) na Mwenyekiti wa Asasi ya vijana ya kupambana na Rushwa amekamatwa, kuteshwa na mwisho kuswekwa rumande mjini Moshi kwa kile kilichodaiwa kupinga wizi unaofanywa na Brookers wa TRA kukamata magari ambayo hayajalipa Road Licence fee.

  Mwalimu Basil ameelezea kuwa jana jioni mwendo wa saa 11.30 baba yake alikamatwa akiwa anaendesha gari lake akitokea kwenye magodown yake huko Bombambuzi Moshi Mjini. Vijana waliomkamata baba huyu mwenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 70 waliongozana na mzee huyo hadi nyumbani kwake eneo la YMCA Moshi ambako walimpigia Mwl. Basil simu ili aje alipeleke gari kwenye yard ya TRA.

  Wakiwa njiani yule kijana wa TRA alimwagiza Mwl Basil kulipeleka gari kwenye ofisi za CCM mkoa wa Kilimanjaro. Mwl Basil alimwuliza kwa nini tupeleke gari CCM badala ya kulipeleka TRA? Akaambiwa kuwa TRA haina yard ya kuhifadhi magari kwa hiyo tumeomba hapa CCM tuhifadhi magari ya wahalifu.

  Leo mchana Mwl alienda TRA kujua gari ya baba yake inatakiwa kulipiwa nini na nini. Akapewa charge zote kuwa zinafikia 332,500/=. including fine ya kukamatwa kwa gari likiwa na makosa. Mwl. akalipa fedha hizo na kuandikiwa kibali cha kuchukua gari. Alipofika yard na kuwakabidhi wale maofisa waliokuwa pale hati alizopewa TRA, ndipo walipogeuka na kudai kuwa wanataka walipwe TSH. 35,000/= kwa ajili ya kuhifadhi gari toka jana hadi leo.

  kitendo cha Lema kukataa kulipa fedha hizo na kuondoa gari kimejibiwa na vurugu kubwa iliyowashirikisha maofisa wa TRA, mabrooker wa MEM Consult na mapolisi. Bw. Lema amenyakuliwa kwenye gari na kubebwa juu juu akipewa kichapo hadi akaingizwa kwenye gari la TRA na kuanza safari ya kwenda kituo cha polisi ambako amefunguliwa charge ya kutaka kuiba gari, kuwaibia maofisa wa TRA na Mabrooker 250,000 na kuwapiga vibaya watu hao wapatao 6.

  Anacholalamika Mwl. Lema
  ni Je kuna

  1. Uhalali gani wa kulipa faini (20,000/=) kwa TRA kwa kosa la kukamwatwa na gari ambayo haina Road Licence na pia ukalipe kwa Brooker 35,000/= kwa kosa hilo hilo?
   Kipengele gani kinawaruhusu TRA kum-arrest mteja wao aliyetoka kulipa ada zao zote wanazomdai
   Siri gani kwamba kwa kutolipa ada ya Brooker gari ya TRA imetumika kumkamata na kumkimbiza kituo cha Polisi?
   Sheria ipi inawaruhusu TRA kuweka Brooker ambaye atagharamiwa na mteja wake?
   
 2. C

  CottonEyeJoe JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2008
  Joined: Jan 8, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hii Kesi pelekeni kwa Mohamed Babu ataitatua chap chap... hapendagi unyanyasiaji wa aina hii....
   
 3. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Kwa mnaomjua Basil Lema ni huyu mwalimu aliyewahi kufundisha shule moja tanga inaitwa Eckernforde???Pls kama kuna mtu anamjua au mr Lema kama uko hapa tafadhali ni PM tafadhali tuongee mawili matatu.
  Aidha uwanja ndo huo tujadili wote??
   
 4. ADAM MILLINGA

  ADAM MILLINGA Senior Member

  #4
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hv hiiii mifisad mbona inatutesa sana jamaniii itatuuua hii mijitu alafu kwa kusingizia kesi ndo yenyewe mim nakwambia itaumbuliwa na mungu siku moja
   
 5. x

  xman Senior Member

  #5
  Apr 30, 2011
  Joined: Apr 27, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  yani huo ni ukatili wa hali ya juu, tanzania twaelekea wapi
   
Loading...