Ajiua baada ya kufumaniwa na mke wa rafiki yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajiua baada ya kufumaniwa na mke wa rafiki yake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Babuji, Mar 11, 2009.

 1. B

  Babuji Senior Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MWANAUME mmoja anayejulikana kwa jina la Tungaraza Harison [31] amejiua kwa kunywa sumu baada ya kufumaniwa akiwa na mke wa rafiki yake kipenzi.

  Tungaraza alijiua kutokana na aibu aliyoipata kwa rafiki yake huyo ambaye alikuwa karibu naye sana katika mambo yao mengi ya kila siku.

  Marehemu alifumaniwa na rafiki yake akiwa na shemeji yake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam wakati rafiki yake huyo mwenye mke alipokuwa katika shughuli zake za kawaida.

  Inasemekana marehemu alikuwa na uhusiano na shemeji yake huyo bila rafiki yake kutambua kinachoendelea.

  Akisimulia mkasa huo,mke wa marehemu aliyejulikana kwa jina la Ester, nyumbani kwao Ukonga Madafu jijini Dar e salaam, alisema kuwa mume wake siku moja kabla ya kujinyonga siku ya Jumapili usiku wa saa mbili alirudi huku akiwa hana furaha hata kidogo.

  Mke wake huyo alisema kuwa siku hiyo usiku shemeji yake alikuja nyumbani kwao na kumpa taarifa za mumewe kutembea na mkewe hali iliyopelekea marehemu kuomba msamaha mbele ya mkewe.

  Shemeji yake huyo aliondoka nyumbani kwao bila kusema chochote kama amemsamehe au la.

  Inasemekana kutokana na aibu aliyoipata kwa mke wake na kwa rafiki yake siku ya jumatatu asubuhi alisubiria mke wake alipokwenda kazini aliamua kujiua kwa kunywa sumu.

  Ester alisema kuwa wakati anarudi kazini alimkuta mumewe akiwa kitandani amenyooka huku mapovu yakiwa yanamtoka na huku ujumbe wa “nimejiua kutokana na aibu niliyoipata, mke wangu naomba unisamehe kwa kitendo nilichokifanya cha kukutia aibu niombee samahani kwa rafiki yangu kipenzi bye” ukiwa pembeni.

  Source: Nifahamishe.com
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Phew!

  That was enough punishment to Tungaraza... but what about his family? do they deserve this? hii ni classic risk na ahdabu tunayowapa tuwapendao kwa tamaa zetu za kimwili

  Pole mke na watoto (kama wapo) na shemeji uliyemegewa, ila huyo mtuhumiwa namba mbili sijui ana hali gani
   
 3. A

  Audax JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  This is very pinful wadau,maana pamoja na aibu ambayo alihisi angeipata kwa rafiki yake,uamuzi wa kujiua haukuwa mzuri saana. Vipi huku nyuma mke na mtot? Yeye aliona aibu kwenye upande wake na je yule mwanamke alilichukulia vipi hili? Lakini pamoja na hayo yoote nawapa pole familia,ndugu,jamaa na marafilki. Kwa wale wenye tamaa,jamani muache maana mnasababisha yatima kuongezeka pasipo sabau ila tamaa za muda mfupi ambazo hazina tija kwa familia,jamii wala taifa zima. Kuwa mwaminifu.
   
 4. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Shit!

  Sijui hii tamaa itafika wapi? Hivi kweli kama unaona mkeo hafanyi vizuri unashindwa kwenda hata kwa wale wanaojiuiza mtaani ukamaliza hamu yako then ukirudi basi.

  Its a shame, pole kwa wafiwa.
   
 5. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  this is sodoma na gomora siyo tungaraza tuu sasa hivi watu wengi sana especially huko bongo nasikia wana cheat kupita kiasi tena nje nje.Mtu ana mke na watoto na anaweza kwenda kutembea na mtoto mdogo rika la mtoto wake.

  Tungaraza kama kweli alikuwa anampenda mke wake then badala ya kucheat then angeconsult kwenda couseling na mke wake inasaidia sana.or do something different na vile mlivyozoea kufanya...kwend anje ya ndoa haisaidii kitu kabisa.

  ila uamuzi aliochukua ni siyo wa kishujaa kabisa.Na atapata adhabu nyingine huko peponi.
   
 6. M

  Makfuhi Senior Member

  #6
  Mar 13, 2009
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 183
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hili ni tatizo kubwa hasa bongo; marafiki zetu wa kike hawana imani nasi na hivyo atamteka rafiki yako ili ukibadili mawazo apate pa kushika. hali hiyo huendelea mpaka mtakapooana. Kwa hiyo tungaraza huenda alianza urafiki na huyu mke wa rafiki yake hata kabla hawajaoana.
   
 7. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ni bora kajiadhibu mwenyewe kwa adhabu aliyoona anastahili
   
 8. Giro

  Giro JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2009
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 360
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Peponi?? Peponi hakuna shida ni maraha tu kwenda mbele,hopefully ulikuwa unamaanisha motoni.
   
 9. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  du! kajiadhibu vibaya sana halafu adhabu ya kibinafsi sana yaani hakufikiri familia yake kuiacha na kwamba kamwe hataonana nayo?!..
  Unapofanya kitu mara nyingi unajua mwisho wake unakuwaje, hamna siri duniani hata ipite miaka ukweli utajulikana labda iwe ya mtu peke yake!
  Naisikitikia familia yake pia aibu alioiacha japokuwa wote ni wadhambi.
   
 10. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  mama wa watu kabaki mjane kwa tamaa za kidunia, pole sana mwanamke mwenzangu!
  40 yao ilifika, na mapenzi ya hivyo utakuta yanadumu sana wana miaka ni wapenzi, rafiki alikuwa ahisi lolote but mungu wa ajabu akashuhudia ghafla.
   
 11. P

  Preacher JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2009
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mshahara wa dhambi ni mauti - ndivyo ilivyotokea kwa Marehemu Tungaraza. Hizo ndizo kazi za ibilisi - anahikikisha anakushawishi hadi unapoteza mwelekeo, unakuwa kipofu na mwishowe unatumbukia shimoni. Shida ya mwanadamu ni kuwa anafanya maovu akidhani Mungu haoni - na hata kama anaona hamwonei Mungu aibu bali mwanadamu mwenzake - angemwonea Mungu aibu, asingejiua kwani angeona aibu kwenda kumface Mungu na kitendo alichofanya - angeomba msamaha kwa Mungu pia ili apate grace na ujasiri wa kuendelea kuishi. Pole kwa watoto na mke aliyemwacha.
   
Loading...