Ajutia kumfunga mwalimu gerezani, aomba ushauri

Ajutia kumfunga mwalimu gerezani, aomba ushauri

Hii stori nikweli ,niliisikia mitandaoni kumhusu mwalimu na huyo mwanafunzi,nidhani ni maeneo ya buchosa kabla hujafika nyehunge,jina la shule nimelisahau kidogo nadhani mleta mada hajatunga ni kweli hii kitu ilishawahi tokea miaka ya nyuma,but
 
Acha tu kaka, asilimia 80% y'a mimba ya wanafunz kwakipind hiki cha 30 years tatizo ni wanafunz wnyw. Wasio jua wataona mwalimu ndo tatizo
Wanafunzi hambaki mwalimu!

Kujiendeleza tu..kama mwalimu hacheki nao ovyo ..wanafunzi wanamuheshimu!
 
Waswahili wanasema "Cha kulanda kinazidi" Mtoto kazidisha mautundu.
Sio kwamba binti yangu ana makosa hapana, binti ameumbwa hivyo, yaani bila kufanya hivyo nilivyofanya nadhani asingemaliza chuo kikuu na Sasa hivi angekuwa analea watoto na pengine angekuwa na ukimwi
 
Mkuu Mimi ni mwalimu kwa taaluma,ogopa sana hawa watoto wanavishawishi vingi sana,mtoto wa kidato cha pili anakuwa na umri wa miaka 15-17 hivyo anakuwa ameshabarehe,lakini kuhusu mada ya huyu memba ni kipindi cha miaka kama nane nyuma,so kama ujuavyo wasukuma huwa wanachelewa sana kupeleka watoto shule ,lakini pia kumbuka hapa nilipo kwa sasa kuna had I watoto wa 21.yrs wako form one na ni wa like,acha kabisa mkuu.
 
Ilitakiwa sheria iwe na nguvu ya kuchambua mazingira ya tukio. Fikiria tu, mwanamke akipiga yowe kuwa unataka kumbaka (sio umembaka). Ukikamatwa na kesi ikaenda mahakamani kama huna jina, ndio umeenda na maji. Wanawake wamekuwa wakiitumia hii kama silaha (mimi ni muhanga wa hili japo mashuhuda waliwahi kunikingia kifua). Mimi ilikuwa sabbu ya chakula tu (food) sitasahau na tangia hapo, simuamini mwanamke yeyote zaidi ya mama, dada angu na mke wangu kwasasa. Hao wengine ni pasua kichwa tu. Sheria ifike mahala hasa kwa wanafunzi, iweke utaratibu wa aidha kumtafuta mtuhumiwa wa kweli katika kurubuni na kusababisha mimba au wote wawili waende jela. Sio mbinu nzuri ila angalau binti atajua kabisa akila chips za watu likatokea la kutokea na yeye analipa kwaaliyoyafanya. Kama nimewakwaza mnisamehe bure
 
Ilitakiwa sheria iwe na nguvu ya kuchambua mazingira ya tukio. Fikiria tu, mwanamke akipiga yowe kuwa unataka kumbaka (sio umembaka). Ukikamatwa na kesi ikaenda mahakamani kama huna jina, ndio umeenda na maji. Wanawake wamekuwa wakiitumia hii kama silaha (mimi ni muhanga wa hili japo mashuhuda waliwahi kunikingia kifua). Mimi ilikuwa sabbu ya chakula tu (food) sitasahau na tangia hapo, simuamini mwanamke yeyote zaidi ya mama, dada angu na mke wangu kwasasa. Hao wengine ni pasua kichwa tu. Sheria ifike mahala hasa kwa wanafunzi, iweke utaratibu wa aidha kumtafuta mtuhumiwa wa kweli katika kurubuni na kusababisha mimba au wote wawili waende jela. Sio mbinu nzuri ila angalau binti atajua kabisa akila chips za watu likatokea la kutokea na yeye analipa kwaaliyoyafanya. Kama nimewakwaza mnisamehe bure
Umeongea vizuri kaka,pole
 
Ni mwanamke sasa, miaka 12 iliyopita akiwa kidato cha pili katika shule moja halmashauri ya Buchosa wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Anasema akiwa kidato cha pili, alijikuta anampenda Mwalimu wake aliyekuwa anamfundisha somo la Physics

Anasema mwalimu huyo ambaye alikuwa ni kijana kati ya miaka 26 na 29 akitokea mkoani Kilimanjaro wala hakuwa na tabia za kuwatongoza wanawake wala wanafunzi, muda mwingi alikuwa anashindia majarubani na shughuli zake binafsi

Anasema "Akiwa hapo shuleni alijikuta anampenda mwalimu huyo bila sababu na alitumia mbinu kadha wa kadha kujitongoza kwa mwalimu huyo lakini mwalimu huyo hakuingia katika mtego pia alimtuma rafiki yake wake wa kike amwambie mwalimu anavyompenda"

Mwalimu huyo aliniita pembeni na kunikataza kuwa yeye hawezi kuwa na mahusiano na mwanafunzi akamsisitiza asome kwanza.

Licha ya kuniambia hivyo sikukata tamaa na kilichosababisha nisimuache kumfuatilia ni pale alipokuwa kila akija kufundisha darasani anamuita Rose, kila swali Rose jibu, kila kitu lazima atuambie Rose, nikawa nawaza huenda mwalimu ana mahusiano na Rose ndo maana ananikataa mimi, nikawa naumia sana

Siku moja niliaga nyumbani naenda part kwa mama mdogo, nilifika kwenye part ila wazo langu ni kwenda kulala kwa mwalimu usiku huo

Nilifika kwenye part lakini baada ya muda mchache,nilimuaga kaka yangu kuwa narudi nyumbani kulala

Niliondoka mpaka kwa mwalimu huyo ambaye alikuwa amepanga mtaani,nilifika kwa mwalimu nilibisha hodi, kwa muda mrefu huku nagonga mlango, ambapo mwalimu ilibidi amke afungue dirisha, kuangalia, akasema njoo huku dirishani, nikaenda dirishani, nikamwambia mwalimu, nifungulie kuna wachawi wananifukuza", Aliniuliza natoka wapi usiku huu?

Nilimwambia nifungulie nitakwambia, ndipo mwalimu alipofungua mlango nikaingia ndani, akanikaribisha ndani nikaingia nikakaa, akawa ananiuliza usiku ule natoka wapi? Nikamwambia natoka kusoma kwao Sarah ila wakati naenda nyumbani nimekutana na wachawi wamenifukuza "mwalimu akauniuliza kwa nini hukurudi kwao Sarah? Nikamwambia" walikuwa wanatokea kwao Sarah

Mwalimu akanambia, basi ngoja nikuache ulale humu ndani ili kesho uende nyumbani, mimi ngoja nikalale kwa mwalimu Peter" Nilikataaa nikamwambia siwezi kulala mwenyewe watanifuata wachawi." Akanambia ngoja nikupeleke nyumbani basi," Nikakataa kata kata "Wazazi wanaweza kukufikiria vibaya,na sasa hivi usiku sana kwetu ni mbali sana, acha tu mwalimu nilale

Mwalimu aliingia chumbani, akaniletea shuka nilale kwenye sofa, nikakubali, yeye akaenda kulala chumbani kwake, nililala kama dakika 20 hivi nikawaza nifanyeje nilale na mwalimu, nikaamka nikaenda chumbani kwa mwalimu na kumwambia" Kuna watu wananishika miguu,naogopa kulala mwenyewe, acha tu nilale na wewe mwalimu, naogopa sana"

Mwalimu alishindwa kunikatalia, tulilala kila mtu shuka lake, lakini nilipogundua mwalimu ameanza kusinzia niliweka shuka langu pembeni, nikavuta la kwake, nikamsogelea na kumkumbatia, mwalimu alishtuka akaniuliza Tatu kulikoni? Nikamwambia mwalimu nimeshindwa kuvumilia, utanikubalia tu na hali, nikavua nguo.......mwalimu akashindwa kunikatalia, ikabidi tu tufanye.

Licha ya mwalimu kuniambia iwe mwanzo na mwisho kufanya mambo hayo, kuwa amejutia kufanya kosa kubwa sana kufanya mapenzi na mwanafunzi wake" maneno hayo aliniambia kipindi anisindikiza alfajiri naenda nyumbani.

Baada ya miezi 5 nilifukuzwa shule kwa ujauzito, wazazi walinibana niwambie ujauzito nimeupata wapi,ilibidi niwambie ni mwalimu.

Kesi ikafunguliwa mahakamani, mwalimu akashtakiwa kwa ubakaji na mimba, akafungwa miaka 30 jela.

Nilitaka nimkane mwalimu ila wazazi na wanasiasa wakaingilia kati wakanitishia ikabidi nikubali

Tatu Limbe sasa yupo mtaani jijini Mwanza anatafuta vibarua ili mwanae ale na asome huku baba wa mtoto akiwa gerezani.

Anasema anajutia,mwalimu hakuwa na kosa, yeye ndiyo alikuwa na makosa.

Anataka kukata rufaa ili hukumu itenguliwe, je itawezekana?
katika andiko lako umejitahidi kujificha kuwa wewe siyo muhusika lakini ulipofika kwenye paragraph fulani ukajisahau na kuanza kujitaja jinis ulivyoenda mpaka kwa mwali. Umeanza Umalaya ukiwa mdogo sana nenda katubu Ushimen
 
Back
Top Bottom